Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 64,622
- 110,304
Hakuna hiyo elimu, hukuelewa tu wakati unafundishwa au aliyekufundisha alikuwa haelewi vizuri anachokufundisha.Elimu potofu ya mzungu - Darwinism
Hakuna hiyo elimu, hukuelewa tu wakati unafundishwa au aliyekufundisha alikuwa haelewi vizuri anachokufundisha.Elimu potofu ya mzungu - Darwinism
Watu wa dini bana
Jiwe na mmea.Kiuhalisia, huwezi kuutambua au kuupima uthabiti wa muundo fulani bila kuwa na rejea (reference) ya muundo mwingine legelege au usio thabiti.
Sio maneno mengi.Maneno meeeengi,
kama Mungu ni muweza wa yote, kwa nini asingeumba dunia ambayo watu wanakua kupitia changamoto bila kuwepo mateso makubwa yasiyo na ulazima? Kwa nini growth lazima ije na mtoto kufa, kansa, njaa au maafa?
Ni mbaya kwa sababu wewe umeruhusu ubongo wako ukubali ni mbaya na unauita mbaya.Ugonjwa ni ukweli lakin mbaya. Not just an arbitrary alternative of well being
Suala si huyu anafanya hivi au huyu hafanyi hivi. Suala ni kwa nini huyu anafanya hivi na huyu afanyi hivi. Ni uelewa.Anayeogopa magonjwa ni yule anayekimbia kuomba hata marehemu na vitu visivyokuwepo ,ilimradi ajidanganye kwamba itamsaidia kupona.au hata akifa kwamba ataishi Tena.
Haha mkuu LIKUD unaongea ukweli mchungu sanaa.Atheists wengi kabla hawajawa Atheists wali kuwa 👇👇👇
Very religious people. And because of that they developed a " Entitlement Mentality".Kwamba kwa sababu wao ni " Righteous People" basi wapo entitled kuwa blessed by God, kuwa protected against all bad things. Chochote wakimuomba Mungu awape on time. Sasa walipokosa hilo wakaamua kuwa " Atheists"
Unaongea mambo nje na uhalisia. We ukipata tatizo unahitimisha ni ukweli tu bas au unatafuta suruhisho?Ni mbaya kwa sababu wewe umeruhusu ubongo wako ukubali ni mbaya na unauita mbaya.
Bali wewe unasema nafurahia haya?Ubongo wako umefungwa na "nitapata faida gani"? Huwezi kufikiri nini chema cha kufanya katika haya. Unafikiri niondolee haya.
Kwa mtazamo huo wako ,japo sijabaini ni kutoka dini gani , ni dhahiri hauna msingi wowote wa maadili ,maana umekataa hakuna baya, pia utakataa umuhim wa utashi/utendaji wa binadamu.Mwili ukiumwa unasema niondolee haya badala ya nini chema cha kufa katika haya? Ndio sababu unasema ugonjwa ni dhidi ya siha njema. Hili ni tatizo lako sio ugonjwa.
Tatizo la kutokuwa na uelewa wa kina wa mambo na elimu ya vitu.
Shukran mkuu.Ukisema kuna uovu na mateso maana yake unaamini kuna wema na haki, sasa swali ni hili, bila Mungu, unapata wapi kipimo cha ulimwengu mzima cha kusema hiki ni kibaya na hiki ni kizuri?
Kwenye u-atheist na nadharia ya evolution, hakuna uovu, kuna viumbe wenye nguvu kuwadhuru wanyonge tu ili wasurvive, huoni unapotaja uovu, unathibitisha kuwepo kwa sheria ya Mungu moyoni mwako bila wewe kujua?
Kwa hiyo atheist wanamtazamo mmoja kumbe?Acha kuwasingizia Atheists ujinga wako wa kidini. Atheists hawasemi kitanda kimetengenezwa na mtu kwa sababu ni mashine, pia msingi wa atheists hauko katika kumuona mungu au kumjua bala katika kufahamu.
"Kitu kuwepo hakithibitishi nani aliyekiumba". Kama ni hivyo kinathibitisha nini? Mawazo?Na kusema “kifo ni ukweli” au “ugonjwa ni ukweli” si jibu. Kitu kuwepo hakuthibitishi nani aliyekiumba.
Kwa Atheists mtazamo sio kitu muhimu. Data, repeatable process na uthibitisho ndio muhimu.Kwa hiyo atheist wanamtazamo mmoja kumbe?
Nyumba imejengwa na fundi Juma wa Kimara"Kitu kuwepo hakithibitishi nani aliyekiumba". Kama ni hivyo kinathibitisha nini? Mawazo?
Fikiria nyumba kama kitu kilichopo. Imejengwa na matofali: Ina ukuta. Ina milango. Ina madirisha. Ina vyumba vya kulala. Ina sebule, mpangilio.
NYUMBA = Ushahidi
Ushahidi wa vitu + Ushahidi wa mpangilio + Ushahidi wa akili nyuma yake.
Matofali bila mjenzi = Malundi
Mjenzi bila matofali = Mawazo tu
Nyumba = Matofali + Mjenzi wakiungana.
Suala si kwamba uthibitisho sio muhimu. Ni muhimu. Na ni muhimu kwa sababu ni jaribio letu (sis binadamu) la kukaribia ukweli.Hapa umefanya non sequitur, umeonesha viumbe vina tabia fulani, halafu ukaruka kusema lazima kuna akili iliyoviumba. Hiyo connection bado hujaithibitisha.
Sasa unaweza kuona tatizo lako ni nini?Nyumba imejengwa na fundi Juma wa Kimara
Tuambie mjenzi wa Dunia Yuko wapi tukamuone kama fundi Juma.
Madai yako ya Ujenzi wa nyumba yana ushahidi wa mjenzi.
Tunaomba utuoneshe evidence ya mjenzi wa Dunia
Reasoning gani hii mkuu, kwamba umewahi kumuona simba akienda chooni akishusha suruali kisha akimaliza anapandisha?.Tuonyeshe ushahidi unao onyesha lazima binadamu aabudu au kiumbe chochote kile?
Na kwa nini iwe binadamu tu, na sio Simba, Nyangumi au Tembo?
Hivyo vitu ulivyovitaja vipo katika ulimwengu huu au ule ulimwengu ulioufafanisha na kufikia hitimisho kuwa ulimwengu wetu ni thabiti?Jiwe na mmea.
Mimea na wanyama.
Binadamu na wanyama.
Jua na sayari.
Ulijuaje?Baada ya kujua kuwa Mungu ndo kila kitu
Nili achana na drama za ku question uwepo wake