The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 617
- 1,800
Hata hivyo, muda si mrefu baada ya kauli ya Bashe, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) lilisema mchele, mafuta ya vilivyotolewa kama msaada na Marekani chini ya Mpango wa Pamoja Tuwalishe' ni salama kwa Walaji ambapo Taasisi ya Global Communities ikiwa ni sehemu ya Wadau waliohusika katika usambazaji
Swali ni: Je, Mchele huo utaendelea kusambwazwa kwenye shule au zoezi ndio limeishia hapo? Kwani inaonekana hakukuwa na muafaka wa nini kinachoendelea?
========== =============
JamiiForums imefanya jitihada za kupata ufafanuzi kutoka katika mamlaka kadhaa kuhusu hoja hii iliyoulizwa na member wa JamiiForums.com
Shirika la Viwango Tanzania (TBS)
Meneja Uhusiano na Masoko, Gladness Kaseka anasema “Hakuna maelezo mengine ya ziada, kila kitu kipo kwenye lile tamko letu la Machi 17, 2024”
Tamko lilieleza mchele, mafuta ya kupikia ya alizeti na maharage ambavyo vyote vimeongezwa Virutubishi vilivyotolewa na Wizara ya Kilimo ya Marekani kwa ushirikiano na Taasisi ya Jumuiya za Kimataifa (Global communities) kwa baadhi ya Shule za Dodoma, vyote ni salama kwa Walaji.
Alipoulizwa kwamba kwa tamko hilo inamaanisha wametoa ruhusa vyakula hivyo kuendelea kusambazwa shuleni na je, virutubisho vilivyoongezwa vilikuwa na nini vya ziada ambavyo hapa Nchini havipo? Amesema “Kila kitu kipo kwenye tamko letu la Machi 17 hakuna cha ziada”.
Wizara ya Elimu
Mkuu wa Mawasiliano Serikalini Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Sylvia Lupembe amesema “Shule zipo chini ya Ofisi ya Rais TAMISEMI, wao ndio waendeshaji Shule, sisi ni watunga sera, waulize wao.”
Wizara ya Kilimo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Geofrey Mweli anasema “Vyakula vipo chini ya Ofisi ya Rais TAMISEMI, wao ndio wanaweza kutoa ufafanuzi, Waziri wa Kilimo (Hussein Bashe) anashughulikia usalama wa chakula alitoa ufafanuzi wa mambo mawili.
“Kwanza nchi ipo salama kwa chakula na pili alieleza tumeshawasiliana na Wafadhili kwamba wanapotaka kuleta chakula kwenye shule, wanaweza kufanya uwekaji wa virutubisho hapa nchini.
“Kuhusu Mkataba wa chakula usambazaji wa hiki chakula upo chini ya TAMISEMI.
“Kulikuwa na hoja nyingi mtandaoni ikiwepo madai kuwa chakula hicho kitaondoa nguvu kwa Watoto lakini tayari TBS walitoa ufafanuzi na kuweka sawa.”
TAMISEMI
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini TAMISEMI, Nteghenjwa Hossesh alipoulizwa alisema “Hilo suala ungewauliza wao Wizara ya Kilimo, sina majibu ya moja kwa moja, ngoja nifuatilie.”
Global communities
Alipotafutwa Afisa mmoja wa juu (jina linahifadhiwa) wa Shirika hilo lililohusika kugawa chakula alisema “Mimi sio msemaji wa Shirika, wewe watafute US Embassy ndio watakupa taarifa kwa wao wao ndio walipost, wao ndio wanatakiwa kusema kama wanaendelea kugawa chakula au wamesitisha.
“Mtafute Godfrey Matumu huyu ndiye atakusaidia kukupa majibu, yeye ndiye mtu sahihi wa kukupa majibu hayo.”
Alipotafutwa Godfrey Matumu ambaye ni mmoja wa watendaji wa kuu wa Global Communities, alipoelezwa kuhusu hoja ya Mdau akasema "Nipo kikaoni, nitakutafuta baadaye."
Pia soma:
Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo: Waagizaji hawakupaswa kuleta mchele wa Msaada kutoka Marekani kwani Tanzania ina hazina ya mchele
TBS: Mchele, mafuta ya kupikia ya alizeti na maharage kutoka Marekani, ni Salama kwa Walaji