TBS: Mchele, mafuta ya kupikia ya alizeti na maharage kutoka Marekani, ni Salama kwa Walaji

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limesema mchele, mafuta ya kupikia ya alizeti na maharage ambavyo vyote vimeongezwa Virutubishi vilivyotolewa na Wizara ya Kilimo ya Marekani kwa ushirikiano na Taasisi ya Jumuiya za Kimataifa (Global communities) kwa baadhi ya Shule za Dodoma, vyote ni salama kwa Walaji

TBS imesema taratibu za uingizwaji wa chakula Nchini zilifuatwa ikiwemo ukaguzi na uchunguzi wa Kimaabara

Meneja Uhusiano na Masoko wa TBS, Gladness Kaseka amesema "Utaratibu wa kuongeza virutubishi kwenye chakula (food fortification) unakubalika kitaalamu na hufanyika kwa lengo la kuboresha hali ya lishe kwa walaji.

Pia, soma; Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo: Waagizaji hawakupaswa kuleta mchele wa Msaada kutoka Marekani kwani Tanzania ina hazina ya mchele

IMG_20240318_070126_464.jpg
 
View attachment 2937867
Swala sio usalama,kwani Tanzania tuna njaa Hadi tupewe Msaada? Hoja ni kuidhalilisha Nchi.

Pia Waziri amesema waje wanunue mazao yetu.Mwisho angekuwa Mwendazake angestamtimua Mkurugenzi wa TBS
 
Mimi nilishangaa watu walivyokuwa wanatoka povu kuhusu hii ishu. Kwamba NGO iingize vyakula bili idhini ya mamlaka husika??

Alichofanya Waziri ni damage control baada ya watu kuhoji. Hii program iko muda na uongezaji wa virutubishi haujaanza leo na upo kisheria.

Mbona tunakula unga wa ngano, mahindi, mafuta na chumvi vyote vimeongezwa virutubishi, hivyo virutubishi tunateneneza sisi??

BTW wakitaka kutumaliza hawashindwi.. wanaanzia kwenye dawa na chanjo za bure. Hatutaki hiyo misaada tujikwamue kiuchumi!!
 
Wamesha lamba asali bila shaka,mbona kauli zao zinakinzana na za Bashe?
Bashe ni tapeli, serikali ya ccm ni tapel8, kwani wewe ulimuamini alibosema vile? Ulijiuliza kwamba hao wamarekani walifika ghafla na kupost kwamba tunatoa msaada? Unaweza peleka msaada nchi nyingine ghafla?

(taarifa walikua nayo) na kama kawaida watanzania wengi sisi ni mtaji wa wanasiasa maana hatuna tafakari, bashe anasema amewaambia watu wamarwkani kwamba badala ya kuwapa hela wakulima wa marekani wanunue huku kwa wakulima wa tanzania kwa sababu mchele upo, kama mchele upo si wawapelekee huko shuleni?

(Mchele upo mashambani alafu tunasubiri marekani atoe hela ndo tupeleke shule kwa muktadha upi? (Kuna free lunch na wamarekani toka lini)
 
Back
Top Bottom