BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

Ngoja ni kuelezee ni kwa nini George Bush jnr alikuwa akijulikana kama Mufti Bush katika nchi za Kiarabu:
Viongozi wa nchi za Kiarabu huwa wanatafuta Wahuni na kuwahifadhisha baadhi ya masuala ya dini, kinachofuatia ni kuvalishwa vilemba, majoho kufundishwa pozi za Scholars, namna gani wanavyotembea, wanavyozungumza n.k
Baada ya Muda utasikia Rais au Mfalme amemteua mmoja wa hawa wahuni kuwa Sheikh wa jimbo au mkoa fulani, kinachofuatia ni kumuona kila siku katika TV,Magazeti, internet n.k wanamkuza, na wananchi wanaambiwa kuwa ukitaka fatwa nenda kamuone Sheikh fulani (huyu Mhuni) na wanamuweka katika payroll yao.
Wakati sasa Bush akitaka fatwa ya mfano Waislamu wasiende Iraq kuwasaidia Waislamu wenzao dhidi ya America, huwapigia simu hawa viongozi na hawa viongozi huwaambia hawa Mashehe wao (wahuni) toeni fatwa kuwa ni haramu kwa kijana wa Kiislamu kwenda Iraq, huyu mhuni atakuja kwenye TV na kutoa fatwa kuwa haifai kwenda Iraq!na atasikilizwa kutokana na jinsi Serikali ilivyom promote.
Hivyo chochote anachokitaka Bush hupewa "fatwa" anayoitaka.
Kwa namna hii George Bush alikuwa akijulikana kama "Mufti Bush" katika nchi za Kiarabu, simu moj tu kutoka Washington kesho una "Sheikh" kwenye TV na fatwa" ya kile anachokitaka Bush
 
Sipati picha kama mkuu wa nchi angekuwa mkristo Mungu si abdala mkuu wa nchi yupo upande wenu sijui mtasemaje
 
Uwe unasoma posts kabla ya kuchangia, hili lilishajibiwa hapa na M-joka:

"Mimi nilisema Wakristo wanaruhusiwa kuendesha na kuweka takwimu za idadi ya waumini wao, hata waislamu vile vile wanaruhusiwa, ikiwemo kanisalakini nani wa kumuamini?,

Nani asiyejipendelea? Ndio maana inakuja kwamba ni serikali, utawala ndio uwe na mamlaka katika jambo hili KITAIFA, KITAIFA ndugu yangu, na sio taasisi za kibinafsi
...SASA KWANINI (SERIKALI) WAKWEPE WAJIBU WAO NA KUKIKWEPA KIPENGELE HICHO CHA DINI???? Sijui Mkuu unafahamu sijui.

kumbe tatizo lenu ni kuwa wakristo kuptia takwimu zao wanajipendelea kuwa wao ni wengi its simple lets we muslims also regards ourselves that we are MANY
 
Kwenye post kuna hii aya
“Kama tatizo ni kuvurugika kwa amani, umoja na utulivu, mbona basi vyombo hivi visivyohusika na takwimu vinatoa takwimu hizi tena hadi kwenye mitandao na Serikali kuvifumbia macho, huku kukiwa hakuna umoja wala amani iliyovunjika? Kwa nini isifanyike sensa ya kidini na kupatikana takwimu halisi?”
1.
Sasa kwa nini msitumie takwimu hizo kujua idadi ya waislamu na wakristu?
2. Hakuna nchi inayojiita ya kidemokrasia na kuanza kuchambua idadi ya waamini wa dini fulani ni wangapi.Namaanisha KWENYE DEMOKRASIA HAMNA DINI.
3. Mkijua kuna Wakristu 70% mtafanya nini?
 
Acha tujue tuko wangapi waislam tulete mabadiliko ktk nchi hii naona inataka kutushinda,tutaanzisha jehad kwa wote mafisadi na makafiri
 
Pamoja na kwamba mimi ni Muislamu,elimu dunia imenisaidia kujua uhalisia wa mambo..Nawashauri viongozi wangu waandaa Sensa ya taifa kama nia yao ni kujua idadi yetu..Waandae dodoso linalolenga kujua taarifa zetu kidini..Tutachangia gharama ktk hilo,LAKINI SENSA YA TAIFA LAZIMA NISHIRIKI..,NINALIPENDA TAIFA NA NATAKA LIENDE MBELE...ALLAH HAJATUAMURU TUPINGE MAENDELEO JAMANI..

We si minkum!
 
Hivi hawa BAKWATA tukiwaita Dhaifu tutakuwa tumekosea?:eyebrows::eyebrows::lol::spy:
 
Kama shida ni kujua idadi ya waislam kwa nini waislam wasifanye sensa yao kujua idadi ya waumini wa dini yao? Kwani ni lazima wategemee sensa ya taifa?

Katika hali ya kawaida kuna misikiti mingi tu kwenye maeneo ya kuishi. Wanaweza kutumia viongozi wa hiyo misikiti kuhesabu idadi ya waumini wao ikiwa ni pamoja na wale wasioenda kuswali mara kwa mara lakini wanaishi katika maeneo ilipo misikiti hiyo. Kila msikiti ukijua idadi ya waumini katika eneo ulipo mwishoe si watajua idadi kiwilaya, mkoa na kitaifa?
 
Mkuu Joka kunavitu viwili ambavyo inabidi tuvitofautishe, kuna wananchi kuwa na dini na kuna dini zao kutambulika na seriakali, sasa ni nani kasema hata wananchi vile vile hawana dini? Mimi kwa mtazamo wangu serikali kama serikali haitaji kutambua dini yako wewe kama wewe, ila dini zote zinatambulika kisheria kama jumuiya, kama zilivyo jumuiya nyingine au taasisi zozote.

Alafu labda nikucaution tu, dont be too delutional. Mi sijapoint fingers kwamba waislamu Tanzania wanafujo, I said swala la udini linaweza kuleta machafuko kama ambavyo imetokea sehemu nyingi duniani. Hilo halina ubishi, mifano tunayo. Alafu isitoshe watu wengi hawana elimu ya kutosha Tanzania kuelewa vitu kama hivi, kwa hiyo ni rahisi kupotoshwa. Hivi haoni kwamba this a 'vulnerable issue'?


Hivi unavyosema 'haki' ukimaanisha kwamba ni jukumu au wajibu wa serikali hauoni kwamba unapingana na mtazamo kwamba serikali haina dini? Kitu ambacho wewe mwenyewe umekubaliana nacho. Huku siyo kuwa delutional kweli?Unaweza kutofautisha mtazamo wako na hiki kipengele cha kutokuwa na dini?

Kwenye point ya tatu, unahofu na ufisadi, maadili kuporomoka au unahofu na ukristo au unahofu na mabepari? Yani sielewi yani? Kwa sababu hivi vitu havina uhusiano. Alafu sioni sababu ya kuhusisha ukristo na mabepari, ndo maana mi nasema you are kind of delutional, hauja fahamu vizuri what do you want, au labda unadhani sensa ya kidini itawaondoa mabepari wa uarabuni au magharibi!!? au anadhani kuporomoka kwa maadili kwenye uislamu kunatokana na idadi ya watu watu wadini za tofauti?

Swala hapa ndugu yangu ni jinsi gani serikali yetu itaendeshwa bila kuhusisha au kujihisisha na dini ya aina yoyote, hasa hizi zilizopitwa na wakati kutoka middle east.


Juzi juzi tu Waziri wetu wa mambo ya nje alinukuliwa akisema kwamba "mila na desturi zetu, sheria zetu and dini zetu" hazitaruhusu kubadilisha sheria ya ndoa ili kuruhusu sheria ya ndoa kwa mashoga kama zinavyoshinikiza nchi za Magharibi kama masharti ya misaada na kulificha shinikizo lao ndani ya mbiu ya "haki za binadamu"

Kwahiyo hapa utaona vitu vitatu:- mila na desturi (culture and traditions), sheria (laws) na dini (religions) zetu ni mihimili ya kiji-jeuri cha kutufanya kujipapatua na utovu wa adabu wa Cameron aliouonesha kule Perth, Australia. Sasa nakuuliza!
1. Hii Millenium Development Goals ambao ndio wadhamini wa hii sensa tunayoizungumzia kaipanga nani?
2. Nini wanakusudia hawa wapangaji wa hiyo "Millenium Development Goals" kukiondosha hicho kipengele cha dini katika sensa wanazozidhamini na kuzilazimisha kwetu?
3. Kwa viongozi wetu wa serikali kukubali bila ya kuhoji kukiondosha kipengele cha "dini" ambacho ni moja kati ya mihimili mitatu inayotufanya angalau tungangarike (kimaskini-jeuri), huoni ya kuwa wanatuuza kwa bei ya dezo? Huoni huo ni uzembe? au unafikiri kwamba wana umbumbumbu kiasi hicho? Hapana mimi nafikiri "they just don't care" alimradi tu wanaendelea kuifisidi nchi.
4. Nini unafikiri utakuwa muhimili wa pili kuondoshwa baada ya huu wa dini? Ni sheria zetu (Laws)na kwahiyo ukizingatia kwamba hawa viongozi wetu ndio wanaotunga sheria kule bungeni, na wao ndio wanaoruhusu vitu kama hivi kwa kuwa tu vinaingizwa kiujanjaujanja. Huoni kwamba wanashirikiana na hao mabaradhuli wa Magharibi kwa kuwapa ujumbe kwamba eti "wasije moja kwa moja kama alivyokuja Cameron kule Perth, bali waje kiujanjaujanja wasije wakawaamsha hawa wapumbavu(Watanzania /Waafrika) na kukitia kitumbua mchanga?
6. Je utakuja kushangaa sensa itakayofuata au legal paperworks nyengine hapa Tanzania zikawa na vipengele vya ajabu ajabu vya kuhusu "gender" na "marital status" au unafikiria wana-concentrate na kuondoshwa tu na sio kuingiza vipengele vipya vyo ajabu ajabu?
5. Nini unafikiri kinachowafanya viongozi wa makanisa kukaa kimya (silence of consent/approval)? Je unafikiri ndio vifuu kiasi cha kutoyajua haya?
6. Nini makosa ya waislamu katika kuyaona haya na kusimama kidete?
 
Waislamu kila kitu nyie mnaonewa!! Mbona ni nyie kila siku? Leo maraisi na Makamu wa bara na visiwani wote ni waislamu lakini bado mnalalamika.Hivi wangekuwa wakristo ingekuwaje?
 
ndugu wadau nafikiri ni wakati muhimu wakujua mantiki ya maombi haya kabla ya kukurupuka. Mimi nafikiri ni muhimu kuwa na kipengele hicho kwanini. Sensa ni kwa ajili ya kupanga maendeleo ya nchi kweli, tukumbuke kwamba maendeleo yanahusisha mambo mbali mbali mfano maendeleo ya mifugo ambayo ni pamoja na nguruwe, je serikali itafanyaje kwenye sehemu kama hizo. Lazima serikali ijue tabia za watu wa eneo fulani ili ijue ni mipango gani inayofaa.
Ukisoma dodoso ya sensa inasema vile vile ni jinsi gani serikali itashawishi mashirika ya kidini kuongeza maendeleo. Nafikiri itakuwa ni rahisi kwa shirika la kidini kujuaidadi ya waumini wake kwenye eneo husika ili kujua jinsi ya kusaidia.
Serikali imekuwa ikiwaomba kila siku viongozi wa dini kusaidia kwenye kupambana na majanga mbalimbali kwa mfano vvu na ukimwi. Kwa kujua idadi ya waumini kwenye eneo husika itakuwa ni rahisi kupanga mipango ya kupambana na majanga hayo kwa kutumia nguvu husika.
Jamani tujiepushe na kujibu hoja kwa udini.
Cha kujiuliza leo hii serikali inasema hakuna haja ya kipengele cha dini, lakini cha kushangaza kwa nini waliwaita viongozi wa dini kujiandaa na sensa, ukweli wanajua umuhimu ila wanapelekeshwa na hisia za kikundi fulani. Kama kweli wanajua hili kwa nini serikali ilikaa kimya pale chombo chake cha habari kilpotoa takwimu potofu za idadi ya watu kwa dini zao, mpaka waislamu walipolalamika ndipo wakaomba msamaha. Vile vile sijamuona kati yenu mnaochangia hapa kukemea hili ila kwa sababu ilikuwa inafavour kikundi fulani ilionekana ni sahihi.
Leo hii mnaongelea udini lakini sijaona mkilalamika kwa nini viongozi wakiapishwa wanatumia vitabu vya kidini badala ya katiba, je sio kujua kati ya hawa wanaoapa wetu ni wangapi na wao ni wangapi, sababu serikali haina dini.
Kwa nini tusijiulize kwa nini unapotaka huduma mbali mbali za serikali kuna kipengele unachotakiwa kutaja wewe ni dini gani, kwa nini msipige kelele hili nalo liondolewe?
Tukichangia kwa hoja itakuwa ni vizuri badala ya kusukumwa na interest ya vikundi vyetu.
 
Uwe unasoma posts kabla ya kuchangia, hili lilishajibiwa hapa na M-joka:

"Mimi nilisema Wakristo wanaruhusiwa kuendesha na kuweka takwimu za idadi ya waumini wao, hata waislamu vile vile wanaruhusiwa, ikiwemo kanisalakini nani wa kumuamini?,

Nani asiyejipendelea? Ndio maana inakuja kwamba ni serikali, utawala ndio uwe na mamlaka katika jambo hili KITAIFA, KITAIFA ndugu yangu, na sio taasisi za kibinafsi
...SASA KWANINI (SERIKALI) WAKWEPE WAJIBU WAO NA KUKIKWEPA KIPENGELE HICHO CHA DINI???? Sijui Mkuu unafahamu sijui.

Ujipendelee kwa kusema mpo wengi ili ikusaidie nini? Kwani leo hii ikitangazwa waislam wapo 99% katika Tanzania, wewe itakusaidia nini, maisha yako yatabadilika au utabaki kama ulivyo? Kwangu mimi whether christians or moslems are the majority, it is imaterial because it adds or reduces nothing.

I am coming from minority tribe, but I am happier than the majority tribe members who have no hope of getting three meals. Tanzania yenye watu 45 milioni inaizidi nini Israel, Norway, Dernmark, Netherlands au Sweden ambazo zina wananchi wachache sana lakini Rais wetu JK kila siku yupo nchini mwao kubembeleza kupewa misaada ya kuwajengea visima vya maji Wakwere? Kweli hakuna ugonjwa mbaya Duniani hapa kama wa kukosa akili. Tunaacha mambo ya maana ya kuendeleza jamii yetu ya Watanzania tunahangaika na kutaka kujua nani ni wengi, wakristo au waislam. Halafu baada ya hapo kinafuata nini? Kwa kulijua hilo tutakuwa tumepata maendeleo gani? Mimi napendekeza kwenye sensa yaongezwe maswali mawili: 1) Unataka wafanywe nini viongozi mafisadi na wala rushwa 2) Wananchi wanaoshinda wamekaa bila kufanya kazi wafanywe nini. Kitakachokuwa kimetajwa na wananchi wengi kipelekwe bungeni kupitishwa kuwa sheria.
 
ndugu wadau nafikiri ni wakati muhimu wakujua mantiki ya maombi haya kabla ya kukurupuka. Mimi nafikiri ni muhimu kuwa na kipengele hicho kwanini. Sensa ni kwa ajili ya kupanga maendeleo ya nchi kweli, tukumbuke kwamba maendeleo yanahusisha mambo mbali mbali mfano maendeleo ya mifugo ambayo ni pamoja na nguruwe, je serikali itafanyaje kwenye sehemu kama hizo. Lazima serikali ijue tabia za watu wa eneo fulani ili ijue ni mipango gani inayofaa.
Ukisoma dodoso ya sensa inasema vile vile ni jinsi gani serikali itashawishi mashirika ya kidini kuongeza maendeleo. Nafikiri itakuwa ni rahisi kwa shirika la kidini kujuaidadi ya waumini wake kwenye eneo husika ili kujua jinsi ya kusaidia.
Serikali imekuwa ikiwaomba kila siku viongozi wa dini kusaidia kwenye kupambana na majanga mbalimbali kwa mfano vvu na ukimwi. Kwa kujua idadi ya waumini kwenye eneo husika itakuwa ni rahisi kupanga mipango ya kupambana na majanga hayo kwa kutumia nguvu husika.
Jamani tujiepushe na kujibu hoja kwa udini.
Cha kujiuliza leo hii serikali inasema hakuna haja ya kipengele cha dini, lakini cha kushangaza kwa nini waliwaita viongozi wa dini kujiandaa na sensa, ukweli wanajua umuhimu ila wanapelekeshwa na hisia za kikundi fulani. Kama kweli wanajua hili kwa nini serikali ilikaa kimya pale chombo chake cha habari kilpotoa takwimu potofu za idadi ya watu kwa dini zao, mpaka waislamu walipolalamika ndipo wakaomba msamaha. Vile vile sijamuona kati yenu mnaochangia hapa kukemea hili ila kwa sababu ilikuwa inafavour kikundi fulani ilionekana ni sahihi.
Leo hii mnaongelea udini lakini sijaona mkilalamika kwa nini viongozi wakiapishwa wanatumia vitabu vya kidini badala ya katiba, je sio kujua kati ya hawa wanaoapa wetu ni wangapi na wao ni wangapi, sababu serikali haina dini.
Kwa nini tusijiulize kwa nini unapotaka huduma mbali mbali za serikali kuna kipengele unachotakiwa kutaja wewe ni dini gani, kwa nini msipige kelele hili nalo liondolewe?
Tukichangia kwa hoja itakuwa ni vizuri badala ya kusukumwa na interest ya vikundi vyetu.

Hoja ulizozitoa ni nyepesi. Kamati ya Ponda walisema wanataka kujua idadi ya waislam ili utawala wa nchi ugawanywe kwa misingi ya kidini. Hapo aliharibu kila kitu, kwani kwa kutamka hivyo alikiuka katiba inayosema wazi kuwa Taifa hili haliendeshwi kwa misingi ya kidini bali kwa matakwa ya katiba, uwezo wa mtu na matakwa ya wapiga kura.

Kujua idadi ya waislam haiwezi kuelezea wapi wafugwe nguruwe na wapi wasifugwe. Kuna waislam na wasabato wengi ambao licha ya kuwa dini zao zinawazuia kufuga na kula nyama ya nguruwe lakini wanafuga na kula pia. Mheshimiwa Yusufu Makamba akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam aliwahi kuwashauri watu kuwa kama wanataka kuondokana na umaskini wafuge nguruwe kwani ni mradi wenye faida kubwa kutokana na uzoefu wake wa kuwa M/Kiti wa kamati ya kuuondoa umaskini.Kama hujui, nchi ya Indonesia ndiyo nchi yenye waislam wengi Duniani kuliko nchi yeyote lakini ni kati ya mataifa yanayoongoza kwa ufugaji na ulaji wa nguruwe (There are about 7.4 million pigs in Indonesia, with about 1.6 million in East Nusa Tenggara, according to the Agriculture Ministry.

There are 900,000 pigs in Bali, 876,000 pigs in West Kalimantan, 760,000 pigs in North Sumatra, 570,000 pigs in Papua and 530,000 pigs in South Sulawesi.

Most of the remaining pigs are in Java).

Maeneo ambayo mpaka leo unaulizwa dini na kabila lako ni polisi, hospitali na mahakamani. Na huko kuna sababu za kuulizwa dini yako. Hospitali na polisi, watu huulizwa dini zao kama tahadhari endapo kama itatokea kifo, basi uhudumiwe kadiri ya imani yako. Mahakamani nako wanahitaji dini yako kwa sababu ya kiapo. Nje ya mambo hayo, taarifa za dini yako hazina msaada wala matumizi mengine yeyote. Na taratibu hizo ziliwekwa na serikali za kikoloni zikarithiwa na serikali huru. Ikumbukwe hapo zamani baadhi ya watu walikuwa hawajui hata kiswahili, hivyo kuna wakati ililazimu kuwapata watu wa kabila lako ili wasaidie katika tafsiri.
 
Ndugu yangu sintachoka kukuelimisha, ingawa najua ni vigumu kukiri ukweli hata kama unauona.
Ulichotakiwa kujibu ni hoja zangu ulizoziita dhaifu badala ya kuquote hoja za watu wengine, hapo ndipo pananifanya nikuone huna hoja za kujibu.
Kuhusu hoja yako ya ufugaji wa nguruwe, ninachokiongea hapa ni kwamba watanzania tunaishi kwa kuvumiluana lakini kuanzisha mradi wa nguruwe kwenye idadi kubwa ya waislamu ni kutafuta migongano kati ya wananchi hapo huleti maendeleo bali ugomvi.
Unapoongelea Indonesia ina idadi kubwa ya nguruwe, kwanza kabisa sina uhakika namaelezo yako lakini sikubishii kwa sababu sina details, lakini hata hivyo lazima wajue maeneo ya kuendesha biashara hiyo ili kusiwe na malalamiko ya wananchi wao. Lakini kama unaweza kutufananisha na Indonesia kwa nini tusijilinganishe na nchi kama Uganda au Uingereza ambao wame kiinclude kipengele cha dini?
Kuhusu kipengele cha dini kwenye huduma za kijamii, kuna haja gani ya kumuuliza mtu wakati kama ni hospitali kaletwa na ndugu zake na wanajua dini yake, polisi huyu aliyekamatwa ana ndugu zake lakini mimi ninayetoa ushahidi dini ya nini?
Serikali haina dini kupa mtu aape kwa katiba inayoendesha nchi na si vitabu vya dini, serikali haina dini. Ninapotaka paspoti dini ya nini?
Na kama ulivyosema haya tumerithi kutoka kwa wakoloni na tunayaendeleza kwa sababu ni mazuri ndio maana haujawahi kuyalalamikia kwani tusirithi nahili la kipengele cha dini ambayo yaliletwa na wakoloni na wao wanaendelea kuyapractise.
Tafadhali endelea kuleta hoja ili niendelee kukuelimisha
 
ingizaji wa dini za waTanzania unaweza kuwa heri na hofu kama kilivyo kisu. Mfano wa nchi za magharibiwanaprofile watu kutokana na iman na rangi pia ili kulinda maslahi ya wenyeji. Je tuishie kuuliza kama mwislamu au mkristo tu au twende mbele kujua kama mkristo, je mkatoliki, luteri pentekoste etc ? Au kama mwislamu, je u mshia, ahmaddiya suni, aga khan etc? Kwangu mimi profiling ya namna hii itasaidia sana kujua wapi kwenye matatizo na jinsi ya kusaidia. Lakini kuuliza tu Mislamu/Mkristo/Mpagani haina faida kwa miango nchi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom