The best 007
JF-Expert Member
- Oct 6, 2019
- 42,480
- 98,527
Nikisomaga comments za Tony huwa nacheka sana, mana hiki kiswahili anachotumiaga huwa kinanchekesha snSwali tu, Saudi Arabia ni Jangwa na hawapandi chakula ila wanalisha watu wao wote. Wanawezaje kufanya hivyo? Hakuna Wakulima wengi huko Saudi Arabia ila wanakula na kukunywa. Saudi Arabia inaimport chakula chao karibu chote. Serikali ya Saudi Arabia ingewezaje kudistribute chakula hicho kwa raia wake bila barabara nzuri? Barabara mbaya kinaongeza makali ya njaa. Simple tu maana hata serikali ikitaka kusaidia wananchi wake, lorry za chakula zinaharibikia njiani, au zinakwama matopeni. Zinapata hitilafu kwa sababu ya barabara mbovu. Puncture na kuvunjika kwa shock absorber ni baadhi ya matatizo yanayozikumba malorry yanayosafiri kwenye barabara mbovu. Kama inachukua siku nne badala ya masaa 18, basi hata baadhi ya vyakula vitakuwa vimeharibikia njiani kwa mfano maziwa au samaki, au mboga kama sukuma wiki. Usipuuze umuhimu wa barabara ya lami kwa kupunguza makali ya njaa. Benefit yake ni indirect lakini itaonekana polepole. Pia barabara mbaya ilikuwa inawafanya Wakenya katika maeneo mengine kutotangamana na Waturkana. Sasa hivi Waturkana wanaweza kusafiri virahisi hadi maeneo mengine ya Kenya na kufanya biashara. Vile vile Wakenya kutoka maeneno mengine ya nchi wanaweza kuenda Turkana na kuinvest katika biashara kama hoteli na kadhalika. Usipuuze the economic benefits ya hii barabara. Manufaa yataonekana baada ya miaka mitano au kumi.







By the way nilikuwa cjui kama sukuma wiki ndio mboga pendwa kule Kenya, lkn Wakenya walikaa kimya wasiseme kama huwa wanategemea sukuma wiki









