Rais Samia: Wakuu wa Mikoa na Wilaya fuateni utaratibu wakati wa kuvunja mikataba, mnatutia hasara

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993

“Kuna suala la mikataba,kuna amri kwamba mikoa, wilaya isimalize kuingia kwenye mikataba mpaka ofisi ya Mwanasheria Mkuu waone mikataba hiyo, lakini kuna wengine wanajifanya mafundi na kusaidi mikataba hiyo. Lakini pia kuna mikataba imefungwa kwa njia inayokubalika, lakini wakati wa kuvunja mikataba inawezekana kabisa labda mkandarasi au mwekezaji ambaye umeingia naye mkataba kwenye mradi fulani anasuasua na anatakiwa kuondoka, lakini namna ya kuvunja mkataba, sio unavunja mkataba uko saiti, mnatupa mzigo serikalini.

“Hii kwasababu mtu huyo akitoka hapo anakimbilia mahakamani, sababu kwenye mkataba wameweka njia za kuvunja mkataba, mkataba ukivunjwa kibabe, ataenda mahakamani na mahakama itampa haki, ndugu zangu tunalipa pesa nyingi sana kwa kuvunja mkataba ovyoovyo.

“Mtu hajatia hata shilingi, amenyang’anywa tu ardhi anakwenda mahakamani wakati mwingine ya kimataifa unaletewa bili kubwa ulipe, umemfanyia sivyo, umekiuka katiba yako na sheria, nk dola milioni 300 lipa, tunakuna kichwa, tunapata shida, kwahiyo uvunjaji wa mikataba ufuate taratibu zilizopo vinginevyo mnatutia hasara sana Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya.

“Inawezekana kabisa umekwenda pahali mtu anaudhi, kaingia mkataba hajaanza kazi ishapita miezi mpaka nane ishapita, lakini fuata taratibu kuvunja mkataba. Wengine ni matapeli tu, wanakuja kukuchokoza tu makusudi ukasirike ye apate kufanya lake, kwahiyo kwenye kuvunja mikataba kuweni makini.”


Rais Samia ameyasema hayo katika hafla ya kuwaapisha wakuu wa Wilaya na Mikoa leo Ikulu Dar es Salaam.
 
Nadhani ni vema akachukua Ushauri wake Mwenyewe... Mikataba / Makubaliano yake kuhusu Bandari kule Emirates alishauriana na nani ?

Ushauri wangu ni uwazi katika kila Mkataba wa Serikali kabla haujafungwa hii itatupunguzia / Kuondoa uvunjaji wa hio Mikataba...., Ni Bora tukachelewa ila tukahakikisha kile Mkataba una manufaa kwa Taifa
 
Back
Top Bottom