Waziri Bashe hakutakiwa kuukataa msaada wa mchele kutoka Marekani na kama alikuwa na mashaka yoyote angewatumia TBS

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,603
Mada hii ni kuelezea mashaka makubwa niliyonayo kwa Waziri wetu wa kilimo namna maamuzi yake yanavyoweza kuharibu mahusiano ya kimataifa kama asipojirekebisha.

Kwanza kabisa nianze Kwa 'declare interest' ,Sina mahusiano ya aina yoyote na NGO iliyoleta mchele wa msaada wenye virutubisho kutoka nchini Marekani chini ya kampeni ya wizara ya kilimo ya Marekani inayoitwa "Pamoja tuwalishe" na 'interest' pekee niliyonayo ni Kwa maslahi mapana ya nchi yangu .

Siku zote mjumbe hauawi na hiyo NGO inabaki kuwa ni mjumbe tu wa wizara ya kilimo ya Marekani ,kitendo Cha Waziri kuonesha kukasirishwa na kitendo Cha mjumbe kinaleta picha isiyopendeza.

Kwa mtazamo wangu badala ya Waziri Bashe kuonesha kukasirishwa na kuletwa Kwa mchele na hiyo NGO angetumia nafasi hiyo kufanya "formal communication" na wizara ya kilimo ya Marekani juu ya mambo tunayohitaji.

Kwa kuwa mchele huo ni msaada sikuona ulazima wowote wa Waziri kusema kwamba mchele tunao ,Kwa kuwa lengo la kampeni hiyo ni zuri ,tunatakiwa kuupokea msaada huo na kushukuru na wizara ingetumia TBS kuchunguza ubora wa mchele huo kimya kimya kabla haujaanza kutumika na kama kungekuwa na mashaka yoyote Serikali ingekataa baada ya kufanyika Kwa uchunguzi na ubora na sio Kwa hoja za Waziri.

Mashaka niliyonayo kwa Waziri Bashe ni kuwa:

Kama Waziri hajui athari za kimahusiano zinazoweza kuibuka kutokana na kauli tu. Kitendo Cha Waziri Bashe kudai Kwa nini wasingeleta virutubisho wachanganye tukiwaona ,sio rafiki Kwa afya ya diplomasia. Kitendo hicho kinaweza kufikirika kama tuhuma ya usalama. Kabla ya kauli hiyo alitakiwa kuwatumia TBS kuuchunguza mchele.

Marekani ni Moja ya nchi zinazozalisha nataka ( mchele na mahindi) Kwa wingi duniani na kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ,nchi yetu inaweza kukumbwa na baa la njaa na tukahitaji msaada wa Chakula kutoka nje. Je, tutapata wapi nguvu za kuomba msaada kutoka Marekani kama tumeamua kukataa msaada Sasa ?

Pengine kulikuwa na Cha zaidi ambacho hatukijui lakini kama ni hiki kilichopo ,ni vema Waziri Bashe angeliendea suala Hilo Kwa busara, angejiridhisha kwanza na angejua hatua Kwa busara ili tuendelee kuimarisha mahusiano na nchi nyingine.

Kila siku Rais anasisitiza mifumo kusomana ili kuepusha migogoro , na kama mifumo ingekuwa inasomana kusingekuwa na kauli za namna Ile kutoka Kwa Waziri.

Ahsante
 
Virutubisho Mchele mchele

hero-image.fill.size_800x450.v1623362691.jpg
 
Hii ni hoja ya msingi sana, Bashe akanywe na mamlaka husika kwa kutaka kuharibu mahusiano yetu na Wamarekani. January Makamba atoe kauli kwamba kauli ya Bashe sio msimamo rasmi wa serikali ya Tanzania.
Hii habari imenipita wakuu.

Kwani waliopewa msaada ni akina nani? Mayatima ?? Walemavu ?? wazee ?? Wajane ?? ama wananchi wa uchumi wa kati ??
 
Watanzania hatujui tunataka nini.

Kuna wanaosema bora mchele tukatae wengine wanasema tuukubali.

Ila mimi naishauri Marekani WAACHE KUTOA MISAADA AMBAYO HAWAKUOMBWA.

Laiti kama tanzania imgekuwa imeomba huu mchele basi Bashe asingeukataa.

Tatizo sio Tanzania kukataa msaada hapana bali tatizo ni la wamarekani kutoa msaada ambao hawakuombwa.

Wapeleke mchele katika nchi zenye njaa na migogoro ambayo inawaletea uhaba wa chakula.
 
Watanzania hatujui tunataka nini.

Kuna wanaosema bora mchele tukatae wengine wanasema tuukubali.

Ila mimi naishauri marekani WAACHE KUTOA MISAADA AMBAYO HAWAKUOMBWA.

laiti kama tanzania imgekuwa imeomba huu mchele basi Bashe asingeukataa.

Tatizo sio tanzania kukataa msaada hapana bali tatizo ni la wamarekani kutoa msaada ambao hawakuombwa.
Huwa tunawaomba Wamarekani watujengee matundu ya vyoo??
 
Bashe yupo sahihi kwamba, badala ya kuleta Michele, walete hizo pesa wanunue Kwa wakulima watanzania hizo shule zipewe, mimi nashangaa, kwanini wasitupe teknolojia na ujuzi wa kuzalisha huo Michele maana ardhi tunayo kama kweli Wana ni ya kutusaidia? Je, hao wamarekani watatulisha hafi lini?
 
Back
Top Bottom