Rais Dk. Mwinyi akutana na Waziri wa Mawasiliano Qatar

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Qatar, Mhe. Mohammed bin Ali Al Mannai na ujumbe wake kando ya ukumbi wa mkutano Hoteli ya Sheraton Grand Doha, Qatar leo tarehe 11 Desemba, 2023.

Katika mazungumzo yao wamegusia ushirikiano na kubadilishana uzoefu katika nyanja mbalimbali za sekta ya mawasiliano na teknolojia ya habari ikiwemo masuala yanayohusu uchumi wa kidijitali kwa maeneo watakayokubaliana kupitia mkataba wa makubaliano (MOU) ambao utaleta mageuzi ya mifumo ya kidijitali utakaoshirikisha Serikali ya Qatar na Tanzania.

Katika kikao hicho wamezungumzia mifumo ya kodi kwa njia za kidijitali kupitia sekta ya Utalii, Huduma za Afya na mapambano dhidi ya rushwa.


IMG-20231211-WA0011.jpg

IMG-20231211-WA0014.jpg
IMG-20231211-WA0016.jpg
 
Kwanini wazanzibar wanataka kutusemea watanganyika, hao Qatar ndio wafadhili wa Hamas lakini badala ya kutumia fursa hiyo kuwasihi wamwachie mateka wa Tanzania.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom