Barua ya wazi kwa Samia kuhusu hali ilivyo sasa baada ya waraka wa wahashamu

Chura

JF-Expert Member
Sep 22, 2009
1,345
2,296
Mods tafadhari msiunganishe huu uzi/barua wala kuufuta haya ni maonyo ya wazi kwa rais wetu mpendwa SASHA.

Niende moja kwa moja kwenye dhima ntawasalimu baadae wakubwa.

Kama ilivyo desturi leo mida ya jionii nilienda kupata zangu gahawa na kashata mitaa ya Barakuda, kilichonishtua ni kwamba sasa hivi watu hawazungumzii tena ubovu au ubora wa mikataba bali wanafungama na aliyesema ni wa dini gani kama Mkatoliki akisema mkataba ni mzuri basi wakatoliki wanaunga mkono wale wengine wanapinga vivo hivyo kwa dini nyingine. Waislamu sasa wanautetea mkataba sababu Samia ni muislamu mwenzao haijailishi una vipengele tata au la. Kule nako wakatoliki wanaupinga mkataba sababu maaskofu wao wameukataa.

Rais Samia, hali imekua mbaya sana baada ya waraka wa TEC wasio wakatoliki wamechukia wanadhani kwamba Roma inajitia ubabe na kiherehere juu ya dini nyingine hivyo wanahoji "Who on earth is TEC ", LIKE WHO are they to decide on behalf of 60M + people?. Hii imewafanya hata waislamu wenzio walio kuwa wanaupinga mkataba awali waanze kuutetea sababu ikiwa wanahisi katoliki inakujumu sababu ww ni muislamu, Sasa hivi hawakusapoti sababu ya utendaji wako bali sababu ya dini yako. Watu wamegawanyika mpambano sasa ni dhidi ya kanisa katoliki hakuna tena hoja sa hivi ni kujitutumua isionekane dini moja ina pelekesha dini nyingine lakini je nikuulize walichokisema TEC kwenye waraka kina makosa?

Upande wa pili napo hakujapoa wakatoliki wanaamini wewe na mkataba wako mmeshapoteza legitimacy hivyo uchutame na kufuata maoni ya viongozi wao maana sauti ya kwao ni ya MUNGU hakuna namna utamshawishi mkatoliki sasa akubari mkataba wako na DP world wakati wahashamu wameukataa. Sa hivi watu hawazungumzii tena ubovu au ubora wa mikataba bali wanafungama na aliyesema ni wa dini gani kama Mktoliki akisema mkataba ni mzuri basi wakatoliki wanaunga mkono wale wengine wanapinga vivo hivyo kwa dini nyingine.Waislamu sasa wanautetea mkataba sababu Samia ni muislamu mwenzao haijaishi una vipengele tata au la.Kule nako wakatoliki wanaupinga mkataba sababu maaskofu wao wameukataa haijalishi una vipengele vizuri au la, ila kwa kua RUMI IKISEMA JAMBO LIMEISHA basi hawataki kuuiskia mkataba tena.
Rais kipenzi Samia badala ya kutafuta suluhu ya kitaifa wwe unatafuta uungwaji mkono na kanisa lenye wafuasi wengi baada ya katoliki, sasa umeanza kutafuta kuungwa mkono na KKKT, Rais kipenzi tunajua kiu ya wa KKKT ni kutoa Rais maana wao wamekuwa wanalia miaka yote kuwa chini ya kivuli cha waroma huenda kwa kiu yao hii ukawapata kwenye mtego wako wakakusapoti lakini je hii itaondoa uhalisia wa hoja za TEC kuhusu mkataba wako na DP world?

Rais kipenzi Samia usiharibu historia yako ya kuwa mwanamke wa kwanza Rais Tanzania aliyeziba uwezekano wa wanawake kuja kutawala tena nchii hii.

Niseme wazi TEC wamepuyanga wameingilia siasa ilihali wao ni watu wa dini lakini walichokiongea ndio maoni ya walio wengi.

Kabla hali haijawa mbaya zaidi nakushauri uwaite viongozi wakuu wote wa dini Mufti, Kardinali, Askofu mkuu Moravian, KKKT nk ujadiliane nao kisha ukubali compromise kama kuna ulazima ili wao wakatulize mizuka ya udini iiyoibuka tuishi kama zaman kiupendo.

Rais kipenzi chetu, jeuri haina mwisho mwema jana kwenye mimbari za KKKT nimekusikia ukisema wewe utanyamaza ila umewasikia maana yake umewapuuza kwa lugha nyepesi.Tena ukasema hakuna mwenye ubavu wa kuligawa taifa hili Rais wangu kipenzi kama kuigawa TZ basi utaigawa wewe kwa kung’ang’ania ambacho kimepingwa na wengi

Kwa kukuonyesha na wao si taasisi ya mchezo katoliki imeamua kuwa, itausoma ule waraka kwa jumapili sita mfululizo kama hiyo haitoshi wamesema kwamba utasomwa kwenye jumuia zao ile kila mkatoliki ajue kwamba Mkataba sio.

Rais wangu kipenz hili swala linaweza hata kukunyima uungwaji mkono na CCM wenzio 2025 usiwe mjeuri hakuna anayekuchukia sababu ya uanamke wako bali utendaji wako wa kimaamuzi katika hili la bandari umetia dosari


“Bwana akiukataa mji waulindao wafanya kazi bure”


SURAT AL HUJURAT 49:9
 
TEC hawajapuyanga bwana mdogo...

TEC wako Proactive, hawajataka kusubiri sijui mpaka Christmass ndipo waje wazungumzie mambo ya mkataba wakati huenda ingekuwa too late...

TEC hawajaanza kutoa nyaraka leo kuhusu mambo mtambuka yahusuyo nchi yetu, ni wewe tu haujajipa muda wa kufuatilia mambo...
 
Mods tafadhari msiunganishe huu uzi/barua wala kuufuta haya ni maonyo ya wazi kwa rais wetu mpendwa SASHA.

Niende moja kwa moja kwenye dhima ntawasalimu baadae wakubwa.

Kama ilivyo desturi leo mida ya jionii nilienda kupata zangu gahawa na kashata mitaa ya Barakuda, kilichonishtua ni kwamba sasa hivi watu hawazungumzii tena ubovu au ubora wa mikataba bali wanafungama na aliyesema ni wa dini

“Bwana akiukataa mji waulindao wafanya kazi bure”
Hoja sahihi kabisa
Lakini TEC hawajatia dosari....
 
Mods tafadhari msiunganishe huu uzi/barua wala kuufuta haya ni maonyo ya wazi kwa rais wetu mpendwa SASHA.

Niende moja kwa moja kwenye dhima ntawasalimu baadae wakubwa.

kama kuna ulazima ili wao wakatulize mizuka ya udini iiyoibuka tuishi kama zaman kiupendo.


“Bwana akiukataa mji waulindao wafanya kazi bure”
Point ya samia kujisogeza KKKT wakiwa na hamu ya kupata Raisi iko wazi kabisa....

Samia kashashindwa kazi anaaza kugombanisha watu. ...maana hata mariziano na chadema yalishakufa ana ha ha kutafuta pa kufia

"If you can't convince them confuse them" nafikiri ndivyo walivyokubaliana kuwagawa wakristo
 
Mambo bado hayajapoa jamani. Hii DP World mbona inataka kutuletea balaa! Naomba wale wote mliomeza ndoano hii yenye "chambo" kitamu itemeni haraka kabla mambo hayajaharibika zaidi. Najua kuitema/kuiondoa ndoano iliyonasa kisawasawa mdomoni sio kazi rahisi. Lazima mtapata maumivu. Tafadhali Vumilieni hayo maumivu ili muinusuru Tanzania isiangamie.
 
Mods tafadhari msiunganishe huu uzi/barua wala kuufuta haya ni maonyo ya wazi kwa rais wetu mpendwa SASHA.

Niende moja kwa moja kwenye dhima ntawasalimu baadae wakubwa.

Kama ilivyo desturi leo mida ya jionii nilienda kupata zangu gahawa na kashata mitaa ya Barakuda, kilichonishtua ni kwamba sasa hivi watu hawazungumzii tena ubovu au ubora wa mikataba bali wanafungama na aliyesema ni wa dini gani kama Mkatoliki akisema mkataba ni mzuri basi wakatoliki wanaunga mkono wale wengine wanapinga vivo hivyo kwa dini nyingine. Waislamu sasa wanautetea mkataba sababu Samia ni muislamu mwenzao haijailishi una vipengele tata au
Maaskofu wetu hawawezi kukaa tena na mpumbavu wa aina yoyote. Huwezi kukaa na mpumbavu kujadili dhuluma
 
Mods tafadhari msiunganishe huu uzi/barua wala kuufuta haya ni maonyo ya wazi kwa rais wetu mpendwa SASHA.

Niende moja kwa moja kwenye dhima ntawasalimu baadae wakubwa.

Kama ilivyo desturi leo mida ya jionii nilienda kupata zangu gahawa na kashata mitaa ya Barakuda, kilichonishtua ni kwamba sasa hivi watu hawazungumzii tena ubovu au ubora wa mikataba bali wanafungama na aliyesema ni wa dini gani kama Mkatoliki akisema mkataba ni mzuri basi wakatoliki wanaunga mkono wale wengine wanapinga vivo hivyo kwa din
Shenzi type "Tena ukome kama ulivyokoma ziwa la mama Yako" alisikika RC akisema
 
Mods tafadhari msiunganishe huu uzi/barua wala kuufuta haya ni maonyo ya wazi kwa rais wetu mpendwa SASHA.

Niende moja kwa moja kwenye dhima ntawasalimu baadae wakubwa.

Kama ilivyo desturi leo mida ya jionii nilienda kupata zangu gahawa na kashata mitaa ya Barakuda, kilichonishtua ni kwamba sasa hivi watu hawazungumzii tena ubovu au ubora wa mikataba bali wanafungama na aliyesema ni wa dini gani kama Mkatoliki akisema mkataba ni mzuri basi wakatoliki wanaunga mkono wale wengine wanapinga vivo hivyo kwa

“Bwana akiukataa mji waulindao wafanya kazi bure”
Kuna sehemu umeandika TEC wamepuyanga hapo umekosea😁
 
Back
Top Bottom