BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

Ni miaka mingi sasa tangu niachane na dini niliyokuwa nayo zamani, hata sijui kama bado nahesabika kama muumini kule.

Kiukweli haihitajiki elimu ya juu sana kujua ni kwa nini sisi ni masikini. Kama leo hii jambo linalohusu mipango ya maeneleo yetu wenyewe linakwama kwa namna hii....!!!

Sipendi kuingia sana kwenye mambo hayo ya kidini, maana mimi mwenyewe sina dini. Ila ningeshauri pande zote zinazo husika (waislam na serikali) wajaribu kukaa meza moja, wajaribu kupitia sababu za msingi za madai yao- naamini watafikia muafaka.

Mimi naona hakuna haja ya kutoana macho ktk hili,sioni kama kuna tatiza ktk kupata idadi ya waislam hapa nchini. Lkn pia siamini kama BAKWATA hawana takwimu za waumini wao hadi kuitumia serikali kuwahesabia waumini wao. Tena mimi naona ni rahisi sana kupata idadi kamili ya waislam kuliko waumini wa dini zingine. Waislam ni wamoja, lakini waumini wa dini zingine ikiwemo za kienyeji si wamoja- kila dini inajiangalia yenyewe.

Sisemi kama ni vibaya watu kujua idadi ya waumini wa dini mbalimbali kitakwimu. Lakini ningeridhika zaidi ikiwa ningepata mtu wa kunisaidia kujua maslahi ya kipengele hiki kwa jamii yetu. Kwamba, ikiwa tutajua dini hii ni 80% na hii ni % kadhaa, na hii ni % kadhaa, na hii...... Hapa nataka kujua mwa mfano, mimi ambaye kwa sasa sio muislam wala mkristo nitanufaika vipi ikiwa nitajua idadi ya wenzangu ambao kila mmoja kwa sabau zake ameamua kuishi kwa staili hiyo.

Kwa hili, JK kazi anayo kwa kweli.
 
Wengi mnapindisha pindisha! Lakini lengo kuu la kujua idadi yao ni kutaka kuibadili nchi iwe ya kiislamu, wakishajua idadi yao wataanzisha lingine la kutaka ipigwe kura ya kutaka nchi iwe ya kiislamu au la na hapo ndiyo katiba mpya inafuata. Mark my words!!
Ni kweli mkuu walishawahi kudai mpaka "keki ya taifa" igawanywe kwa uwiano wa idadi ya watu kidini. Hii ni hatari sana!
 
Wafanye sensa kwenye timu za football watakuta waislam wengi, wakienda kwa graduates na wataalam watakuta wakristo wengi, distribution haiko sawa pote
 
Nakumbuka sensa iliyopita kuna jamii ya watu waligoma kuhesabiwa na wakamwambia mkuu wa mkoa kuwa ili wahesabiwe ni lazima kwanza wapelekewe nyama ya pundamilia na gunia tatu za bange,kwa mtazamo wangu angalau naona walikuwa na madai ya msingi kulikn hawa wanaogoma sasa!
 
Sensa ya mwaka 1957 ya kikoloni kipengele cha kuonesha dini kilikuwepo na ndio kinachoonesha takwimu waislamu wangapi na wakristo wangapi, na ukiangalia mwaka huo 1957 waislamu walikuwa ni 65%.

Baada ya hapo sensa zote zilizofuata kipengele cha dini kilifutwa; ajabu leo hii watu wanasema wakristo wapo wengi kuliko waislamu kwa takwimu zipi ikiwa kipengele cha kuorodhesha watu dini zao hakipo.

Pili ni kwanini wanaogopa kuhesabu watu kwa kutumia kigezo cha dini? Wengi watasema wanaogopa udini, hii hoja ni dhaifu maana nchi nyingi duniani sensa zinahebabiwa kwa mtindo wakujua idadi ya watu na dini zao ni asilimia ngapi katika nchi hizo.
Kama ulichokiandika ndicho unachomaanisha inaelekea haukusoma na kama umesoma inaelekea ulikuwa unakariri na hauna ufahamu wa mambo. Jitahidi uwe mwelewa wa umuhimu wa kipengele cha dini katika sensa.
 
Kama hoja ni kujua tu idadi ya watu na dini zao, sio mabya kitakwimu. Lakini sio busara kutumia point hii kuzuia sensa. Nimesema BAKWATA wana kazi rahisi tu kujua idadi ya waumini wao, kupitia taasisi zao zilizopo maeneo mbali mbali hapa nchini. Sio lazima kutegemea sensa ya jumla kama hii.
 
Hivi huyu Rais wetu wa sasa aliyebakiza miaka yake miwili Na nusu aondoke Na Chama lake ana MSHAURI kweli BABU HUYU..!! Akifanya mchezo muda wake uliobaki utamletea huzuni ya milele..

Nilisikia kwamba washauri wake wote walimkimbia Kwa sababu alikuwa anawatosa..Kabaki Wassira.. Sasa huyu aliyewahi kukiasi Chama toka lini akawa mshauri mzuri.. Ushauri wake utakuwa umautimauti tu, kwanini serikali isikae Na viongozi hawa wa Dini Na kuwauliza Chanzo cha vurugu zao badala ya kuwaona wapuuzi wanaostahili kumwagiwa Maji ya uchungu Na virungu.. Hata Kama kweli ni wapuuzi Lakini bado ni raia halali Wa JMT.. Wanastahili kusikilizwa Na kuelekezwa wanachodhani ni Hoja Na mtagundua ni nani Yuko nyuma ya mapazia Haya ya chokochoko.

Sasa serikali iko kimya, inaachia raia wahukumiane.. Na hukumu ya raia ni ubaguzi Na Chuki vitazuka.. Kwanini serikali hii sio SIKIVUU..

Mrisho.. Muda wako uliobaki ni kidogo.. Usipobadili mwelekeo nakwambia Utaona 2 years Kama gunia la Miaka Elfu ..
 
hili ni suala la kuwa na uelewa tu. Malengo ya kuwa na sensa ni maandalizi ya kupanga mipango ya Taifa ya Maendeleo. Kigezo cha dini hakina msaada wowote katika mipango ya maendeleo yetu
 
Kama hoja ni kujua tu idadi ya watu na dini zao, sio mabya kitakwimu. Lakini sio busara kutumia point hii kuzuia sensa. Nimesema BAKWATA wana kazi rahisi tu kujua idadi ya waumini wao, kupitia taasisi zao zilizopo maeneo mbali mbali hapa nchini. Sio lazima kutegemea sensa ya jumla kama hii.

that's right! wapitie katika misikiti kuanzia mitaani then wajumlishe idadi mpaka kitaifa. wakumbuke kuangalia na kiwango cha elimu cha waumini wote na kujua sababu za kuwepo hapo. Then wachukue hatua za mabadiliko
 
Kwani kuna tatizo gani kuweka dini kwenye sensa, mbona nchi nyingi duniani wameweka sehemu ya dini, kama Uingereza, Misri, Israel, na hakuna tatizo lolote.

..na kuna tatizo gani isipowekwa?
 
Ebu tuongelee 'Kisayansi' hili swala.....kwenye 'Sensa', kama ilivyokuwa kwenye scientific survey nyingine...lazima uwe na 'definition' ya variables zako. Sasa kama dini inalazimishwa iwe mojawapo...lazima uidefine...na pia udefine 'criteria' za kumuita huyu ni 'muIslamu' na yule ni 'mKristo'.

Sasa swali....'muIslamu' ni nani na 'mKristo' ni nani? Kwa juu juu tu mtu unaweza kudhani ni rahisi kujibu..si huyu anaitwa Juma, Rashidi, Fatma, Shamsa..wazazi wake ni waIslamu bla bla blaa...au huyu anaitwa Joseph, Richard, Faith, Sasha...wazazi wake ni waKristo bla bla blaa.....Is that scientific enough kudefine variable ya uDini kwenye sensa? Je mtu kuwa dini fulani ni jina tuu lenye mahadhi ya hiyo dini au wazazi wake kuwa waumini wa hiyo dini?

Naamini kuna vigezo/misingi kadhaa vya kuweza kujua kama mtu ana imani thabiti ya kiIslamu au kiKristo..ambayo haiwezi kujibiwa na swali moja tu kwenye questionnaire ya sensa kama' Dini:...........' How sure you are kuwa atakachojaza mtu ndio imani yake...utakuta mlevi fuska anaitwa Jafari au Geophrey umuhesabu kama muIsalmu au mKristo, kisha utambe sisi tuko wengi zaidi tunadeserve mgawanyo mkubwa zaidi wa rasilimali!? Upuuzi mtupu..
 
Bakwata bwana hoja zao za kiaya-aya, Wakwaya nao watataka kujua wako wangapi, Wakala pia. Nendeni mkale tende huko. Agrr
 
hivi ... leo nikihesabiwa kama muislam halafu kesho nikabadilisha dini na kuwa mkristu .... hizi data zitakuwa zinapotosha mbali na kuwa useless
 
Sensa ya mwaka 1957 ya kikoloni kipengele cha kuonesha dini kilikuwepo na ndio kinachoonesha takwimu waislamu wangapi na wakristo wangapi, na ukiangalia mwaka huo 1957 waislamu walikuwa ni 65%.

Baada ya hapo sensa zote zilizofuata kipengele cha dini kilifutwa; ajabu leo hii watu wanasema wakristo wapo wengi kuliko waislamu kwa takwimu zipi ikiwa kipengele cha kuorodhesha watu dini zao hakipo.

Pili ni kwanini wanaogopa kuhesabu watu kwa kutumia kigezo cha dini? Wengi watasema wanaogopa udini, hii hoja ni dhaifu maana nchi nyingi duniani sensa zinahebabiwa kwa mtindo wakujua idadi ya watu na dini zao ni asilimia ngapi katika nchi hizo.
The 1967 census the total figures for Tanzania Mainland were 32% Christian, 30% Muslim and 37% local belief. This shows Pagans as a leading majority. The 1967 census has not been able to show the reasons for the sudden decrease of Muslim population nor the growth of Paganism. This was the last population census showing religious distribution.
ISLAM AND POLITICS IN TANZANIA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom