nafikri tuwewaadilifu kidogo tunapojadili haya masuala,hao waislam wasingekuja na hiyo hoja ya kutaka dini iwe ni moja ya vigezo vya kuhesabiwa na pia hata wao kama wengi walivyochangia ni kwamba wafanye utaratibu wa kujihesabu wenyewe!sababu nizionazo mie ni baada ya wakristu kutoa takwimu zinazoonyesha percentage ya watanzania kwa dini zao hivyo kuondoa hilo ambalo wao waislaam wanaamini ni cooked data na ili pia wao kujihesabu wenywewe hawaoni maantiki kwa sababu wasifanye kama walichofanya maaskofu na kuoondoa huo mkanganyiko ambao unaweza kutumiwa vibaya na baadhi ya wasiowatakia mema,jukumu hilo lifanywe na serikali tena wakati huu ambao taifa linaelekea kwenye zoezi hilo,tungeunga mkono hoja hii ilikuzipa nguvu data zilizotolewa na maaskofu kuwa wakristo ni wengi zaidi katika nchi hii hivyo pia wanastahiki kupata ruzuku kubwa kama inavyofanywa sasa hivi katika kutekeleza huduma za kijamii.
Mkuu umeanza vizuri kabisa, ila natofautiana na wewe kidogo.
Kwanza ni vema ukatambua kuwa Maaskofu hawawakilishi wakristo wote. Kuna varieties nyingi ktk dini ya kikristo, kama uko nje ya ukristo huwezi kulitambua hili. Na hili ni jambo ambalo watu wengi ama wanakwepa kulizungumza au hawalitambui. Ni vema ukasema takwimu za maaskofu na sio wakristo kwa ujumla wake.
Pili kwenye ruzuku hapo sijakuelewa vizuri, kwani hiyo ruzuku inatolewa kwa muumini mmoja mmoja au kwa taasisi. Mimi naunga mkono kabisa taasis za kiislam kupewa ruzuku, lakini sijaona mantiki ya kutoa ruzuku kwa kuzingatia wingi wa waumini. Ninavyojua mimi ruzuku inatolewa ktk taasis zenye kutoa huduma kwa jamii kama vile hospitali, mashule nk.Kwa hiyo kama ni issue ya ruzuku sijaona mantiki ya kukataa kuhesabiwa. Wanachotakiwa kufanya, nikufanya mazungumzo na serikali. Maadam wanataka kutoa huduma kwa jamii nzima, huduma ambayo haibagui imani ya mtu, mimi naona ni kheri kabisa. Maana watakuwa wanatusemea nasi tusiokuwa na dini.
Na kama ndio hivyo, ni mwendawazimu ndiye anaweza kupinga ruzuku hii, maana endapo shule hii au hospitali hii ya kiislam itawezeshwa itatoa huduma kwa jamii bila kujali dini zetu. Kwa mfano kama ninaumwa nitaenda hapo hospitali nitatibiwa.
Tatu, kama ni issue ya 'cooked data' hata mimi siungi mkono kabisa. Lakini BAKWATA nao wangekuja na data zao sahihi za sasa tupate nafasi ya kupembua kati ya pumba na mchele. Hili si jambo la kutona macho. BAKWATA wasikwepe jukumu lao la kujua idadi sahihi ya waumini wao. Si vema kuendelea kutumia data za sensa ya miaka mingi iliyopit.
Mwisho, leo hii ni wazi kuna kutoaminiana miongoni mwetu. Je, huoni hata kama kipengele hicho kitawekwa kwenye dodoso, matokeo ya sensa yatakapotolewa bado zinaweza kuibuka hisia za kutoamini matokeo hayo? Hujaona haja ya BAKWATA kutoa takwimu zao ili iwe kama reference ya kulinganisha na matokeo ya sensa ikiwa hicho kipengele kitawekwa?