Hii yote inaweza kuwa explained kitaalamu. Ukiuliza kwa heshima unaweza kujibiwa. Uchumi wenu wa Tanzania umejikita zaidi katika subsistence farming. Yaani upandaji wa vyakula kama mahindi mihogo, mboga na kadhalika. Mimea hizi hazileti faida kubwa kwa mkulima maana anaziuza tu kwenye soko la mtaani kwa bei ndogo.
Kwa upande mwingine, Agricultural sector ya Kenya imejikita zaidi kwa commercial farming yaani upandaji wa mimea kwa ajili ya kuyaexport na kupata pesa nono kutoka kwa nchi za ulaya. Hio ni kumaanisha kuwa Kenya hatujajitosheleza katika upandaji wa chakula cha kila siku na inabidi tununue kutoka kwa majirani. Hio haimaanishi kwamba tuna uchumi mdogo bali inamaanisha kwamba hatujafocuss kwa kupanda mahindi bali tunapanda kahawa, chai, avocado, maua na kadhalika kwa minajili ya kuvuna pesa nono kutoka ulaya halafu tunatumia pesa hii kununua chakula kutoka kwenu.