Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Thank you bro for the latest news

Tanzania miradi ni mingi sana kuliko kenya kwa vile hatuna wapiga picha wengi na waandishi wa Habari wa kutangazia.

Nimejaribu kufukua Kwenye vyanzo vyangu
Shida ni kwamba waandishi wengi wanazipa kipaumbele habari za wasanii ambazo kimantiki nyingi ya hizo habari ni upuuzi mtupu.
 
Uhuru ameimaliza Kenya yote kwa kuuibia mashamba sasa kawaibia kile kijiwe chao cha free Wi-Fi kwa Jina la muarabu

Uhuru Park saivi ni Mali halali ya muarabu

It's so official
Poleni kwa maumivu, NMS is working well
 
😂😂😂😂😂 Tanzania na urban planning ni kama Mbingu na Nchi. Japokuwa kuna juhudi nyingi za serikali zinahitajika, Moshi kuna afadhali kwasababu ya ustaarabu wa Wachagga. Maana wameweza kujitengenezea town yenye miundombinu mizuri, Usafi, na mpangilio mzuri. Sijawahi kukaa sehemu yoyote Tanzania yenye ustaarabu kama Moshi!
Miji mingi tuu ya zamani Tanzania ilikuwa imepangika vizuri, tatizo lilianza miaka 40 hivi iliyopita, ambapo wahusika waliacha kusimamia mipango miji. Miji ambayo haikuongezeka haraka kama Tanga bado imebaki katika mpangilio.

Dar es salaam kwa mfano, sehemu nyingi tuu za nje ya mji (kwa wakati huo) zilikuwa zimepangiliwa vizuri, mfano Tandika, Chang'ombe, Mwenge Kijijini, Sinza, Magomeni na hata Kinondoni. Nje ya sehemu hizo wahusika waliaacha wananchi wajifanyie watakavyo.
 
Hivi can 1 city have more than one CBD? Unajua maana ya CBD?

Naona mpo obsessed sana na neno CBD with zero knowledge of it
Yes, one city can have more than one CBD depending on how the city is planned.

CBD in full is
C- Central (Area of Focus)
B- Bussiness( Any Activity that earns money)
D- District(Location)

So in simplified terms, CBD just means an area of a city or a town that is the economic backbone (which can be more than one) of that City. For example, most cities have more than two CBDs - Administration District, Commercial District, Financial District. All these Districts are called CBDs.
 
Hii cable stayed bridge viaduct iko kwenye final touch, soon itakamilika, nina uhakika na hii road wataikarabati mana imechoka sn hii barabara since uhuru alafu viongozi wanapita hapo wakitoka Airpot kuelekea Magogoni, inaleta view mbaya na yenye kukera machoni nna uhakika itakarabatiwa mana BRT ipo karibu na hapo hawawezi kuiacha hivyo hivyo.View attachment 2025389View attachment 2025390View attachment 2025391View attachment 2025392View attachment 2025393View attachment 2025394
Hiyo inatakiwa kujengwa wakati watakapo jenga brt false 3
 
Kuna watu wanauliza kuwa nina elimu gani Hii ni article ya Mwananchi. Msije mkasema ninawaonea.




Mwanza. “Watu wengi tunakimbilia kuishi milimani kwa sababu tunapata viwanja kwa bei nafuu; pia tunaepuka mizunguko mingi tukitaka kununua viwanja kwenye maeneo ambayo siyo ya milimani.”

Hayo ni maneno yanayosemwa na baadhi ya wakazi wanaoishi kwenye maeneo ya milimani jijini hapa.
Wakazi hao wanaeleza kuwa asilimia 75 wanaishi milimani na kwamba kwa kawaida umbali kutoka eneo la tambarare hadi kufika juu ya milima hiyo huanzia mita 50 hadi 300.
Gazeti hili lilitembelea mitaa mitano ya maeneo ya milimani mkoani hapa ambayo ni Mtaa wa Nyerere A, Nyerere B, Mbugani, Mabatini Kusini na Mabatini Kaskazini na kuzungumza na wakazi wa maeneo hayo, ambao walieleza kuwa kwa kiasi kikubwa wapo mbali na huduma za jiji.

Kwa nini watu wanakimbilia milimani
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakazi hao wanasema wanakimbilia kuishi milimani kwa sababu viwanja vinauzwa kwa bei nafuu, kwani sehemu ya kujenga chumba kimoja unapata kwa Sh150,000 hadi Sh200, 000.

Mkazi wa Mtaa wa Nyerere A, Msila Majonge na mkewe Rose Mary Majoge ambao ni wazazi wa watoto wanane, wanasema watu wengi wanakimbilia kuishi maeneo ya milimani kwa sababu ya upatikanaji wa viwanja hausumbui tofauti na maeneo mengine.

“Mimi nina familia ya watoto wanane, tunaishi huku juu kwa muda mrefu, lakini chanzo cha kuja kuishi huku ni tatizo la upatikanaji wa viwanja, ukitaka eneo zuri huwezi kupata kwa wakati, kwani kuna kuwa na mizunguko mingi, lakini huku unapata kwa muda mfupi tena kwa bei nafuu,” anasema Majoge.
Mwenyekiti wa mtaa huo, Hassan Maulid anasema, watu wanaoishi milimani wana changamoto nyingi hasa upatikanaji wa huduma za kiutawala kutoka jiji, kutokana na maeneo hayo kuwa mbali.

“Huku milimani tunaishi tu, lakini masuala ya kiutawala hakuna, Jiji wametutenga hauwezi kupata huduma yoyote ya kijamii kutoka Halmashauri kwa haraka kwa madai kuwa maeneo ya huku hayafikiki kwa urahisi,” anasema Maulid na kuongeza: “Mimi ninaishi huku tangu mwaka 2002 na niliamua kuja kwa sababu ya hali ya maisha niliyokuwa nayo kwa wakati ule, kwani nilinunua eneo kwa bei ndogo na kujenga chumba kimoja maisha yakaendelea kama kawaida.”

Anasema asilimia kubwa ya wakazi wa Jiji la Mwanza wanaishi milimani, katika mtaa wake ana kaya 1, 068, watu 6, 587 na nyumba 658, na kwamba huo ni mtaa mmoja tu.
Hali ya usafi kwenye maeneo ya milimani ikoje
Akizungumzia hali ya mazingira na usafi kwenye maeneo hayo, Athumani Hussein anasema, watu wanaoishi milimani changamoto yao kubwa ni usafi, kwani maeneo ya kutupa taka hakuna na kwamba wamekuwa wakiishi kwenye mazingira magumu.

“Licha ya kwamba watu wengi tunakimbilia kuishi huku milimani, tuna changamoto kubwa ya usafi, kwani maeneo ya kutupa taka ni ya shida kulingana na jiografia ya maeneo husika,”anasema Hussein.
Kuhusu huduma za afya
Maulidi anasema: “Kinachotusaidia watu tunaoishi milimani ni umoja tuliokuwa nao, mtu akiumwa usiku wa manani kwa kuwa vituo vya afya vipo mbali, tunapiga filimbi tunakusanyika pamoja na tunamkimbiza mgonjwa hospitali.”
Anasema kutokana na umbali uliopo kufika barabarani wamekuwa wakishirikina kwa kila jambo la maendeleo, ili kuhakikisha maisha yao yanakwenda vizuri.

Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza anasemaje?

Akizungumzia makazi hayo, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Halifa Hida anasema siyo sahihi watu kuishi kwenye maeneo ya milinani na kwamba wengi ni wavamizi kwani maeneo hayo hayajapimwa.
Anasema Jiji haliwezi kupeleka huduma za kijamii kwenye maeneo hayo, kwa kuwa wakazi wake wengi wanaishi kinyume na utaratibu.
“Naomba nikwambie kwamba watu wengi wanaoishi milimani kwa hapa Mwanza ni wavamizi, kwani Jiji hatujapima viwanja hivyo na kwamba hata huduma za kijamii ndio maana hazifiki kwenye maeneo hayo,”anasema.

NEMC wanasemaje?

Ofisa Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Mazingira Kanda ya Ziwa (Nemc), Edika Masisi anasema kwamba maeneo mengi ya milimani siyo salama, kwani hayana miti na kwamba sababu hiyo inaondoa uoto wa asili.

Masisi anasema, “Shughuli za ujenzi zinazofanywa kwenye milima mfano hapa Mwanza siyo salama, kwani uchimbaji wa mawe unaofanyika ili kujenga nyumba unasababisha kuondoa nguvu ambayo imeshikilia mawe hayo.”

Anaongeza: “Ikinyesha mvua kidogo, lazima kutatokea madhara, maeneo hayo hayana uoto wa asili, hivyo kutokana na jambo hilo inasababisha maeneo hayo kutokuwa salama kwa makazi ya binadamu.”
Anaongeza kwamba sababu kubwa inayosababisha watu wa milimani kupata madhara nyakati za mvua ni kwamba maisha yao ni ya kawaida, hivyo hata ujenzi wa nyumba zao zinakuwa siyo imara.

Akizungumzia usafi wa mazingira kwenye maeneo hayo Masisi anasema watu wanaosihi milimani wengi mazingira yao siyo salama kiafya na kwamba hayana vyoo kutokana na maeneo hayo kuwa na miamba mikubwa inayofanya zoezi la kuchimba vyoo kuwa gumu.
“Kwa kweli maeneo mengi ya milimani hakuna vyoo kwa sababu uchimbaji wake ni mgumu kutokana na miamba iliyopo, wanasubiri nyakati za mvua wanafungulia baadhi ya vyoo au wengine kujisaidia kwenye mifuko.

Kauli ya TMA

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imesema watu wanaojenga milimani wanapaswa kuchukua tahadhari, kwa kuangalia usalama wa eneo husika ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.
Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agnes Kijazi, anasema ni vyema watu kabla hawajakimbilia kujenga milimani wakaangalia usalama wa eneo husika ili kuondoa madhara ambayo yanajitokeza, kwa kuwa maeneo hayo yanachangamoto zake hasa nyakati za mvua.

“Kitu ambacho naweza kusema kwa watu wanaoishi milimani ni kwamba wanatakiwa kuchukua tahadhari kabla ya kujenga, kwani siyo mawe tu yanaweza kuleta madhara hata udongo unaweza kusababisha athari kama hautatazamwa vyema,”alisema Dk Kijazi na kuongeza:
“Mwezi Septemba mwaka huu tutatoa taarifa ya hali ya hewa ambayo itaonyesha viwango vya mvua nchi nzima, hivyo wakati huo ukifika kila mtu atafahamu kitu gani kinaendelea kwenye hali ya hewa.”

Matukio ya vifo

Hivi karibuni watu wanne walipoteza maisha baada ya kudondokewa na jiwe kwenye eneo la mabatini kutokana na mvua kubwa iliyonyesha.
Kwani hii nguvu yote ni ya nini?
 
Miji mingi tuu ya zamani Tanzania ilikuwa imepangika vizuri, tatizo lilianza miaka 40 hivi iliyopita, ambapo wahusika waliacha kusimamia mipango miji. Miji ambayo haikuongezeka haraka kama Tanga bado imebaki katika mpangilio.

Dar es salaam kwa mfano, sehemu nyingi tuu za nje ya mji (kwa wakati huo) zilikuwa zimepangiliwa vizuri, mfano Tandika, Chang'ombe, Mwenge Kijijini, Sinza, Magomeni na hata Kinondoni. Nje ya sehemu hizo wahusika waliaacha wananchi wajifanyie watakavyo.
Ni kweli sehemu nyingi karibu zote Dar zina masterplan tatizo ni ubishi wa watu kujenga Kwenye road reserve na wapimaji wachache wa viwanja na maafisa ardhi wanaopenda ela .
Watu wakija kubomolewa wanalia
 
Back
Top Bottom