Balozi Sefue: Baadhi ya Wakuu wa Wilaya na Mikoa wanatumia vibaya Mamlaka yao

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Fuatilia yanayojiri kwenye Kikao cha Wajumbe wa Tume ya Haki Jinai, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais na Wahariri wa vyombo vya habari, leo Julai 20, 2024.

Kikao hiki kinafanyika Ikulu ya Dar es Salaam.

Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha taasisi za Haki Jinai nchini inaongozwa na Mwenyekiti Jaji Mohamed Othman Chande na Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Balozi Ombeni Sefue.

Wajumbe ni:
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Dk Eliezer Feleshi
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais (Utumishi) Dk Laurean Ndumbaro
Mkuu wa Jeshi la Polisi mstaafu Said Mwema
Mkuu wa Jeshi la Polisi mstaafu Balozi Ernest Mangu.
Rais mstaafu wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Dk Edward Hosea
Askari Polisi mstaafu, Saada Makungu
Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco, Omar Issa
Ofisa mwandamizi Ofisi ya Rais, Baraka Leonard
Mkurugenzi wa Utafiti katika Chuo Kikuu cha Zanzibar na Rais mstaafu wa Chama cha Wanasheria Zanzibar, Yahya Khamisi Hamad.

===​
c060438d-994d-404e-88fb-24157f1f43fb.jpg

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus akizungumza katika Mkutano wa Wajumbe wa Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai pamoja na Wahariri, Ikulu Jijini Dar es Salam tarehe 20 Julai, 2023.
a859a055-f1f8-4854-a9e3-bb37c325a3a2.jpg

Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Balozi Ombeni Sefue: Wakuu wa Mikoa na Wiaya Wanatumia vibaya Mamlaka yao.
Wajumbe wa Tume ya Haki Jinai na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais wanazungumza na Wahariri wa vyombo vya habari, Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Julai 20, 2023.

Akijibu swali kuhusu nguvu ya kikatiba waliyopewa Wakuu wa Wilaya, Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Balozi Ombeni Sefue amesema “Wananchi wamelalamika sana, kuna mahali mtu kasema Mkuu wa Wilaya anammezea mate mpenzi wako wa kike, anakuweka ndani Ijumaa na hautoki hadi Jumatatu.”

Ameongeza “Mamlaka waliyopewa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya yalikuwa na sababu lakini yametumika vibaya mno, kila saa wanatembea na Vyombo vya Dola kila wanapoenda."
42ce19aa-e581-4cce-a9af-42d3a6219293.jpg

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Mhe. Balozi Ombeni Yohana Sefue akizungumza kwenye Mkutano wa Tume hiyo pamoja na Wahariri kutoka Vyombo mbalimbali vya Habari, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Julai, 2023.

Balozi Sefue: Mkuu wa Mkoa au Wilaya akimkamata mtu anatakiwa kutoa taarifa kwa hakimu.
Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Balozi Ombeni Sefue anasema “Kuhusu mamlaka ya Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya Serikali yenyewe itafanya tathimini kama wayaondoe au yabaki lakini kama yakibaki wazingatie masharti.”

“Sheria imeeleza ukishamkamata mtu lazima utoe taarifa kwa Hakimu, je mmesikia wakifanya hivyo? Wakibaki na madaraka hayo wazingatie Sheria.”

Kuhusu Watendaji wa ngazi za chini kuwa na mamlaka ya kuagiza watu wakamatwe amesema “Wale wanyang’anywe kabisa, zamani walipewa madaraka hayo kwa kuwa Polisi walikuwa hawajafika ngazi ya Kata.”

Kibanda: Jeshi la Polisi linapaswa kuundwa upya
Mwanahabari mkongwe Absalom Kibanda akichangia mada katika mkutano wa Wajumbe wa Tume ya Haki Jinai, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais na Wahariri wa Vyombo vya Habari, amesema “Lazima tuwe wakweli Jeshi la Polisi linapaswa kuundwa upya, kwa namna gani sifahamu lakini kuwe na tahadhari na tuwe makini kwa kuwa Nchi jirani tumeona Askari Polisi wakikimbizwa na raia.”

Ameongeza “Mwaka 2014 nikiwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nilisema kuna haja ya Jeshi la Polisi kufumuliwa kwa kuwa kuna Waandishi walikamatwa na kushirikiliwa licha ya kuwa wao walienda kuripoti kitendo cha kiongozi wa kisiasa kushikiliwa.”

Kibanda: Vyombo vya habari vimekuwa Bingwa wa Kuhukumu watu na kuwapa majina yasiyofaa.
Mwanahabari mkongwe Absalom Kibanda amesema “Vyombo vya Habari vimekuwa vinara wa kuwahukumu watu, kuwapandikiza majina mabaya mbalimbali ikiwemo mafisadi, wezi wa mali za umma, wabadhirifu na wakati mwingine kuchukua maneno ya Wanasiasa na kuyaandika kama yalivyo, hivyo nadhani kuna haja ya kubadilisha mtazamo binafsi wa jamii.

Ameongeza kuwa Vyombo vya Habari vinapaswa kuingia katika Taasisi za Haki Jinai, amesema hayo wakati akichangia mada katika mkutano wa Wajumbe wa Tume ya Haki Jinai, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais na Wahariri wa Vyombo vya Habari.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji, Dkt. Eliezer Feleshi
Wakuu wa Wilaya na Mikoa waliokiuka Sheria na kuathiri watu wengine, uzoefu wangu unaonesha matukio mengi ya aina hiyo yanaishia hewani, hivyo tunaposema elimu mojawapo ni kujua mtu aliyekiuka Sheria na jinsi ya kumchukulia hatua.

Madai kuwa kuna uwezekano wa waathirika wa matukio kama hayo kupata fidia, hilo ni jambo binafsi na linatakiwa kuangaliwa kwa njia hiyo, kwamba anaenda kumshtaki nani na kama anayeshtaki ana uthibitisho wa kutosha.
56799c58-2f30-4442-a313-4d3444d593d6.jpg

Mjumbe wa Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai Ndugu Omar Issa akitolea ufafanuzi masuala mbalimbali katika Mkutano wa Tume hiyo pamoja na Wahariri kutoka Vyombo mbalimbali vya Habari, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Julai, 2023.

Mkuu wa Jeshi la Polisi mstaafu Balozi Ernest Mangu
Tumependekeza kuwe na sheria moja inayodhibiti makosa ya usalama barabarani badala ya kuwa na mamlaka tofautitofauti zinazosimamia adhabu hizo
Kuhusu dhana ya kuwa Jeshi la Polisi kuogopewa na Wananchi, tunasema sehemu ya maelekezo ni kufanya mabadiliko ili iwe karibu zaidi na Wananchi na Jeshi lielekeze sera zake katika kuzuia uhalifu badala ya kukamatana kamatana.

Amesema hoja ya kuwa mamlaka inatakiwa kufuta adhabu ya kifo ina utata kwa kuwa kuna baadhi ya mazingira ambayo mtuhumiwa akirejea mtaani jamii iliyoathirika na kosa lililofanywa inaweza kulipiza kisasi kwa mtuhumiwa.

Balozi Mangu amebainisha hayo katika mazungumzo kati ya Wajumbe wa Tume ya #HakiJinai, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais na Wahariri wa Vyombo vya Habari.

Hoja ya kuwa mamlaka inatakiwa kufuta adhabu ya kifo ina utata kwa kuwa kuna baadhi ya mazingira ambayo mtuhumiwa akirejea mtaani jamii iliyoathirika na kosa lililofanywa inaweza kulipiza kisasi kwa mtuhumiwa.

Amebainisha hayo katika mazungumzo kati ya Wajumbe wa Tume ya Haki Jinai, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais na Wahariri wa Vyombo vya Habari.
0e47db07-6795-4f7c-8b7a-4e09ee7f65c6.jpg

Mjumbe wa Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza katika Mkutano wa Tume hiyo pamoja na Wahariri kutoka Vyombo mbalimbali vya Habari, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Julai, 2023.

Dkt. Ndumbaro: Matumizi ya ving'ora
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais (Utumishi) Dkt. Laurean Ndumbaro amesema Sheria ya Usalama Barabarani imetoa mwongozo wa watu wanaotakiwa kutumia ving’ora kuwa ni Gari la Wagonjwa (Ambulance), Zimamoto na baadhi ya viongozi wakuu ambao wanaongozwa na Jeshi la Polisi.

Amesema hayo wakati akifafanua uwepo wa ving’ora vingi barabarani hali ambayo imekuwa kero kwa Wananchi wengi kusababisha wasitishe shughuli zao ili kupisha misafara ya viongozi.

8e2a69c1-d7f3-44dc-8435-8a3ed5d7e8cf.jpg

Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu ambaye pia ni Mjumbe wa Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai Balozi Mhe. Ernest Mangu akitolea ufafanuzi masuala mbalimbali yaliyoibuka kwenye mkutano kati ya Tume hiyo na Wahariri kutoka Vyombo mbalimbali vya Habari, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Julai, 2023.
cd4ef6ff-5fa5-49ec-b60c-36c3907b7e80.jpg

983e4857-84d2-4e03-8e5f-25f2609376e6.jpg

Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya Habari nchini wakiwa kwenye Mkutano kati yao na Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Julai, 2023.
 
Adhabu ya kifo isiondolewe ila itekelezwe kwa namna hii:

Tuingie makubaliano maalumu na nchi Kama China, wanaotenda jinai zinazostahili hukumu ya kifo washtakiwe na kuhukumiwa kwa Sheri za China.

Adhabu iendelee kuwepo na watu waendelee kuhukumiwa ili itengeneze hofu kwa wote wanaofanya jinai. Iendelee kuwepo hata kama utekelezaji wake ni mgumu.

Adhabu ya kifo ikiondolewa itanyima haki wote waliouawa. Amani, usalama vitadumishwa kwa kanuni ya jino kwa jino au jicho kwa jicho
 
Cc
Sukuma gang waione kwenye jalada kwa maombolezo zaidi. Ilifikia mahali mkui wa wilaya a akatuambia leseni za biashara?
 
Cc
Sukuma gang waione kwenye jalada kwa maombolezo zaidi. Ilifikia mahali mkui wa wilaya a akatuambia leseni za biashara?
Hata mliposema anaupiga mwingi mkawa mnasema anawakomesha sukuma gang kumbe amawatongoza ili awauze kwa wajomba zake!

Saa hii hakuna mtu anatamani kuiona hata sura yake labda yale mataahira yake kama kina Faizafoxy
 
Haya ni mapendekezo, ninamashaka kwenye utekelezaji.
Rejea mapendekezo ya CAG...😎
 
Fuatilia yanayojiri kwenye Kikao cha Wajumbe wa Tume ya Haki Jinai, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais na Wahariri wa vyombo vya habari, leo Julai 20, 2024.

Kikao hiki kinafanyika Ikulu ya Dar es Salaam.

Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha taasisi za Haki Jinai nchini inaongozwa na Mwenyekiti Jaji Mohamed Othman Chande na Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Balozi Ombeni Sefue.

Wajumbe:
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Dk Eliezer Feleshi
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais (Utumishi) Dk Laurean Ndumbaro
Mkuu wa Jeshi la Polisi mstaafu Said Mwema
Mkuu wa Jeshi la Polisi mstaafu Balozi Ernest Mangu.
Rais mstaafu wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Dk Edward Hosea
Askari Polisi mstaafu, Saada Makungu
Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco, Omar Issa
Ofisa mwandamizi Ofisi ya Rais, Baraka Leonard
Mkurugenzi wa Utafiti katika Chuo Kikuu cha Zanzibar na Rais mstaafu wa Chama cha Wanasheria Zanzibar, Yahya Khamisi Hamad.

===​

Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Balozi Ombeni Sefue: Wakuu wa Mikoa na Wiaya Wanatumia vibaya Mamlaka yao.
Wajumbe wa Tume ya Haki Jinai na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais wanazungumza na Wahariri wa vyombo vya habari, Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Julai 20, 2023.

Akijibu swali kuhusu nguvu ya kikatiba waliyopewa Wakuu wa Wilaya, Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Balozi Ombeni Sefue amesema “Wananchi wamelalamika sana, kuna mahali mtu kasema Mkuu wa Wilaya anammezea mate mpenzi wako wa kike, anakuweka ndani Ijumaa na hautoki hadi Jumatatu.”

Ameongeza “Mamlaka waliyopewa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya yalikuwa na sababu lakini yametumika vibaya mno, kila saa wanatembea na Vyombo vya Dola kila wanapoenda."

Balozi Sefue: Mkuu wa Mkoa au Wilaya akimkamata mtu anatakiwa kutoa taarifa kwa hakimu.
Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Balozi Ombeni Sefue anasema “Kuhusu mamlaka ya Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya Serikali yenyewe itafanya tathimini kama wayaondoe au yabaki lakini kama yakibaki wazingatie masharti.”

“Sheria imeeleza ukishamkamata mtu lazima utoe taarifa kwa Hakimu, je mmesikia wakifanya hivyo? Wakibaki na madaraka hayo wazingatie Sheria.”

Kuhusu Watendaji wa ngazi za chini kuwa na mamlaka ya kuagiza watu wakamatwe amesema “Wale wanyang’anywe kabisa, zamani walipewa madaraka hayo kwa kuwa Polisi walikuwa hawajafika ngazi ya Kata.”

Kibanda: Jeshi la Polisi linapaswa kuundwa upya
Mwanahabari mkongwe Absalom Kibanda akichangia mada katika mkutano wa Wajumbe wa Tume ya Haki Jinai, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais na Wahariri wa Vyombo vya Habari, amesema “Lazima tuwe wakweli Jeshi la Polisi linapaswa kuundwa upya, kwa namna gani sifahamu lakini kuwe na tahadhari na tuwe makini kwa kuwa Nchi jirani tumeona Askari Polisi wakikimbizwa na raia.”

Ameongeza “Mwaka 2014 nikiwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nilisema kuna haja ya Jeshi la Polisi kufumuliwa kwa kuwa kuna Waandishi walikamatwa na kushirikiliwa licha ya kuwa wao walienda kuripoti kitendo cha kiongozi wa kisiasa kushikiliwa.”

Kibanda: Vyombo vya habari vimekuwa Bingwa wa Kuhukumu watu na kuwapa majina yasiyofaa.
Mwanahabari mkongwe Absalom Kibanda amesema “Vyombo vya Habari vimekuwa vinara wa kuwahukumu watu, kuwapandikiza majina mabaya mbalimbali ikiwemo mafisadi, wezi wa mali za umma, wabadhirifu na wakati mwingine kuchukua maneno ya Wanasiasa na kuyaandika kama yalivyo, hivyo nadhani kuna haja ya kubadilisha mtazamo binafsi wa jamii.

Ameongeza kuwa Vyombo vya Habari vinapaswa kuingia katika Taasisi za Haki Jinai, amesema hayo wakati akichangia mada katika mkutano wa Wajumbe wa Tume ya #HakiJinai, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais na Wahariri wa Vyombo vya Habari.

Nyie UVCCM msitutoe kwenye reli kuhusu hoja za bandari. Sasa hivi tumestick kwenye hoja za mkataba wa kijambazi wa bandari zetu. Ni spana baada ya spana mpaka muite maji mma. Mmejimilikisha rasilimali za nchi utafikiri ni mali za familia zenu.Nyambafu!!!
 
binafsi mimi sioni tofauti ya Polisi na Jambazi au Kibaka au Mwizi wa kawaida.

kwanza kuna wakati bora hata Jambazi,Kibaka au Mwizi wa kawaida maana binafsi sijawahi kudhurika nao sana ila Polisi hata leo kuishi nafikiri ni kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu tu.

Polisi hapana 🙌

hata nikikuta anapigana na Nyoka namsaidia Nyoka
 
Tume imefanya kazi nzuri sana.
Lakini kwa vichwa vya watendaji wa Serikali ya Ccm hakuna litakalo fanyika.
Ni hivi jana tuu nimeona polisi ana leteana kiburi na rais na kumtishia ata msweka ndani. Hakuna haki jinai kwa polisi tusahau. Labda liundwe upya. Na lisimamiwe na Jwt.
 
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki Jinai, Ombeni Sefue amesema baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya wamelalamikiwa na Wananchi kutumia Mamlaka yao vibaya na kuwaweka Watu ndani hata kwasababu binafsi za kimapenzi.

Sefue ameyasema hayo leo kwenye Kikao cha Wajumbe wa Tume ya Haki Jinai, DPC na Wahariri wa Vyombo vya Habari Ikulu Dare salaam.

“Kuhusu Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kukamata ni kweli Wananchi wamelalamika sana na niwaambie ukweli tu kuna mahali Mtu kasema kwamba ‘DC anammezea mate Girlfriend wako, anakusweka ndani Ijumaa hutoki mpaka Jumatatu’, sasa tunachosema yake Mamlaka waliyopewa Ma-RC na Ma-DC yalikuwa na sababu tatizo sio wao kuwa na Mamlaka tatizo yanatumika vibaya mno”

Halafu na hivyo sasa kila saa wanatembea na Vyombo vya Dola, Kamati za Ulinzi na Usalama kwanza tunachosema wale Sheria inawatambua kwamba ni Wenyeviti wa Usalama ile component ya Ulinzi haipo lakini unaona wanaitumia halafu kila wanakoenda hata shughuli ambayo haiitaji hizi Kamati lakini wako nayo lakini hawa Watu wa hizi Kamati wana majukumu yao ya msingi sasa kama kila siku anafuatana na DC majukumu yao ya msingi watafanya saa ngapi?”

“Kama ni Polisi pengine ile gari inahitajika kwenda kupambana na Wahalifu lakini Mkubwa anasindikizana na DC wanakwenda kukagua darasa , aah pale ile Kamati haiitajiki”

“Serikali itatathmini majukumu haya kama yanaweza kuondolewa ni vizuri lakini yakibaki wazingatie masharti kwasababu Sheria inayowapa madaraka haya imeeleza ni mazingira gani DC au RC unaweza kutoa amri ya kukamata Mtu na ukishamkamata lazima utoe taarifa kwa Hakimu lakini nyie mmesikia wanafanya hivyo!?”
 
Back
Top Bottom