Simon ameweka data tafadhali zipitie, zinathibitisha kwamba hakuna siku TANESCO imezidiwa na demand ya umeme, hakuna tofauti yoyote ya Kiwango cha matumizi Kati ya kipindi cha Magufuli na hivi Sasa, tofauti ni uongozi tu umebadilika, ndio chanzo cha haya yote tunayoyaona.
Jambo Moja linanishangaza kwa sisi washabiki wa viongozi ni kwamba, pale kunapotokea jambo zuri, tunasema ni matokeo ya uongozi uliopo, ila kukitokea jambo baya hatukubali kwamba ni matokeo ya uongozi uliopo, katika hili la umeme, hakuna njia ya kumsafisha Makamba
Sent from my itel L5007 using
JamiiForums mobile app