Atheists wanaweza kuwa wagonjwa wa akili?

Atheists wanaweza kuwa wagonjwa wa akili?

Kuna mwanafalsafa wa miaka ya 1770s anaitwa Paley ndio aliyeanzisha hii hoja ya teleological.

Yeye alitumia mfano wa saa.

Yeye alisema "ukienda beach ukawa unatembea fukweni halafu ukaokota saa, basi ni lazima utasema tu kuwa ile saa imetengenezwa na kuna mtu aliyeileta hapo"

Then kupitia mfano huo akaja kuhusianisha na ulimwengu na dhana ya Mungu katika uhusika wa kuumba huo ulimwengu.

Kwasababu saa imelazimika kuwa na muundaji wake, je hiyo inafanya na ulimwengu kuhitaji muumbaji?

Aliyekuta saa fukweni, akiendelea na matembezi yake akaokota mwamvuli je utafikiria kuwa aliyetengeneza saa ndio aliyetengeneza mwamvuli?

Huyo mtu akaendelea na matembezi akakuta midoli, je atafikiria kuwa aliyetengeneza saa na mwamvuli ndio huyo huyo aliyetengeneza na huo mwamvuli?

Je hii haiwezi kuhusisha watengenezaji wengi tofauti?

Je hii haiwezi kuhusisha watengenezaji wengi tofauti tofauti wa ulimwengu kuwa wamewajibika kwa kila kilichoumbwa?
Kwenye falsafa hiyo hiyo unayotaka kuigusia, kuna kanuni inaitwa occam’s razor inasema kwamba jibu rahisi na lenye mantiki zaidi ndilo la kweli. Kuliko kubuni nadharia ya kamati ya miungu elfu moja waliokaa kikao kuunda ulimwengu, ni rahisi na ina mantiki zaidi kukubali uwepo wa Muumba Mmoja Mwenye Nguvu Zote.
 
Umekiri mwenyewe, hawajui, sasa kama wanasayansi wenyewe wanajibu we don’t know kuhusu kilichokuwepo kabla ya Big Bang, nyinyi atheists mnaoibuka na kusema hakuna Mungu" mmetoa wapi hiyo absolute confidence?
Asilimia kubwa ya atheists wa leo wanasema hakuna mungu kwa muktadha wa "Abrahamic god" anayezungumzwa na Wakristo, Waislamu na Wayahudi, huyo wana uhakika hayupo.

Pia wanaona uwezekano wa kutokuwepo mungu wa aina yeyote/ yoyote ni mkubwa zaidi kutokana na unresolvable contradictions zilizopo au zinazoibuka kutokana na madai ya uwepo wa mungu.
 
Asilimia kubwa ya atheists wa leo wanasema hakuna mungu kwa muktadha wa "Abrahamic god" anayezungumzwa na Wakristo, Waislamu na Wayahudi, huyo wana uhakika hayupo.

Pia wanaona uwezekano wa kutokuwepo mungu wa aina yoyote ni mkubwa zaidi
Wewe unaamini nini hapo?
 
Asilimia kubwa ya atheists wa leo wanasema hakuna mungu kwa muktadha wa "Abrahamic god" anayezungumzwa na Wakristo, Waislamu na Wayahudi, huyo wana uhakika hayupo.

Pia wanaona uwezekano wa kutokuwepo mungu wa aina yeyote/ yoyote ni mkubwa zaidi kutokana na unresolvable contradictions zilizopo au zinazoibuka kutokana na madai ya uwepo wa mungu.
Yaani mna absolute certainty kwamba Mungu wa Ibrahimu hayupo, lakini mkiulizwa nini kiko beyond the Big Bang mnasema hamjui? Ndio nini sasa?
 
Mimi sijui tumetokea wapi ila Mungu huyu wa Wakristo na Waislamu sidhani kama yupo
Kama Mungu yupo, basi sio huyo Mungu wa Ibrahimu
Hujui ulipotoka lakini unajua nani hayupo? Hiyo logic umeitoa wapi mzee? Kama hujui ukweli ni upi, unakuwaje na uhakika na uongo? Huwezi kusema jibu la hesabu ni kosa wakati wewe mwenyewe hujui jibu sahihi ni nini. Hiyo ni chuki yako tu na dini.
 
Ndiyo,
Ni kama vile kusema sijui nani ni rais wa Vanuatu au hata sijui kabisa kama Vanuatu ina rais ila nina uhakika sio Donald Trump.
Mfano wako hauna uhusiano kabisa na hoja iliyopo. Donald Trump unamjua sifa zake, uraia wake, na mipaka yake ya kijiografia, ndio maana una uhakika hawezi kuwa rais wa Vanuatu. Lakini Mungu humjui, hujasoma habari zake, na humuelewi, sasa huo uhakika kwamba sio yeye" unautoa wapi kama sio kukariri?
 
Wewe unaamini nini hapo?
Sijui kama yupo, sijali sana kama yupo au hayupo na pia kama yupo nafikiri hata yeye hajali kinachoendelea ulimwenguni.
Kuhusu Abrahamic god huyo ni uhakika hayupo. Biblia, Quran na Tanakh ni story tu za fiction za Mashariki ya kati kutoka jamii mbalimbali zilizorithishwa kutoka kizazi hadi kizazi kama sehemu ya binadamu kutafuta meaning.
 
Mfano wako hauna uhusiano kabisa na hoja iliyopo. Donald Trump unamjua sifa zake, uraia wake, na mipaka yake ya kijiografia, ndio maana una uhakika hawezi kuwa rais wa Vanuatu. Lakini Mungu humjui, hujasoma habari zake, na humuelewi, sasa huo uhakika kwamba sio yeye" unautoa wapi kama sio kukariri?
Mungu wa Abraham nimemsoma katika vitabu vyake na kuwasikiliza waamini wake kuhusu sifa zake, kupitia ufahamu huo nimeona uwezekano wa uwepo wake hakuna hasa zaidi nikiangalia the problem of evil, morality and suffering.
 
Hujui ulipotoka lakini unajua nani hayupo? Hiyo logic umeitoa wapi mzee? Kama hujui ukweli ni upi, unakuwaje na uhakika na uongo? Huwezi kusema jibu la hesabu ni kosa wakati wewe mwenyewe hujui jibu sahihi ni nini. Hiyo ni chuki yako tu na dini.
Tufanye ni chuki na dini yeah
Ila mimi siamini vitu ambavyo akilini mwangu havimake sense. Eti ni muweza wa yote ila anaamua tu kuacha watu duniani waendelee kuteseka na kufanyiana ukatili. Au tukifa ipo siku tutapaa kwenda kuonana nae. Ana huruma ila atatuchoma moto tusiomwamini, tena moto wa milele. Kwenye Biblia kaua watu wengi, anaonekana ni short tempered na mwenye hasira za karibu. Ana madhaifu mengi sana
 
Mungu wa Abraham nimemsoma katika vitabu vyake na kuwasikiliza waamini wake kuhusu sifa zake, kupitia ufahamu huo nimeona uwezekano wa uwepo wake hakuna hasa zaidi nikiangalia the problem of evil, morality and suffering.
Ukisema kuna uovu na mateso maana yake unaamini kuna wema na haki, sasa swali ni hili, bila Mungu, unapata wapi kipimo cha ulimwengu mzima cha kusema hiki ni kibaya na hiki ni kizuri?

Kwenye u-atheist na nadharia ya evolution, hakuna uovu, kuna viumbe wenye nguvu kuwadhuru wanyonge tu ili wasurvive, huoni unapotaja uovu, unathibitisha kuwepo kwa sheria ya Mungu moyoni mwako bila wewe kujua?
 
Hawafahamu chochote kuhusu mungu, hawajaona uthibitisho au ushahidi wake unaopimika mpaka sasa, ndio maana wanataka nyie mnaodai mnaamini yupo mthibitishe uwepo wake.
Kama hawa fahamu kwa nini wanasema hayupo?
 
Hujui ulipotoka lakini unajua nani hayupo? Hiyo logic umeitoa wapi mzee? Kama hujui ukweli ni upi, unakuwaje na uhakika na uongo? Huwezi kusema jibu la hesabu ni kosa wakati wewe mwenyewe hujui jibu sahihi ni nini. Hiyo ni chuki yako tu na dini.
Mambo mengi tu tunaweza kujua ni makosa, sio sahihi na haya make sense bila hata kujua usahihi au ukweli ni upi. Watanzania karibia wote wanajua Samia hakupata 98% ya kura na watu milioni 31 hawakupiga kura katika uchaguzi wa 2025 hata kama hawajui namba sahihi za huo uchaguzi ni zipi.
 
Back
Top Bottom