Serikali yaridhia kufuta tozo kwenye miamala ya simu

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
Naibu Waziri wa Wizara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Injinia Kundo Mathew amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la Wizara hiyo chini ya Waziri Nape Moses Nnauye la kufuta tozo katika miamala ya simu.

Naibu Waziri Kundo ameyasema haya leo July 04, 2023 akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Rukwa "Fahari ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Rais ni pamoja na kuwasikiliza Watanzania na Wananchi anaowaongoza, ndio maana ameruhusu na kutoa maelekezo ya moja kwa moja kuondoa tozo katika miamala ya simu"

"Rais wenu kipenzi Mkuu wa Nchi ameruhusu na kutoa maelekezo tozo inayotokana na miamala ya simu iondolewe, hakutokuwa na tozo kwenye miamala ya simu, ile tozo mliokuwa mnasema Rais ameshapangua huyu ndio Mwanamapinduzi halisi wa maendeleo ya Taifa letu"

"Kila Mtu kwenye Familia yake ajue kwamba kuondoka kwa tozo hii ambayo ulitakiwa ukatwe labda Tsh.Elfu 5 haujanunua mboga jamani? ni Rais mmoja tu ambaye ameona uchungu wa Watu wake na sisi tumuunge mkono" ——— Amesema Naibu Waziri Injinia Kundo.
 
Tunataka bandari zetu zote watanganyika walizopewa waarabu, mwanzo Samia aligoma alipoambiwa afute tozo, iweje leo amekubali?

Kufuta tozo hakuwezi kuwa kisingizio cha kutoa bandari zetu zote milele kwa waarabu, hapana.
 
Naibu Waziri wa Wizara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Injinia Kundo Mathew amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la Wizara hiyo chini ya Waziri Nape Moses Nnauye la kufuta tozo katika miamala ya simu.

Naibu Waziri Kundo ameyasema haya leo July 04,2023 akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Rukwa "Fahari ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Rais ni pamoja na kuwasikiliza Watanzania na Wananchi anaowaongoza, ndio maana ameruhusu na kutoa maelekezo ya moja kwa moja kuondoa tozo katika miamala ya simu"

"Rais wenu kipenzi Mkuu wa Nchi ameruhusu na kutoa maelekezo tozo inayotokana na miamala ya simu iondolewe, hakutokuwa na tozo kwenye miamala ya simu, ile tozo mliokuwa mnasema Rais ameshapangua huyu ndio Mwanamapinduzi halisi wa maendeleo ya Taifa letu"

"Kila Mtu kwenye Familia yake ajue kwamba kuondoka kwa tozo hii ambayo ulitakiwa ukatwe labda Tsh.Elfu 5 haujanunua mboga jamani? ni Rais mmoja tu ambaye ameona uchungu wa Watu wake na sisi tumuunge mkono" ——— amesema Naibu Waziri Injinia Kundo.
Bandari, bandari kwanza
 
BANDARI ZA TANGANYIKA ZIBAKIE KWA WATANGANYIKA HATUTOKI KTK RELI.
IWE MVUA IWE JUA TUNAZITAKA BANDARI ZETU KWA SHARI AU KWA HERI
 
Tatizo alilolitengeneza yeye akiumiza wananchi, anataka asifiwe kuliondoa...?

Yaani sisi wananchi tulioumizwa na tozo hizo kwa yeye kuzisaini kuwa chanzo cha mapato ya serikali, leo anapoziondoa hizo tozo kandamiizi, ccm mnatulazimisha wananchi, raisi wetu tumuone ni mwenye huruma na ni shujaa?

Acheni polojo!

Mngetueleza tu kwamba tangu mmeanza kutukandamiza kukata pesa zetu mpaka leo mnapogundua ilikuwa haramu, mmekusanya sh ngapi na zimetumika tumikaje, basi!
 
Labda akawadanganye wajinga ,tatizo si alitengeneza yeye?baada ya uchumi kudorora ndio anajifanya kafuta,halafu anapandisha bei za Saruji na kuongeza tozo kwenye mafuta ili afidie.

Halafu mnataka tumpongeze?
kama watu akili zao ni sawa na mapipa basi hili lazma washangilie.
 
Naibu Waziri wa Wizara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Injinia Kundo Mathew amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la Wizara hiyo chini ya Waziri Nape Moses Nnauye la kufuta tozo katika miamala ya simu.

Naibu Waziri Kundo ameyasema haya leo July 04,2023 akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Rukwa "Fahari ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Rais ni pamoja na kuwasikiliza Watanzania na Wananchi anaowaongoza, ndio maana ameruhusu na kutoa maelekezo ya moja kwa moja kuondoa tozo katika miamala ya simu"

"Rais wenu kipenzi Mkuu wa Nchi ameruhusu na kutoa maelekezo tozo inayotokana na miamala ya simu iondolewe, hakutokuwa na tozo kwenye miamala ya simu, ile tozo mliokuwa mnasema Rais ameshapangua huyu ndio Mwanamapinduzi halisi wa maendeleo ya Taifa letu"

"Kila Mtu kwenye Familia yake ajue kwamba kuondoka kwa tozo hii ambayo ulitakiwa ukatwe labda Tsh.Elfu 5 haujanunua mboga jamani? ni Rais mmoja tu ambaye ameona uchungu wa Watu wake na sisi tumuunge mkono" ——— amesema Naibu Waziri Injinia Kundo.
Yaani aliyekuchoma kisu akichomoa anakuwa Mzalendo? Huu ujinga kawaelezeni Mazuzu wenzenu huko Lumumba.
 
Back
Top Bottom