Barua ya wazi kwa maaskofu wa TEC: Baba zetu tuokoeni, nchi yetu inauzwa Uhuru wetu unamong'onyolewa

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,505
51,106
Kwenu baba zetu maaskofu.

Nawaandikieni nikiwa na hisia nzito iliyojaa huzuni kubwa juu ya mustakbali wangu na Taifa langu na vizazi vijavyo.

Baba zetu, siku zote Taifa letu linapokuwa katika mtanzuko mzito, hamjawahi kusita kusimama thabiti na kutoa muelekeo wenye kuponya ili kuwasaidia kondoo zenu.

Wakati, Utawala ulipokana Uwepo wa ugonjwa wa maangamizi wa Covid mlisimama kidete kuuambia wazi utawala kuwa Haiwezekani useme ugonjwa haupo, wakati watawa wenu wanafariki kwa ugonjwa huo.

Wakati utawala uliopita ulipominya Demokrasia, mlitoa waraka wa Kwaresma kukemea uminywahi huo wa haki.

Sasa leo mababa askofu, Bandari yetu, lango letu kuu la uchumi linapewa watu wa nje kwa mkataba ambao ni dhahiri siyo mzuri. Mkataba huu una mapungufu mengi sana ikiwemo:

1. Hauna ukomo.

2. Scope yake ni kubwa hadi kugusa bandari za kwenye maziwa yetu.

3. Mkataba hauelezei Share zetu zisipungue ngapi.

4. Mkataba hauelezi tunaweza kujitoaje pindi mwekezaji asipokidhi masilahi yetu.

5. Mkataba huu unavunja sheria ya bandari ya mwaka 2004 na ya rasilimali ya mwaka 2017 na hata katiba ya nchi kwenye suala la bandari maana bandari ni jambo la muungano.

6. Mkataba unatishia suala la muungano wetu maana ni bandari za upande mmoja tu wa muungano ndo zinaguswa ila za upande mwingine haziguswi. Hii inaibua hisia mbaya dhidi ya muungano.

7. Mkataba hauelezei chochote juu ya matakwa ya mwekezaji kulinda haki za binadamu.

8. Mkataba Unampa veto mwekezaji juu ya masuala yetu ya uwekezaji kwenye mambo ya bandari, maana yake Sovereignity yetu remote tumempa mgeni

Kwa hoja hizo hapo juu mababa askofu, mimi binafsi sina amani, nina wasiwasi na uhuru wangu na watoto wangu na watoto wa nchi hii. Kwa hivyo nakuombeni mababa zetu maaskofu.

1. Tusaidieni kuwaambia watawala kwa waraka mzito kuwa mnakataa vipengele vibaya katika mkataba huu na kwamba watawala wakae na mwekezaji wavirekebishe.

2. Nyie kama wachungaji wema Tunawaomba mfikishe ujumbe wa tahadhari kwa waumini wenu wote nchi hii ili wajue hatari ya mkataba huu.

3. Tunawaomba ikibidi muandae hata matembezi na makongamano ya amani ili kujenga awareness ya umma juu ya suala hili.

Asanteni sana.
 
Mpaka wateme ndoano
 
Attachments

  • 69480.jpg
    69480.jpg
    14.9 KB · Views: 7
Hii nchi si ya kidini we kenge pamoja na ukuda wako. Mnafki mpotoshaji usiye na haya. Kanisa gani hao wabibafsi na wabaguzi? Wapiga dili na wezi hao. Umesahau magunia ya pesa za EPA yalitolewa Mkombozi Bank inayomilikiwa na hilo kanisa katoliki? Hujasikia ndio waliosababisha mauaji ya halaiki Rwanda? Hao amabo maaskofu na mapadre wao ni wabakaji?

Umekosa pakushika kiasi hicho? Kanisa katoliki hawana usafi wowote wa kuishauri hii serikali, kwanza ni wabaguzi wa kidini walokubuhu wasio na na hata aibu. Maaskofu hawaoni nchi hii iangamie kulinda maslahi yao, wameona akiingia hapo mtu huru hawawezi kupitisha bidhaa zao kimagendo, wameshazoea vya bure, kubebwa.
 
Hii nchi si ya kidini we kenge pamoja na ukuda wako. Mnafki mpotoshaji usiye na haya. Kanisa gani hao wabibafsi na wabaguzi? Wapiga dili na wezi hao. Umesahau magunia ya pesa za EPA yalitolewa Mkombozi Bank inayomilikiwa na hilo kanisa katoliki? Hujasikia ndio waliosababisha mauaji ya halaiki Rwanda? Hao amabo maaskofu na mapadre wao ni wabakaji? Umekosa pakushika kiasi hicho? Kanisa katoliki hawana usafi wowote wa kuishauri hii serikali, kwanza ni wabaguzi wa kidini walokubuhu wasio na na hata aibu. Maaskofu hawaoni nchi hii iangamie kulinda maslahi yao, wameona akiingia hapo mtu huru hawawezi kupitisha bidhaa zao kimagendo, wameshazoea vya bure, kubebwa.
Wana Haqi zoote kwenye Nchi Yao...
 
Nao ni watanzania
 
Watanzania ni watu wanaoshangaza sana hasa middle class, why unaomba watu wengine wakupiganie battles zako?,why hawa maaskofu wakupiganie?,why usiingie mitaani ambako ndiko kwenye real battles za kudai haki yako?elewa Zambians, Kenyans, malawians, South Africans,Senegalese, etc etc hawa wote wamefanya street battles kudai haki yao, jasho la damu limemwagika
 
Kumbe organs of the state sio tena tatu Bali NNE...ya nne ndio hiyo TEC eeh, ngoja tuone kama wanaweza kuturudisha nyuma!
 
Watanzania ni watu wanaoshangaza sana hasa middle class, why unaomba watu wengine wakupiganie battles zako?,why hawa maaskofu wakupiganie?,why usiingie mitaani ambako ndiko kwenye real battles za kudai haki yako?elewa Zambians, Kenyans, malawians, South Africans,Senegalese, etc etc hawa wote wamefanya street battles kudai haki yao, jasho la damu limemwagika
Unanilinganisha mimi na Dude kubwa lenye mtandao mpana sana la TEC?

Nipo ground napambana pia
 
Umekosea ku-mention TEC peke yao ingeleta maana zaidi kama ungewajumuisha na BAKWATA.

Ukweli ni kwamba sisi kama nchi kuongozwa na mwanamke tena kutoka ng'ambo ya pili ni kosa la karne hakuna siku kama taifa tutaacha kulalamikia hata akiwa hayupo madarakani athari zake zitatuandama.
 
Back
Top Bottom