BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

Mi naona waandae sensa ya kwao wenyewe.

Mbona kuna njia nyingi wanaweza kuzitumia kujua wahumini wao,siyo kulazimisha serikali.
 
Hebu wawekewe hicho kipengele tuone faida yake.
Labda kuna maandalizi ya jambo flani so wanahitaji kujua idadi yao wajiandae vema.
Wawekeeni yaishe.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Mkuu kama hukusikiliza BBC asubuhi ya leo basi shehe Kundecha alitegua mtego kwa kudai kuwa wananyimwa haki ya mahakama ya kadhi kuingizwa kwenye katiba kwa kudhaniwa kuwa ni wachache!
 
Samahani mkuu, please justify your assertions in red fonts, ni nini msingi na kwa jinsi gani udini utakavyochangia maendeleo ya taifa letu.

Hebu soma tena labda utapata kilichokusudiwa
 
Nitajie mikoa mingapi unaamini mko wengi kuliko wakristo? Jibu lako litanisaidia kufahamu uelewa wako kuhusu nchi yetu.
Siasa at work, ukweli waislamu wapo wengi. ingekuwa wakisto wapo wengi sensa ingefanyika haraka sana tena bila hoja hizo kuzungumzwa.
 
Aslimia 91 ya watumishi wa uma ni wakristu,kati ya hawa asilimia 90 ni mafisadi.mbona hiyo ya ufisadi na kutakaswa pesa makanisani sio siri? wengine ninao hapa ofisini ndio walionipa habari hizo
Nakuunga mkono alafu walivyo wajanja wanawasingizia waislamu wachache walioko kwenye ajira hii adimu kwao.
Mara utasikia Nazir Karamagi Rostam Azizi Bazir Pesambili Mramba nk.
Wanaenda mbali hata wanawataja walioko nje ya ajira. Utasikia mara Patel, Yusuph Manj nk.
 
We ndo mbumbumbu kabisa...yaani unaona hapo umejibu sayansi, labda sayansi ya maji marefu! Napenda ubishi wa kisayansi...ndio fani yangu! Twende kazi....

Ukimuuliza mtu 'wewe ni dini gani' akakujibu 'mimi ni muIslamu/mKristo/mPagani etc'...hakuna sayansi hapo! Kisayansi unatakiwa uprob kupata evidence kuthibitisha anachosema ambacho tayari kilishakuwa primarily defined (evidence ndio sayansi yenyewe). Lazima atoe vigezo vya yeye kujiita muIslamu au mKristo na uoanishe na defined criteria (kwa misingi ya dini yenyewe) za mtu kuwa muIslamu au mKristo. Then hapo ndio kiSayansi utasema huyu ni wa dini fulani na idadi yao ni wangapi.

Unachosema wewe hapo HUTAPATA IDADI YA WAISLAMU AU WAKRISTO....BALI NI IDADI YA WATU WALIOJIBU KUWA NI WAISLAMU AU WAKRISTO...hivyo ni vitu viwili tofauti, kuwa muIslamu au mKristo...na kujibu kuwa ni muIslamu au mKristo!

Ukiniuliza mimi dini yangu nitakujibu ni mKristo...lakini siendi kanisani, sishiriki jumuiya za kanisa, sisimamii amri kumi za mungu, sitoi sadaka, sitoi fungu la kumi, nakunywa pombe etc...ukinihesabu mimi kiSayansi sitakuwa kwenye fungu la waKristo kwamba nina vigezo vya kuitwa mKristo...bali nitakuwa katika fungu la waliojibu kuwa ni 'waKristo'!

Nonsense kabisa!!!!

Hivi nikuulize ushawahi kufanya research wewe? Au unafurahisha kijiwe? Hebu nikuulize swali evidence gani utaipata katika gender????? Katika forms za sensa kuna swali la jinsia JE NIKUULIZE WATAJUAJE KAMA WEWE NI MWANAMKE, MWANAUME, JIKE DUME AU HUNA GENDER YEYOTE?

Swali la Gender halina tofauti na swali dini kwani linataka kujua diversity ya demographic. Unasema sayansi inakuwa tayari ishakuwa primarily defined how? Mfano mtu alizaliwa mwanamke, ikisha akabadilisha jinsia akawa mwanaume how is that possible ati alishakuwa defined?

VILE VILE HAUTAPATA IDADI KAMILI YA JINSIA ZA WATU KWASABABU WATAKAOJAZA WENGINEO KWELI NI WANAWAKE, WANAUME, WANAOPENDA KUWA WANAWAKE, WANAOPENDA KUWA WANAUME HAYA TUCHAMBULIE WEWE UMEPATA TAARIFA GANI?
 
Jamani tuwe wakweli mimi nimeajiriwa na BOSI wangu ni mwislamu mzuri sana.
Katika Kampuni yake waajiriwa wa kudumu tulikuwa tisa, mmoja akaacha mwenyewe na mwingine akafukuzwa.
Tukabakia saba na wote saba ni ama wakristo au wapagani. Mwislamu alikuwa mmoja ndiye aliyeacha kazi. Sasa sikujua aliona labda bosi wetu naye anatumia mfumo Kristo.
Sababu za kuajiri hivi ni kutokana sifa za wafanyakazi anaohitaji na sana sana ni elimu zaidi!.

Hizo ni ngonjera mkuu,ajira za serikali haziko wazi kuna ufisadi mwingi,zingekuwa zinatolewa kwa ushindani wala usingesikia haya.Wewe si ndo unafanya kazi katika ile kampuni ya kitimoto? sasa unadhani waislamu watakuja huko saa ngapi bana!
 
Mkuu sredi kama hii ipo tayari kama unadhani unahitaji kufungua sredi nyingi basi hakikisha ina hoja nzito zilizo shiba kutofautisha na sredi iliyopo
Na si kuja na the same old story with defferent tittle.

Ni sensa ya wapi inahusisha miradi? Unajua maana ya sensa ya watu wewe?

Udini utaleta maendeleo gani kwa taifa?

Mod unganisheni hii thread haina lolote jipya

I thought you were a great thinker!
 
Thread imejaa wachangiaji na watazamaji bila shaka watazamaji wengi ni TISS.

There are currently 304 users browsing this thread. (96 members and 208 guests)
 
Always unaajiri mbumbumbu au mwelewa??? Always mbumbumbu haajiliwi...

Waache waelewa waajiriwe
 
duuuh mwaka huu lazma JK aombe likizo za kutosha daaah...huyu mzee wa watu hapumui?? likitoka hili linaibuka lile mbaya zaidi ni dini yake, so anakua kwenye tension ya hatari sana...pole JK pole sana duuh!!
 
kumchaya

Kwani Hospital ya Bugando, KCMC na zinginezo wanatibiwa Wakristo peke yao tu?? HAwa jamaa hata wawe na midigirii mingapi ni hakuna kabisa!
 
Last edited by a moderator:
#Dotto hao takataka, wanataka Ajira nusu kwa nusu wakati hakuna lolote
 
Mimi sipingi suala la dini kuigizwa kwenye sensa kwa sababu ya kuhatarisha amani, kwani kama nilivyosema kwenye post nyengine ya udini, hata tusipoweka idadi ya wenye dini hii au ile tunajuana. Ninachopinga ni kuwa "SENSA NI KWA AJILI YA KUJUA IDADI YA WATU NA KUSAIDIA KUANDAA MIRADI YA MAENDELEO NA KUTOA HUDUMA ZA KIJAMII" kama vile shule, afya, maji, umeme, barabara, mipango miji na sio kujenga misikiti, makanisa, mahekalu, masinagogi n.k.

Ama kweli "Ibilisi akikosa la kufanya hujipunga nzi kwa mkia wake". Kama BAKWATA, BAGOTI, BAKICHWA, BAMKWE au vyovyote watakavyojiita wanataka kujua idadi ya waumini wao kwa ksababu wanazozijua wao, wafanye sensa yao - kwishney - Tusijiumize vichwa kwa mambo ya kipuuzi kama haya.
 
SHULE chache, vyuo utata, hospital waulize wanazo ngapi??? Alf eti ooooh Mara uuuuh HAKUNA LOLOTE MAAMUMA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom