Tume ya Haki Jinai: Wakuu wa Mikoa/Wilaya wanatumia vibaya mamlaka ya kukamata na kuweka watu maabusu, waondolewe hayo mamlaka

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Akiwasilisha Mapendekezo mbele ya Rais Samia, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mkuu Mstaafu, Mohamed O. Chande amebainisha kuwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanalalamikiwa kutumia vibaya madaraka yao ya kukamata na kuwaweka wananchi maabusu kwa mujibu wa Kifungu cha 7 na 15 cha Sheria ya Tawala za Mikoa Sura ya 97, na mara nyingi amri hizi hutolewa bila kuzingatia masharti yaliyoanishwa katika sheria hiyo. Wadau wamependekeza mamlaka hayo yafutwe

Pili wakuu wa Mikoa/Wilaya wamekuwa wakiambatana na wajumbe wa kamati za usalama hata katika ziara ambazo hazistahili uwepo wa kamati hizo

Wakuu wa Mikoa/Wilaya kujitambulisha kama wenyeviti wa kamati ya Ulinzi na Usalama kinyume na sheria sura ya 16 inayowatambua kama wenyeviti wa kamati za usalama za mikoa au kamati za usalama za wilaya

Wakuu hao kuambatana na kamati za Usalama katika ziara zao kunasababisha kwanza hofu kwa wananchi na kuwafanya wakati mwingine washindwe kufikisha kero zao kwa kuogopa kukamatwa na pili baadhi ya majukumu yanayotakiwa kutekelezwa na wajumbe wa kamati hizo kwa nafasi zao kusimama.

Pia desturi hii inaiongezea serikali gharama kutokana na matumizi ya gharama na posho wanazolipwa watumishi kwenye ziara hizo.

 
Back
Top Bottom