Wewe nawe ni mtu wa story za vijiweni. Ila nikushauri, achaa ujuaji usio na tija.
Nikuweke tu sawa:
1. Malema alianzisha EFF kwakua alitimuliwa ANC ambapo alikua akiongoza ligi ya vijana ya ANC baada ya bifu zito na Zuma waliyempigania kushinda uenyekiti wa ANC in Mangaung na baadaye kumrecall Mbeki kuachia Urais wa South Africa.
2. Mandela hakuwa na uwezo wowote wa kuwasaidia watu weusi kiuchumi kutokana na katiba waliokuwa nayo na misimamo ya chama cha ANC.
Kwa mfano, ndani ya South Africa, kuna eneo linaitwa 'Orania' hili eneo ni wazungu tu, na hawataki kuona mtu mweusi yoyete hata Polisi mweusi kuingia huko. Na pia, wana currency yao inaitwa 'Ora', ambayo, South African Reserve Bank (SARB) wamekataa kuiendorse, wana mfumo wao wa elimu tofauti na wa South Africa, wana Redio yao na Bendera yao pia.
Orania ni kanchi ndani ya nchi, why? Kwakua inatambuliwa kikatiba kama private area.
Maswala haya yameanzia kwenye negotiations in 1980s ambapo Tanzania chini ya Nyerere ndio walikua wakiwaamuru ANC negotiators nini kiwepo na nini kisiwepo.
Ninakuwekea clip ya video hapa, umsikie Rais Thabo Mbeki akilieleza kwa ufupi hili upangaji wa makubaliano ulivyoratibiwa na Tanzania ndani ya University of South Africa (UNISA).