Atheists wanaweza kuwa wagonjwa wa akili?

Atheists wanaweza kuwa wagonjwa wa akili?

Ulijuaje?
Ni baada ya kujua kila kitu ni kimoja...
We are one, separation is an illusion..

GOD is a culmination of all.

We are just the expression of that.

God, in us and us in God
 
Sasa unaweza kuona tatizo lako ni nini?

Ni uelewa.

Una kubali mpangilio wa ulimwengu, nyumba. Lakini unakana hujui nyuma ya huo mpangilio kuna akili, fundi Juma.

Ajabu!
Nyumba inatuthibitishia uwepo wa fundi kwa sababu tuna ushahidi wa mafundi walioijenga. Ulimwengu haututhibitishii moja kwa moja uwepo wa huyo Mungu alieiumba , kama yupo tuoneshe kama Ambavyo tunaweza kukuonesha FUNDI JUMA.
 
Ni baada ya kujua kila kitu ni kimoja...
We are one, separation is an illusion..

GOD is a culmination of all.

We are just the expression of that.

God, in us and us in God
Dini zinazaa vichaa sana

Unasema ‘everything is one’ na separation ni illusion. Mimi na wewe tuna miili tofauti, DNA tofauti, consciousness tofauti, kumbukumbu tofauti na uzoefu tofauti. Ni ushahidi gani unaothibitisha kwamba tofauti hizo ni illusion?


Ukisema Mungu ni culmination of all, basi kila kitu ni sehemu ya Mungu? Kama ndiyo, uovu, mauaji, magonjwa na mateso pia ni sehemu ya Mungu?


Na ukisema ‘God is in us and us in God’, je, sisi ni Mungu mwenyewe au ni sehemu ya Mungu? Kama sisi ni Mungu, kwa nini mimi sina uwezo, ujuzi na ufahamu wa Mungu?
 
Maandiko ambayo ndio msingi wa dini (UKRISTO) yanasema wale wanaoisikia sauti ya Mungu na kutii hao ndio wanaunda taifa teule la Mungu (kut 19:5). Sauti ya Mungu ni Agalo (mkataba) kwahiyo kama kuna agano maana yake kuna vitu viwili (HAKI & WAJIBU) ninapolielewa agano na kutenda kama linavyoniagiza ndipo ninapokuwa mwenye haki mbele za Mungu, Ndipo Mungu anaweza kupendezwa nami na kunipa baraka alizoahidi.

Jambo tunalotakiwa kuelewa ni kuwa Mungu katika kila enzi huchaguwa watu na kuweka nao Agano mf (israel/ wayahudi) ndio maana tunamuita Mungu wa maagano. Kama ilivyokuwa tangu enzi ya Abrahamu Mungu alisimama tuu na taifa lile aliloweka naLo Agano japokuwa mataifa mengine yalikuwapo lakini Mungu alisimama na Israel pekee sababu ndio alioweka nao agano. Hata wewe leo huwezi wajibika kwa mtu pasipo makubaliano baina yenu.

Maandiko yanaonyesha Israel walioteuliwa na kupewa agano na Mungu kupitia mitume na manabii walikuwa na ukaidi katika kuenda sawa na maagizo ya Mungu (kukosa kuitii sauti ya Mungu). Mungu kupitia manabii akaahidi kuikomboa israel kwa kumleta MFALME, MWANA WA PEKEE, YESU KRISTO, ambaye alikuja kwa mujibu wa maandiko ambayo wayahudi hawa walikuwa wakiyasoma kila sabato, Ajabu ni kwamba walishindwa kumtambua na kumpokea, Ahadi ya kuja kwa mkombozi walikuwa nayo na walikuwa wakikiri kuwa Mungu aliwaahidi mkombozi kutokea shina la Daudi. Yet alipokuja walimpinga na kumsulubisha (matend 13:27)

Kwakumkataa yesu na kumsulubisha (math 27:20-26) baraka iliondolewa kwao kwakuwa hawakuweza kutii na kulishika Agano (mapenzi ya Mungu) la Mungu ambapo ilikuwa ni wao kumpokea na kumsikiliza yesu. Ndipo lilipokuja Agano Jipya ambalo hili tofauti na la mwanzo huitaji kuwa muisraeli ili kuwa taifa la Mungu unachoitaji ni kumkiri yesu nakuamini kuwa ndiye bwana na mwokozi (MKRISTO) (sound simple but its not) (math 8:11-13). Kupitia kristo tunaesabiwa haki kwa IMANI (warum 10:5). kuna hivi vitu vitatu vya msingi sana katika maisha ya imani (MAARIFA, IMANI, MATENDO).

IMANI msingi wake ni MAARIFA ili niweze kukuamini natakiwa kukujua kwanza then IMANI yangu kwako itapimwa kupitia matendo yangu. Mfn ninaamka kula siku ninawai kazini na kutimiza majukumu yangu kama tulivyokubaliana na boss wangu kwa sababu ninafahamu fika(MAARIFA) boss wangu(KAMPUNI) anaouwezo wa kulipa kile tulichokubaliana. Yesu mwenyewe anasema (yoh 14:21) kumpenda yeye ni kushika amri zake (neno lake) Ambalo ndilo Agano, ndiyo mapenzi ya Mungu aliyotumwa kuja kutufundisha.

MHUB 1:9, Inasema hakuna jipya chini ya jua. WAYAHUDI (VIONGOZI WA DINI) WALIKUA NA AGANO LA KALE (MAANDIKO) WALIKUA WAKIISHI MAISHA YA IMANI KAMA SISI SASA, LAKINI WALISHINDWA KULISHIKA AGANO, WALIKUWA NA IMANI AMBAO MSINGI WAKE ULIKUWA NI MAWAZO YA WANADAMU (Isaya 29:13) TUKUMBUKE MAWAZO YA MUNGU SI YA MWANADAMU NI MBINGU NA ARDHI. BIBLIA IMEFUNGWA KWA MAFUMBO NA MIFANO NI PALE TUU UTAKAPOELEWA MAANA ZA MAFUMBO NA MIFANO ILIYOTUMIKA NDIPO UTAKAPO WEZA KUELEWA UJUMBE ULIOPO. MUNGU PEKEE NDIO ANAYEWEZA KUFICHUA MAFUMBO HAYA YAANI MAANA YA YOTE YALIYOFICHWA KWENYE BIBLIA ZINAPATIKANA KUPITIA BIBLIA PEKEE. HAPO NDIPO UTAKAPOWEZA KUISOMA BIBLIA NA USIONE CONTRADICTION YEYOTE. (yerem 33:3)(math 5:6)(math 7:7), Ufalme wa MUNGU hauji kwa kuutamani,kuulilia, tunapaswa kuutafuta na kuyajua MAANDKIKO (AGANO) yasiyoghushiwa ndio njia ya kuuendea ufalme wa MUNGU.​



🙂🙂
 
Hivyo vitu ulivyovitaja vipo katika ulimwengu huu au ule ulimwengu ulioufafanisha na kufikia hitimisho kuwa ulimwengu wetu ni thabiti?
Binadamu hadi sasa hajafanikiwa kufika au kwenda ulimwengu mwingine.
 
Nyumba inatuthibitishia uwepo wa fundi kwa sababu tuna ushahidi wa mafundi walioijenga. Ulimwengu haututhibitishii moja kwa moja uwepo wa huyo Mungu alieiumba , kama yupo tuoneshe kama Ambavyo tunaweza kukuonesha FUNDI JUMA.
Si andiki kubishana.
Uelewa.
 
Uumbaji ni creation Yani unaanza kutengeneza kitu from the scratch, energy iko transformed tu sasa mbona wewe unaibatiza jina la uumbaji? Hebu nisaidie hapo
TUMIA AKILI MUNGU ANAUMBA KWA KUIFANYA ENERGY ATAKAVYO
 
Back
Top Bottom