Azzan Zungu ataka uwepo wa kodi ya uzalendo itakayokatwa kwenye Mitandao ya simu kwa kila Mtanzania

Bungeni mtu akiongea pumba naona bora wangekua wanamzomea tu ingepunguza watu kuongea upuuzi humo ndani
Alaf hili ndo jina lake rasmi azzan zungu duh
 
Siungi mkono wazo lake, Kwanza nadhani hakuushirikisha ubongo wake wakati anawaza na kutoa wazo Hilo. Serikali inatakiwa ipanue wigo wa frusa kwa wananchi wake ndipo na wigo wa ukusanyaji mapato utapanuka.

Serikali yoyote haiwezi kuendelea kwa kuwafanya wanachi wake watumwa kwa kuwanyonya na kuwaongezea majukumu makubwa Sana ya kuipatia serikali pesa Huku wao serikali hio hela wanaendea kununulia ndege zisizo mfaidisha mwanachi.
 
Kwanza kodi ya uzalendo ndo kodi gani hiyo
Mbunge wa Ilala, Azzan Zungu ametaka kuwepo na kodi ya uzalendo itakayokatwa katika mitandao ya simu kwa kila Mtanzania kwa siku kama chanzo kipya cha mapato kwa Serikali...
 
Posho zote zikiwemo za wabunge zikatwe kodi. Chanzo kipya
Mkuu naomba na kubali nitofautiane na wewe. Huwezi kutoza posho zote Kodi. Kodi izingatie unono wa posho yenyewe. Posho za kutisha na zinazotokana na majukumu yanayojirudia yatozwe kodi maradufu.
 
Kila muamala kwa benki, kwa simu n.k serikali inapata pesa.

Kila tukiweka vocha serikali inachikua kodi.

Sasa huyu muuza unga anataka nini tena?

Anadhani tumesahau alivyoua vijana aliokuwa akiwatuma Uchina kufuata heroine?
 
Mbunge wa Ilala, Azzan Zungu ametaka kuwepo na kodi ya uzalendo itakayokatwa katika mitandao ya simu kwa kila Mtanzania kwa siku kama chanzo kipya cha mapato kwa Serikali....
Wabunge wengine hawana huruma na watanzania. Suala la muhimu ni kupanua vyanzo vya mapato na sio kuwanyonya watanzania.
 
Mbunge wa Ilala, Azzan Zungu ametaka kuwepo na kodi ya uzalendo itakayokatwa katika mitandao ya simu kwa kila Mtanzania kwa siku kama chanzo kipya cha mapato kwa Serikali.

Amesema kiasi hicho kikikatwa kwa Watanzania milioni 30 kati ya wote waliopo nchini huweza kufikisha shilingi bilioni 540 kwa kila siku.

View attachment 1758533
Chee ilala walichagua kitu cha ajabu
 
Ashazeeka kichwa akifanyi kazi tena inatakiwa apumzike tuu yaani wao wanafikiri kuumiza wananchi kila kukicha na kututangazia wamealikwa kufuturu na Rais azungumzii wakatwe hela zao ili kuonyesha huo uzalendo anaosema anataka kuwabebesha mzigo wananchi tena huku vifurushi tuu havieleweki...
 
Mbunge wa Ilala, Azzan Zungu ametaka kuwepo na kodi ya uzalendo itakayokatwa katika mitandao ya simu kwa kila Mtanzania kwa siku kama chanzo kipya cha mapato kwa Serikali.

Amesema kiasi hicho kikikatwa kwa Watanzania milioni 30 kati ya wote waliopo nchini huweza kufikisha shilingi bilioni 540 kwa kila siku.

View attachment 1758533
Huyu dingi anazeeka vibaya!

Kweli anayeshiba hajui maana ya njaa!

Pamoja na hoja yake kuwa mbaya,hata hesabu hajui kabisa. Au mleta hoja umemuwekea maneno mdomoni? Kama ni yeye aliyesema hesabu ya kupata bilioni 540 kwa siku kutoka kwa watumiaji wa simu anaota ndoto za mchana.

Kama watumiaji wote wa simu kulingana na hesabu yake ya 30m watakatwa sh 50 zitapatokana mil150. Ili kupata hizo bilioni zake inabidi kila mtumiaji akatwe 18,000!
 
Baba aliniambia "mwanangu ata wajinga na wapumbavu nao pia huzeeka na sio kila alie kiongozi ana akili timamu"
 
Azzan Zungu anadhani kutumia simu ni anasa!

Hajui kuna wananchi wanastrugle hata kuweka 200 tu waweze kupata sms!
 
Back
Top Bottom