Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,538
- 51,270
Kwenu baba zetu maaskofu.
Nawaandikieni nikiwa na hisia nzito iliyojaa huzuni kubwa juu ya mustakbali wangu na Taifa langu na vizazi vijavyo.
Baba zetu, siku zote Taifa letu linapokuwa katika mtanzuko mzito, hamjawahi kusita kusimama thabiti na kutoa muelekeo wenye kuponya ili kuwasaidia kondoo zenu.
Wakati, Utawala ulipokana Uwepo wa ugonjwa wa maangamizi wa Covid mlisimama kidete kuuambia wazi utawala kuwa Haiwezekani useme ugonjwa haupo, wakati watawa wenu wanafariki kwa ugonjwa huo.
Wakati utawala uliopita ulipominya Demokrasia, mlitoa waraka wa Kwaresma kukemea uminywahi huo wa haki.
Sasa leo mababa askofu, Bandari yetu, lango letu kuu la uchumi linapewa watu wa nje kwa mkataba ambao ni dhahiri siyo mzuri. Mkataba huu una mapungufu mengi sana ikiwemo:
1. Hauna ukomo.
2. Scope yake ni kubwa hadi kugusa bandari za kwenye maziwa yetu.
3. Mkataba hauelezei Share zetu zisipungue ngapi.
4. Mkataba hauelezi tunaweza kujitoaje pindi mwekezaji asipokidhi masilahi yetu.
5. Mkataba huu unavunja sheria ya bandari ya mwaka 2004 na ya rasilimali ya mwaka 2017 na hata katiba ya nchi kwenye suala la bandari maana bandari ni jambo la muungano.
6. Mkataba unatishia suala la muungano wetu maana ni bandari za upande mmoja tu wa muungano ndo zinaguswa ila za upande mwingine haziguswi. Hii inaibua hisia mbaya dhidi ya muungano.
7. Mkataba hauelezei chochote juu ya matakwa ya mwekezaji kulinda haki za binadamu.
8. Mkataba Unampa veto mwekezaji juu ya masuala yetu ya uwekezaji kwenye mambo ya bandari, maana yake Sovereignity yetu remote tumempa mgeni
Kwa hoja hizo hapo juu mababa askofu, mimi binafsi sina amani, nina wasiwasi na uhuru wangu na watoto wangu na watoto wa nchi hii. Kwa hivyo nakuombeni mababa zetu maaskofu.
1. Tusaidieni kuwaambia watawala kwa waraka mzito kuwa mnakataa vipengele vibaya katika mkataba huu na kwamba watawala wakae na mwekezaji wavirekebishe.
2. Nyie kama wachungaji wema Tunawaomba mfikishe ujumbe wa tahadhari kwa waumini wenu wote nchi hii ili wajue hatari ya mkataba huu.
3. Tunawaomba ikibidi muandae hata matembezi na makongamano ya amani ili kujenga awareness ya umma juu ya suala hili.
Asanteni sana.