MISA-TAN yahuzunishwa na DC wa Bariadi, Simon Simalenga kuwafukuza waandishi wa habari kwenye kikao cha ushauri cha wilaya

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,800
Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA TAN) imeeleza kusikitishwa na kuhuzunishwa na tukio lilotokea mnamo February 19, 2024 la kufukuzwa kwa waandishi wa habari mkoani Simiyu katika kikao cha ushauri cha wilaya ya Bariadi, kilichofanywa na Mkuu wa Wilaya hiyo Bw. Simon Simarenga.

MISA TAN imefanya uchunguzi na kuukumbusha umma:

a) Majukumu ya muhimu ya waandishi wa habari ni pamoja na kuhabarisha umma juu ya mambo yanayotokea katika jamii husika hivyo kuzuia ama kupinga vyombo vya habari kufanya jukumu hilo ni kwenda kinyume na ibara ya 18 ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inayosema kila mtu anahaki ya kutafuta, kuchakata, na kutoa taarifa.

b) Ikumbukwe kuwa Mkuu wa Mkoa wa Bariadi Bw. Simon Simarenga ni mwanataaluma wa tasnia ya habari hivyo kitendo alichokifanya ni kuikosea hadhi taaluma na kuwanyima haki waandishi kutimiza wajibu wao

c) MISA TAN inaamini kuwa shambulio lolote kwa Mwandishi wa habari ni shambulio kwa Umma na kuuminya umma haki ya msingi ya kupata taarifa ya kikao cha wazi na sio kikao cha siri

d) MISA TAN inaamini kuwa kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya (DCC) ambacho waandishi walipaswa kuwepo ili kuweza kuhabarisha umma juu ya maamuzi na mambo yaliyojadiliwa kwa maslahi ya Umma. Hivyo kulikuwa hakuna ulazima kwa waandishi wa habari kutolewa nje katika kikao hicho Tena kwa kauli zenye kuhakikisha wanahabari ambayo tayari walikuwa wameanza kazi ukumbini.

e) MISA TAN inatoa wito kwa mamlaka husika kuheshimu na kusimamia majukumu na haki za waandishi wa habari wapofanya majukumu yao ya kila siku ya kuhabarisha umma bila kupata vitisho na kufanyiwa unyanyasaji wowote kwani kutokufanya hivyo kunarudisha nyuma juhudi za Mh Rais, Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha vyombo vya habari vinafanya kazi kwa uhuru bila kubugudhiwa.

f) MISA TAN inasimama pamoja na waandishi wa habari wote nchini, kutetea uhuru wa vyombo vya habari, ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari na haki ya waandishi kufanya kazi bila kubugudhiwa.

Misa= Tan.jpg
 
View attachment 2913218
ha ha eti misa tan mnamlaani simalenga,vipi nyie mlivyomfanya mfanyakazi wenu andrew marawiti.acheni unafiki wapumbavu sana nyie
 
MisaTan walikuwa vizuri sana kabla hawajaingiliwa na matapeli, kuna kikao kimoja NewAfrica Hotel, masaa yasiyozidi matatu nikajikuta na dola 150, that was 2005/2004
 
Back
Top Bottom