Azzan Zungu ataka uwepo wa kodi ya uzalendo itakayokatwa kwenye Mitandao ya simu kwa kila Mtanzania

Mu7

JF-Expert Member
Jun 15, 2013
804
1,000
Serikali ifanyie kazi Ushauri huu Mzuri sana. Hata isipoitwa kodi ya Uzalendo lakini HAKIKA HIKI NI CHANZO KIZURI SANA CHA MAPATO/KODI KWASABABU TANZANIA HII MTU YUPO RADHI AKOSE VINGINE LAKINI SIO KUKOSA BANDO LA KUCHATI KWENYE GROUP NA TWITTER KUFUATIA MANGE, KIGOGO, KAJALA NA PAULA
Kumbe na ww watu kuchati kunakuuma eeh?? Wachawi mko wengi Tanzania hii Wallah!!!
 

chivala

Member
Apr 13, 2021
76
125
Mbunge wa Ilala, Azzan Zungu ametaka kuwepo na kodi ya uzalendo itakayokatwa katika mitandao ya simu kwa kila Mtanzania kwa siku kama chanzo kipya cha mapato kwa Serikali...
Wazo lake hilo la kodi ya UZALENDO linawahusu watu wenye UZALENDO sio WAZALENDO. maana yake unaweza ukawa MZALENDO lakini huna UZALENDO Kwa hivyo, hiyo nikodi ya hiyari inayo wahusu watu maalum wenye UZALENDO
 

Muite

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
702
1,000
Kumbe na ww watu kuchati kunakuuma eeh?? Wachawi mko wengi Tanzania hii Wallah!!!
Kwani Kodi ikiongezwa Utaacha kutumia Simu? Obviously utatumia tu, Maisha ya Kijamaa yametudekeza sana ndio maana tunataka kila kitu bure tu. Hata Bia ikiongezwa Kodi mnalalama tu.

Kweli waganga wa kienyeji mko wengi Tanzania hii Wallah!!!
 

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
35,116
2,000
Kila muamala wa simu tunalipa kodi. Yeye aseme tu wanatafuta njia ya kurudisha kodi ya kichwa pengine mambo ni magumu huko kwenye chungu kikuu. Tumeona kwenye yatokanayo na bei za miamala.
Hawa makuma wakatwe wao hela ili watie akili maana wanaishi kama wako peponi with 0.0005% productive level
 

1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
5,067
2,000
Sisi waafrika ndio wapumbavu kabisa.

Hivi mtu kama Azani Zungu amepataje ubunge wakati kuna Wafrika wenzetu waadilifu waligombea wanampa yule sijui ni Beberu kutoka nchi gani waliotunyonya tangu babu zao mpaka leo wameendelea kunufaikwa rasilimali za nchi hii bila kutoa jasho zaidi ya kucheza madili na wanasiasa na watawala kwa rushwa.

Kwa nini atamani 50 ya maskini wakati wao ni matajiri waliotunyonya nchini kwetu na kuingia bungeni kwa rushwa na kubebwa kwenda kula mishahara inayotokana na kodi za wanyonge wanaolipwa mishahara isiyofika laki 5.
Watanzania wamepumbazwa sana na CCM kuwakumbatia wezi na kujifanya ni malaika wakati ndio walioua uchumi wa nchi hii.

Chanzo gani cha fedha za kadafu zinazotokana na vimishahara na vibiashara vya kuuza karanga.

Nchi ina Gesi na Urenium halafu inakua na wabunge waliojaza ma..... kichwani.

Hivi wangemsikiliza Mhongo na kumwelewa wakati anakuja na sera za Mafuta na Gesi leo si tungekua tuna Export Gesi Afriaka nzika kama Urusi inavyouza Gesi ulaya nzima na ndio maana inawawahemea wazungu kisogoni na wanafyata mikia.
Watanzania na Wazalendo Feki badala ya kuweka sheria kali dhidi ya wezi walioko madarakani inaweka sheria ngumu kwa wakezaji ambao wanakuja na mitaji yao.

Nyonga mawaziri wezi , funga wakurugenzi na makatibu wezi walarushwa nchi itasonga mbele. Ooh wazungu wanatuibia , wakati kuna mawaziri wanaoingia nao mikataba ha siri na kujipa hisa na rushwa za kila aina.

CCM kuwani Sirias. Wizi upo kwenye mioyo ya Wana CCM wanaoiba kura . Mtu anaiba kura atashindwaje kuiba fedha na mali za umma. Hapo ndio Marais wote waliposhindwa na kuonyesha kuwa wote ni Wabinafsi na waska Mali kwa mgongo wa kujofanya wazalendo.
Haiwezekani mtu aibe kura za serikali za mitaa kisha awe ni mtu Mwadilifu. Never ever. Uadilifu unaonekana pale mtu anapoweza kumwambia mtu wewe ni ndugu yangu na mwanachama wa chama changu lakini umeshindwa kwenye kura kwa hiyo siwezi kukupa ushindi kwa dhulma. Uovu mkubwa unaofanywa na wanasiasa wa CCM umeligharimu sana Taifa mana Mungu anaendelea kuingilia kati na kulinyoosha Taifa kwa haki.
Ukisema wewe ni mzalendo uwe mzalendo mwenye kutenda haki kwa wote mana wote ni watu wako ,ukibagua basi wewe sio mzalendo bali ni Mtu aliyepambana kujenga maisha bora ya familia yake kupitia Kodi za wananchi maskini
 

cool d

JF-Expert Member
Jan 20, 2015
882
1,000
Aache huo ujinga waongeze gharama na matumizi yatashuka hizo hela zitatoka wapi? Vyanzo vya mapato serikali imevikalia Kama maji dar tu mjini maji hayajawafikia wananchi na umeme hivyo hivyo kuna hela zingepatikana nyingi tu.
 

Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
4,269
2,000
Haya bhana! Angelikuwa mtu mwingine ningesema amekumbwa na lishe duni utotoni
 

Mpandisha mishahara

JF-Expert Member
Mar 1, 2014
1,237
2,000
Mbunge wa Ilala, Azzan Zungu ametaka kuwepo na kodi ya uzalendo itakayokatwa katika mitandao ya simu kwa kila Mtanzania kwa siku kama chanzo kipya cha mapato kwa Serikali.

Amesema kiasi hicho kikikatwa kwa Watanzania milioni 30 kati ya wote waliopo nchini huweza kufikisha shilingi bilioni 540 kwa kila siku.

View attachment 1758533
Akili yake imeganda, Ni akili barafu
 

mjombakim

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
842
1,000
Watakuja kuuza figo zetu hawa watu maana kutanua wigo wa kodi kwao ni kumpokonya mwana Nchi kile alicho nacho!
 

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
22,509
2,000
Mbunge wa Ilala, Azzan Zungu ametaka kuwepo na kodi ya uzalendo itakayokatwa katika mitandao ya simu kwa kila Mtanzania kwa siku kama chanzo kipya cha mapato kwa Serikali.

Amesema kiasi hicho kikikatwa kwa Watanzania milioni 30 kati ya wote waliopo nchini huweza kufikisha shilingi bilioni 540 kwa kila siku.

View attachment 1758533
Dah...!!!
Kodi ya uzalendo...!!! Hivi wale tunaoitwa SIYO wazalendo, kodi hiyo tutakatwa?
 

dndagula

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
511
500
Mbunge wa Ilala, Azzan Zungu ametaka kuwepo na kodi ya uzalendo itakayokatwa katika mitandao ya simu kwa kila Mtanzania kwa siku kama chanzo kipya cha mapato kwa Serikali.

Amesema kiasi hicho kikikatwa kwa Watanzania milioni 30 kati ya wote waliopo nchini huweza kufikisha shilingi bilioni 540 kwa kila siku.

View attachment 1758533
Nakubaliana na wewe lakini pia taxi bubu nchini ziandikishwe na kupewa sticker kulipia kodi ya shs 30000/= kwa mwezi. Chanzo kipya sasa taxi hizo ni nyingi na zinaingiza pato lisilollipiwa kodi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom