Kim Jong Jr
JF-Expert Member
- Mar 15, 2014
- 12,022
- 22,367
Sawa, nimekuelewa kuhusu energy. Lakini bado sioni Mungu anaingia wapi kwenye hoja yako. Kwamba energy haiwezi kuharibika bali hubadilika kutoka hali moja kwenda nyingine, hakuthibitishi kwamba Mungu yupo. Hilo linaeleza tabia ya energy, si nani aliyeumba energy.Low IQ ..kuna tofauti ya kusema binadamu ana Energy na kusema binadamu ni Energy...wewe kwa akili zako finyu unadhani ni sawa ? Binadamu na vitu vyote ni energy vilikuwako milele katika form tofauti ila vilikuwako ..you can't destroy Energy but energy charge from one form to another
Ok nikukubalie pia kuwa energy imekuwepo milele, kama kuna kitu kinaweza kuwepo milele bila kuhitaji aliyeumba, kwa nini Mungu awe lazima? Kwa nini isiwe energy au reality yenyewe?
Na ukisema Mungu ndiye aliyeumba energy basi tayari umesha jipinga Kwa kusema kuwa energy ni ya milele. Ukisema energy ni ya milele, basi hakuna haja ya kusema kuna mtu aliyeianzisha. Ukisema Mungu ndiye chanzo chake, basi ni lazima uonyeshe ushahidi wa Mungu. Unaruka ruka with EGo halafu unatuita siSI ni low IQ
Kuhusu kuniita low IQ, hilo halijibu hoja. Kama nimekosea, onyesha nilipokosea. IQ yangu haiwezi kufanya hoja ya kweli iwe uongo, wala IQ yako haiwezi kufanya hoja ya uongo iwe kweli.
Kwa hiyo swali langu bado lipo pale pale, Umeonyesha kwamba energy ipo; hujaonyesha kwamba Mungu yupo. Mungu anaingia wapi kwenye hiyo connection?”