BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

wengi mnapindisha pindisha! Lakini lengo kuu la kujua idadi yao ni kutaka kuibadili nchi iwe ya kiislamu, wakishajua idadi yao wataanzisha lingine la kutaka ipigwe kura ya kutaka nchi iwe ya kiislamu au la na hapo ndiyo katiba mpya inafuata. Mark my words!!
ni mara yangu ya kwanza kuchangia ktk thread inayohusu dini!comment yako ndio hasa nimeipenda!kwa nini wenzetu kila kitu wanalalamika!!?ni kama tu kuna ajenda nyuma ya pazia!ni dhahiri zanzibar wangependa nchi iendeshwe kidini na inaonekana wanaona waislam wa bara ndio wenzao!sasa kutaka idadi ya waislam na kuvalia njuga lengo ni nini hasa!!?mi nafikili wakati umefika na wakristu tuanze kulalama!
 
Pinda ‘awapigia magoti’ viongozi wa dini

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amewaomba viongozi wa dini na viongozi wa vyama vyote vya siasa wakiwamo madiwani, kuhamasisha na kuelimisha wananchi kushiriki katika zoezi la Sensa kitaifa ambalo litafanyika kuanzia Agosti 26 mwaka huu nchini kote.


Pinda alitoa wito huo jana, wakati akifungua mafunzo ya wakufunzi 150 wa sensa ya watu na makazi ngazi ya Taifa , katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo vijijini mjini hapa.


Waziri Mkuu alisema viongozi hao wakiwamo masheha, watendaji wa kata, wenyeviti wa mitaa na vijiji, wanapaswa kuwaeleza wananchi umuhimu wa kushirikiana na makarani, wasimamizi na watumishi wengine watakaofanyakazi ya sensa katika kipindi cha kuhesabu watu, ili kufanikisha zoezi hilo.


“Naomba pia kutumia fursa hii, kuwakumbusha wananchi wote, kuwa kazi ya kuhesabu watu itaanza Agosti 26 na kuendelea kwa siku saba, ninaomba wananchi mtunze kumbukumbu za taarifa za maswali yatakayoulizwa kwa watu wote watakaolala kwenye kaya zenu usiku wa kuamkia siku ya sensa Agosti 26, mwaka huu’’, alisema Pinda.


Alisema kazi ya sensa haikusudii kusimamisha shughuli za kiuchumi au kijamii kwani makarani wa sensa watapita kwenye kaya muda wowote katika kipindi cha simu saba.


“Jambo la msingi ni kuhakikisha kuwa kila mtu atakayelala nchini usiku wa kuamkia Agosti 26 lazima ahesabiwe mara moja”, alisema Pinda.


Hata hivyo, Waziri Mkuu, aliwatoa hofu watu kuhusiana na zoezi hilo kwa kuwaeleza kuwa taarifa zote zitakazotolewa na mtu, zitakuwa ni za siri.


Pinda alisema katika zoezi hilo la sensa mwaka huu, Serikali imeamua kwamba uingizaji wa takwimu za sensa kwenye kompyuta utafanyika kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya “Scanning” ijulikanayo kama Optical Mark Reader(OMR) technolojia ambayo ilitumika pia katika sensa ya mwaka 2002 na kuwa na ufanisi mkubwa.


Katika ufunguzi huo, Waziri mkuu pia aliwataka wakufunzi hao, kwenda kutoa elimu nzuri katika ngazi mbalimbali ili kufanikisha zoezi hilo la sensa mwaka huu.


Awali waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa, alisema Serikali imetenga fedha za kutosha kufanikisha zoezi hilo ambalo lengo lake kuu ni kujua idadi ya watu na kukusanya taarifa za kina za kidemografia, Kiuchumi, kijamii na maelezo ya makazi ili kupata takwimu muhimu za kupanga mipango endelevu ya maendeleo ya wananchi hasa katika utekelezaji mipango kadhaa ya maendeleo ya Taifa, ikiwapo ya malengo ya millenia.
Pinda
 
Hayo ya kutakiwa kujaza dini yako kwenye form za hospitali, polisi au mahakamani, kwangu mimi ni upuuzi. Na siku moja nilipokamatwa na traffic police kutokana na traffic offence, aliponiuliza dini na kabila langu, nilimjibu kuwa hakukuwa na umuhimu. Hakuandika chochote. Hayo ni kati ya mambo ya kijinga yaliyorithiwa tangu enzi za ukoloni ambayo hayastahili kuwepo. Suala la kuheshimiana na kuvumiliana kwa misingi ya kiimani ni muhimu sana na ni lazima kwa jamii yeyote iliyostaarabika, ndiyo maana kule Zanzibar tunaona kuna watu hayawani ambao hawawezi kuheshimu na kuvumilia uwepo wa makanisa au baa.

Kuhusu Uingereza au nchi nyingine zinazoingiza suala la dini katika sensa, mimi sioni kama ni jambo la ajabu, na hata hapa Tanzania kama wangeliingiza, pia nisingeona jambo la ajabu. Kioja na jambo la kushangaza ni pale ambapo Ponda na wenzake wanasema kuwa nia ya kutaka kuingiza kipengere ya kujua dini ya mtu ni kutaka kujua waislam wapo wangapi ili nafasi za uongozi, utawala na ajira zigawiwe kufuatana na dini. Na hapo ndipo upumbavu ulipo. Serikali imefanya vema kutokuitikia ombi la kipumbavu la akina Ponda kwa sababu ya nia ovu ya Ponda na wenzake. Kwa sababu tukikubali kufanya sensa ya dini kwaajili ya mgawanyo wa uongozi au ajira, baadaye tutataka ifanyike ya makabili ili madaraka na nafasi za uongozi zigawanywe kwa uwiano wa uwingi wa watu katika kabila au eneo fulani. Sensa ifanyike kwaajili ya kupanga maendeleo ya watu wote maana mahitaji ya msingi kama barabara, maji, chakula, elimu, makazi, n.k. haviathiriwi na dini au imani ya mtu, ni mahitaji universal. Serikali imepanga kufanya sensa kwa mahitaji yake, na kama katika hiyo nia yake, hawaoni umuhimu wa dini au kabila la mtu, kwa nini jumuiya au kundi fulani liilazimishe? Waislam kama wana mipango ya maendeleo ambayo inategemea idadi ya waumini wake, hawakatazwi, wanaweza kujihesabu kwa kutumia mifumo yao ya ndani, na hilo siyo jambo gumu.
 
Utaeleweka tu kama hiyo sensa itakayofanywa na Waislamu itatambulika rasmi Kitaifa (serikali).


Kwa maoni yangu, kama sensa hiyo itafanyika kwa uhakika, itakubalika. Na hamna sheria itakaozuia taasisi za kiislamu kuitangaza hiyo report yao katika vyombo vya habari vya ndani na nje na katika mitandao. Najua inaweza isikubaliwe na watu wote na inaweza kuhojiwa katika baadhi ya maeneo. Hata hiyo taarifa ya sensa ya Serikali pia haiwezi kuwa sahihi asilimia mia moja. Kuna maaeneo inayoweza kuhojiwa.

Kwa mtizamo wangu kugomea sensa sio suluhisho. Kama tunataka kipengele cha dini kiwemo katika kila sensa tuliingize hili katika maoni yetu ya mchakato wa katiba mpya unaoendelea
 
Tatizo lenu jingine! mmejisahau kabisa kuwa Waislamu nao ni Watanzania! hili ndio tatizo kubwa,ss wote ni watanzania kwanini tuanze kuulizana dini! dini ni imani binafsi tuache institution zinazohusu dini zifanye mambo ya dini na serikali ifanye mambo kwa maslahi ya watanzania wote.
Hakuna mzizi wa fitina,hakuna uadui ni kuelewana tu ili kujenga nchi yenye amani na maendeleo.
 
Sasa nikmwambie kitu katika dodoso la sensa limetaja idadi ya nyumba za ibada (makanisa na misikiti). wanataka kujua idadi ya nyumba hizo lakini wanakataa kujua idadi ya waumini wa nyumba hizo za ibada!!!. Inachekesha sana. Hii ni sawa na kusema nyama ya nguruwe haramu lakini mchuzi wake halali. Nashangaa kitu kingine, inakuwaje kama nyinyi mnajitangazia wengi (kwenye mitandao yenu, kalenda na hata TBC) lakini mnaogopa kuhesabiwa rasmini na serikali?!!!. Hta mtoto wa darasa la kwanza atagundua kuna kitu mnaficha. Tunasema hatushiriki sensa mpaka tunayoyataka yafanyiwe kazi. Huu ndio msimamo wa waislamu wote ukienda kinyume na haya uislamu wako utakuwa na mashaka, ujichunguze.
 
Nimesoma post nyingi humu nimegundua kuwa; mosi, wanao pinga kuweka kipengere cha DINI hoja yao ni kuwa hakina umuhimu kwa serikali maana serikali haina dini, pili, na kwakutokana na hoja ya kwanza, inaonekana wanaotaka kipengere hiki hawaelewi au wanashupalia kitu kisicho muhimu. SASA Kama kipengere cha dini hakina maana na hakina faida wala hakina hasara basi kiwekwe ilimradi kuondoa manunguniko maaan hatuna cha kupoteza kikiwepo.
 
Sasa nikmwambie kitu katika dodoso la sensa limetaja idadi ya nyumba za ibada (makanisa na misikiti). wanataka kujua idadi ya nyumba hizo lakini wanakataa kujua idadi ya waumini wa nyumba hizo za ibada!!!. Inachekesha sana. Hii ni sawa na kusema nyama ya nguruwe haramu lakini mchuzi wake halali. Nashangaa kitu kingine, inakuwaje kama nyinyi mnajitangazia wengi (kwenye mitandao yenu, kalenda na hata TBC) lakini mnaogopa kuhesabiwa rasmini na serikali?!!!. Hta mtoto wa darasa la kwanza atagundua kuna kitu mnaficha. Tunasema hatushiriki sensa mpaka tunayoyataka yafanyiwe kazi. Huu ndio msimamo wa waislamu wote ukienda kinyume na haya uislamu wako utakuwa na mashaka, ujichunguze.

Acha kupotosha watu, mimi ninayo nakala ya dodoso la sensa, ambalo mdogo wangu ni mwalimu walifanyia mazoezi. Hilo swali la nyumba za ibada Makanisa na misikiti halimo.

Ukweli ni kwamba kwa hatua ambayo NBS wamefikia hawawezi kuongeza wala kupunguza kipengele hata kimoja kwenye dodoso la sensa, hivyo swali la dini lisiwemo au liwemo kwasasa is irrelevant, subirini sensa nyingine ya mwaka 2022! Najua Ukweli ni mbaya na unauma. Dodoso limeshakuwa CODED, TRAINED, PILOTED and PROGRAMMED to the computer. Kwa mda uliobaki HAIWEZEKANI DODOSO kufanyiwa marekebisho yoyote.
 
Nimesoma post nyingi humu nimegundua kuwa; mosi, wanao pinga kuweka kipengere cha DINI hoja yao ni kuwa hakina umuhimu kwa serikali maana serikali haina dini, pili, na kwakutokana na hoja ya kwanza, inaonekana wanaotaka kipengere hiki hawaelewi au wanashupalia kitu kisicho muhimu. SASA Kama kipengere cha dini hakina maana na hakina faida wala hakina hasara basi kiwekwe ilimradi kuondoa manunguniko maaan hatuna cha kupoteza kikiwepo.

Hakina faida lakini hasara ipo. Wehu akina Ponda wanasema kuwa wakijua idadi ya waislam wanataka watumie idadi hiyo kuomba uwiano wa uongozi na ajira kwa misingi ya dini. Hao wendawazimu nia yao ni kutafuta mahali pa kuanzishia chokochoko za kidini.Kama nia ni kutaka kujua tu kuwa nani wengi kati ya wakristo, waislam na wapagani Tanzania, serikali itangaze kuwa waislam ni wengi na baada ya hapo tutaona faida itakayopatikana kwa hao walio wengi.
 
Leo asubuhi sheikh ponda amepinga kauli ya mufti aliyoitoa jana akiagiza waislamu kushiriki ktk sensa ya mwezi agosti mwaka huu. akihojiwa na redio imaan iliyopo morogoro, sheikh ponda amesema kuwa bakwata ni moja ya taasisi za kiislamu hivyo mufti hawezi kuamua peke yake bila kuwashirikisha wajumbe kutoka taasisi nyingine.


"tulikutana dodoma na waziri wassira tukiwa wajumbe wa taasisi zaidi ya 10 za kiislamu, bakwata ikiwa moja wapo. msimao wetu ulikua mmoja kuwa hatutoshiriki sensa hadi yafanywe mambo mawili. la kwanza kipengele cha dini kiwekwe kwenye dodoso. la pili tume ya taifa ya sensa iwe na mchanganyiko wa wajumbe waislamu na wakristo. waislamu kwenye tume ni 20%." alisema ponda.


alipoulizwa nini kitaendelea akasema kuwa taasisi zote zinakutana leo na leo ama kesho watafanya press conference ili kuwaeleza watanzania maazimio yao. "Mufti amejidhalilisha. nina imani waislamu watafuata maelekezo yetu. mufti ataonekana jinsi asivyo fuatwa na kusikilizwa na waislamu wengi."


source: redio imaan
 
Sasa huyu ni gaidi anatakiwa akamatwe.

Serikali naomba imuangalie huyu mtu ni tishio kwa usalama wa nchi.
 
Yeye kama hataki kuhesabiwa basi asifungue mlango siku ya sensa. Hawa ndio wale mashehe njaa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom