4Rs za Rais Samia gumzo kila kona, Padri Kitima, Askofu Mwamakula, Zitto wakoshwa

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC), Charles Kitima, amesema dhamira ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kufanya mageuzi makubwa kwa kutumia falsafa ya uongozi kwa kutumia 4Rs, inajidhihirisha kwa vitendo. Mbalina Padri Kitima, Askofu Emmaus

Mwamakula, ameelezea mageuzi ya Miswada ya Sheria mbalimbali za uchaguzi, kuwa ni dhamira njema ya Rais Dk. Samia kufanya mageuzi nchini.

Mwaka jana, nchi ilipoadhimisha miaka 32 ya kurejea mfumo wa vyama vingi vya siasa, Rais Dk. Samia alitangaza kuongoza nchi kwa falsafa ya 4Rs (kwa kiswahili; Mageuzi, Kujenga, Ustahamilivu na Maridhiano).

KITIMA
Wakizungumza katika mahojiano kwa nyakati tofauti baada ya Bunge kusoma kwa mara ya kwanza miswada mitatu juzi, Kitima alisema Novemba 10, 2023 ni siku ya furaha kwa taifa.

Kitima ambaye amekuwa akitoa maoni mara kwa mara ya namna ya kuimarisha mifumo ya uchaguzi nchini,
alisema Rais Dk. Samia anaiheshimisha Tanzania kimataifa.

"Kama kuna siku ya furaha, basi leo (juzi) taifa letu lina furaha. Watanzania wanatamani uchaguzi huru na wa haki. Miswada hii inakwenda kuleta mageuzi makubwa," alisema Kitima. Akirejea uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2019 na mkuu mwaka 2020, Kitima alisema dosari zake zitazibwa na mabadiliko hayo ya sheria mbalimbali za uchaguzi.

Alifafanua kuwa siyo taswira nzuri kwa nchi ya kidemokrasia Bunge lake kuongozwa na chama kimoja cha siasa, hivyo dhamira ya Rais Dk. Samia kufanya mageuzi ya mitumo ya kisiasa inaleta taswira nzuri kwa nchi kimataifa.

"Hii ndiyo maana ya Rais Samia kuongoza kwa 4R. Aliwahi kusema alipokuwa ziarani Ulaya kwamba, atafanya mageuzi makubwa ya mifumo ya uchaguzi bila kujali kama atapoteza nafasi uchaguzi ukifanyika. Amedhihirisha kwa vitendo," aliongeza
akirejea ongozi wa Rais Dk. Samia kwa kuzingatia 4Rs. Alishauri maoni ya wananchi wa chini, wakiwemo wa vijijni yasikilizwe muda wa kuyapokea ukifika, kwani ndiyo wapiga kura wazuri.

Kuhusu zuio la kiongozi kupita bila kupingwa, alisema hilo ni jambo kubwa na la msingi kwani hakuna kiongozi anayekubalika kwa watu wote.
MWAMAKULA
Akizungumzia dhamira njema ya Rais Samia kuimarisha nguzo za demokrasia nchini, Askofu Mwamakula alisema: "Kila jambo lina mwanzo. Huu ni mwanzo mzuri mno. Ni dhamira ya Rais kufanya mageuzi".

Askofu Mwamakula ambaye mara kwa mara amekuwa akitoa maoni ya kuwepo uchaguzi huru kwa kufanya
mabadiliko ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, alisema kipengele cha kuzuia mgombea kupita bila kupingwa kitaondoa dosari za kukwamishana katika uchaguzi.

Alisema kwa muda mrefu pia wamekuwa wakisisitiza mabadiliko ya sheria za uchaguzi, hivyo kuwasilishwa bungeni kwa miswada hiyo ni mwanzo mzuri.

ZITTO KABWE

Kwa upande wake, Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo, alisema miswada hiyo mitatu kila mmoja una umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya kisiasa nchini Akitolea mfano, Zitto mwanasiasa mpenda maridhiano ya kitaifa na mwenye msimamo wa wastani katika siasa, alisema mgombea kupita bila kupingwa imepigwa marufuku.

Kwa mujibu wa Zitto, kitendo cha wagombea kupita bila kupingwa kilileta shida katika siku za nyuma, hivyo kuondolewa kunaleta matumaini makubwa.

Akizungumzia Sheria ya NEC, Zitto alisema kitendo cha wajumbe wa tume kuomba nafasi, kitajenga taasisi hiyo
kuwa na watu wenye weledi. Pia, alisifia utaratibu wa kumpata Mkurugenzi wa NEC, akisema umewekwa kumpata mtendaji kwä vigezo stahiki.

Kuhusu vyama vya siasa kutoa maoni, alisema miezi mitatu kuanzia hivi sasa vijiandae kutoa maoni yao punde Kamati ya Bunge itakapoanza kuchukua maoni.

"Haya ni mabadiliko makubwa mno kwa nchi. Utakapofika wakati wa kupokea maoni basi tujitokeze. Pia, tunaamini serikali itaendelea kuwa sikivu kupokea maoni tofauti ya kuboresha miswada hii, "alisisitiza Zitto.

Juzi,serikali iliwasilisha bungeni miswada mitatu; mmoja wa mabadiliko ya Sheria ya NEC, wa mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya wagombea wakiwemo wa urais na ubunge.
 
Tusubilie
 
Back
Top Bottom