El Matador
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 7,132
- 3,936
Who wrote these?? OMG 😳😳😳😳😳😵
![]()
hahaha. ...dar has a long way to go
Who wrote these?? OMG 😳😳😳😳😳😵
![]()
basi umefurahi dar kuitwa fishing village.....watu wa hotbed of terror na nchi ya uhaba wa unga mnachekesha sana.hahaha. ...dar has a long way to go
kuna jam crazy hapo kasarani area
GDP ya kupika data.Look at that gap. no minerals no nothing lol. Kenya the trend setter View attachment 582124 View attachment 582125 View attachment 582126 View attachment 582127 View attachment 582129
asante kwa opinion yako,umeeleweka vizuri sana mdau.Mimi ninadhani ni vizuri tukazichambua kwa undani hizi nchi mbili yaani Tanzania na Kenya tangu kupata uhuru, Kenya ilichagua mfumo wa kibepari ambao msingi wake ni mali, Jommo Kenyatta alianza na kujenga uchumi moja kwa moja kuanzia 1963, yeye aliamini uchumi kwanza mambo mengine kama siasa ya kujenga utaifa vitafuata baadae, matokeo yake ichumi wa Kenya uliimarika sana kwa kipindi cha miongo minne yaani kuanzia 1963 Kenya ilipojipatia Uhuru hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000 uchumi ulipoanza kupungua kasi ya ukuaji wake, kwa sababu Siasa za kibepari hazimjali sana mtu wa chini, pengo la wenye nacho na wasio nacho likaendelea kukua kwa kasi, jamii ya Kenya ikagawanyika sana kwa misingi ya masikini na matajiri iliyokolezwa na ukabila na kikanda.
Kinyume chake ndicho kilichotokea Tanzania, Nyerere yeye aliamua kutoanza na uchumi, yeye alianza na siasa na utengamano wa Taifa, Siasa za ujamaa wa nyerere msingi wake mkuu ni UTU, nyerere aliamini kwenye usawa miongoni mwa binadamu, usawa wa mambo mengi ikiwemo kipato, Nyerere alipinga uonevu na dhuluma popote duniani hasa Afrika, ndiyo pale aliposema "Japo Tanzania imepata Uhuru, lakini uhuru huo hauna maana kama waafrika wengine bado wanakandamizwa", ndipo alipoamua kupigana vita kuzikomboa nchi zilizokua bado hazijapata uhuru kusini mwa Africa, kipindi chote hiki cha kujenga umoja wa kitaifa na vita vya ukombozi, uchumi wa Tanzania ulikua haukui kabisa.
Kenya kwa sababu ilianza na kujenga uchumi, hivi sasa inabidi kugeuka kujenga umoja wa kitaifa, ili kuwaleta watu pamoja kupunguza athari hasi za mfumo wa kibepari, swali la kujiuliza ni lini Kenya itaanza kazi hii ya kujenga taifa liwe pamoja, au Kenya bado inaona umoja wa kitaifa si muhimu, muhimu ni kuendelea na uchumi kama alivyofanya mzee Jommo Kenyatta?
Tanzania iliyoanza na ujenzi wa utaifa na kuweka kando ujenzi wa uchumi, je inadhani bado ni wakati wa kuendelea kujenga utaifa au inadhani kazi ya ujenzi wa utaifa imefanikiwa na sasa inabidi nchi igeukie kujenga uchumi?, na je hiyo kazi ya kujenga uchumi imeanza na kama imeanza kuna dalili zozote za mafanikio?
Naomba kuwakilisha jamvini
Sent using Jamii Forums mobile app