Mimi ningeshauri, tungelinganisha au tungezungumzia hii miradi inayoendelea Kenya na Tanzania kama kweli inaleta tija na faida katika nchi na wananchi wake, kwa mfano, bado mimi ninapata wasiwasi kama ule mpango wa laptop kwa wanafunzi ni mradi wa maana na wenye tija kwa Kenya, mradi wa bandari ya Lamu pia sioni kama ni jambo la kulitekeleza kwa sasa, ninaomba kama kuna wakenya humu jamvini wanaojua faida za miradi hii miwili ukiachia faida ya kuleta sifa na kiki, wanieleze hasa faida zake za msingi miradi hii miwili.
Naomba kuwakilisha
Sent using
Jamii Forums mobile app