Haipo Sheria kama hiyo kabisa. As a matter of fact, Sheria ya Tanzania inakataza kumfanyisha kazi mtu kwa shuruti! Hoja aliyoitumia Rais ni uzalendo na kuwa kisa alikopa hela serikalini basi kazi yake ni lazima iwe serikalini. Kwani wagonjwa kwenye hospitali binafsi sio watanzania? Na Kwa nini mtu asifate preference yake ya mazingira ya kazi?
Sijapanic Bali nimesikitishwa na hatua ya ghafla na isiyo na misingi ya kisheria ambayo Rais anataka kuichukua. Kumfutia mtu leseni ya udaktari na kuifunga hospitali binafsi aliyohamia...kisa uzalendo? Hili suala haliingii akilini. Na Ndio maana nasema kuwa Rais wetu anafanya mambo mengi mazuri lakini kuna maneno ambayo anaongea haya-reflect nafasi yake kama Kiongozi wa nchi.