Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Victoria Mwanziva amefanya ziara ya kimkakati ya ukaguzi wa Miradi ya Maji Wilayani Ludewa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Mhe. Victoria Mwanziva amefanya ziara ya kimkakati ya ukaguzi wa Miradi ya Maji Wilayani Ludewa.

Akitembelea miradi mbalimbali DC Victoria amesema kuwa Lengo la ziara hii ni kuhakikisha kuwa Wana-Ludewa wanapata huduma ya Maji bora, safi, salama na yenye kutosheleza Sambamba na kuonesha kazi kubwa inayofanywa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sekta ya Maji Ludewa.

Aidha, katika ziara hiyo imethibitika kuwa Wilaya ya Ludewa inaendelea kutekeleza miradi saba (7) ya maji yenye gharama ya Tsh. 13,866,290,252.86. Kukamilika kwa miradi hii kunalenga kuongeza huduma ya maji kutoka asimia 74.3% hadi asilimia 79.7 eneo la vijijini na asimia 100% kwa wakazi wa mji wa Ludewa.

Pia; amepokea Taarifa za miradi Wilaya nzima na kutembelea Miradi iliyopo Kata za- Mavanga, Ludewa, Iwela, na Manda katika kukagua hali ya upatikanaji wa maji na hali za miradi.

Sambamba na hapo- ametembelea Vyanzo vya maji vya Mavanga, sambamba na kumkagua mkandarasi anayelaza mabomba eneo la Nyamapinda, na kutembelea ujenzi wa ofisi ya vyombo vya usimamizi wa watumia maji ngazi ya jamii CBWSO- na kukagua vituo vya ugawaji wa maji kwenye jamii. Pia amekagua zoezi la uchimbaji visima linaloendelea kata ya Manda.

Katika hatua nyingine, DC Mwanziva amesitiza juu ya adhma ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan juu ya kumtua mama ndoo kichwani, ameasa uelimishwaji wa jamii juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji ili vinufaishe vizazi vijavyo- sambamba na kutunza miundombinu yote ya maji.

Mwisho, Mkuu wa Wilaya ya Ludewa amesisitiza wakandarasi waliopewa dhamana za kutekeleza miradi ya Maji Wilaya ya Ludewa kufanya kazi kwa ufanisi, ubora na kwenda na wakati ili kukamilisha miradi husika.

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, ameambatana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg. Sunday Deogratius- Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Ludewa.; Meneja wa RUWASA Wilaya ya Ludewa Eng. Jeremiah Maduhu; Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Ludewa Eng. Enock Ngoyinde
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-12-20 at 09.47.29.jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-20 at 09.47.29.jpeg
    178.1 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-12-20 at 09.47.29(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-20 at 09.47.29(1).jpeg
    66.6 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-12-20 at 09.47.30.jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-20 at 09.47.30.jpeg
    253 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-12-20 at 09.47.30(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-20 at 09.47.30(1).jpeg
    230 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-12-20 at 09.47.31.jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-20 at 09.47.31.jpeg
    111.8 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-12-20 at 09.47.32.jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-20 at 09.47.32.jpeg
    216 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-12-20 at 09.47.32(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-20 at 09.47.32(1).jpeg
    261 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-12-20 at 09.47.33.jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-20 at 09.47.33.jpeg
    302.3 KB · Views: 4

Similar Discussions

Back
Top Bottom