Askari Polisi amuua kwa Risasi Mlinzi wa Baa ya Boardroom Iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dares Salaam lilipokea taarifa kuwa tarehe 29/11/2023, Saa sita usiku maeneo ya Sinza Mapambano Kinondoni askari wawili walimjeruhi kwa risasi mu mmoja aliyefahamika kwa Jina la Razaki Azan mwenye umri miaka 29 mlinzi binafsi wa Bar itwayo Board room iliyopo Sinza Dar es salaam ambaye baaade alipoteza maisha.

Jeshi la Polisi tayari limewakamata askari hao na mambo ya kisheria yanakamilishwa na watachukuliwa hatua za kisheria haraka Kadri iwezekanavyo kwa kufuata mifumo ya kisheria kiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospital ya Rufaa Mwananyamala kukamilisha uchunguzi.
Screenshot 2023-11-29 at 19.11.28.png

Video hizi zifuatazo chini zinaonesha namna hali ilivyokuwa kabla ya tukio la Askari kufyatua risasi

Sijui dunia inaenda wapi? Hao Sheria ifate mkondo wake mapema maana hakuna aliye na haki ya kumunyang'anya mwenzake haki ya kuishi.Kwa nini wanatembea na siraha Hadi bar? Naisi binadamu tuna shida Sana kwa sasa Mungu tu aingilie Kati ili ulimwengu uwe sehemu salama pa kuishi
 
Wapo wengi wa hivyo, waliovumilia ni hawa coplo ukute Form Four failures hana oa kutokea!
Ni kweli na yeye aliingia akiwa na elimu ya form six akajiongeza akapiga degree ya Law kwa kujisomesha sasa hivi anapiga law school ila anahangaika sana aache kazi mapema. Hao wengine wengi wao ni sababu anakuwa hana option vyeti vyenyewe unakuta vya mchongo anaona bora atulie tu.
 
Sijui dunia inaenda wapi? Hao Sheria ifate mkondo wake mapema maana hakuna aliye na haki ya kumunyang'anya mwenzake haki ya kuishi.Kwa nini wanatembea na siraha Hadi bar? Naisi binadamu tuna shida Sana kwa sasa Mungu tu aingilie Kati ili ulimwengu uwe sehemu salama pa kuishi
Ndugu mbona unataka kumtwisha Mungu mzigo ambao hahusiki? Yaani aingilie polisi kuingia bar na bunduki? Hili ni kosa la ki-mfumo na kama nchi tumeshapoteza mwelekeo. Hakuna tena rule of law, watawala wako busy kulaghai raia na raia wamelala fofofo wanaomba eti Mungu aingilie kati.
 
Ndugu mbona unataka kumtwisha Mungu mzigo ambao hausiki? Yaani aingilie polisi kuingia bar na bunduki? Hili ni kosa la ki-mfumo na kama nchi tumeshapoteza mwelekeo. Hakuna tena rule of law, watawala wako busy kulaghai raia na raia wamelala fofofo wanaomba eti Mungu aingilie kati.
Mungu angekuwepo, kusingekuwa na bunduki.

Uwepo wa bunduki ni ushahidi Mungu hayupo.

Pole kwa wafiwa.
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dares Salaam lilipokea taarifa kuwa tarehe 29/11/2023, Saa sita usiku maeneo ya Sinza Mapambano Kinondoni askari wawili walimjeruhi kwa risasi mu mmoja aliyefahamika kwa Jina la Razaki Azan mwenye umri miaka 29 mlinzi binafsi wa Bar itwayo Board room iliyopo Sinza Dar es salaam ambaye baaade alipoteza maisha.

Jeshi la Polisi tayari limewakamata askari hao na mambo ya kisheria yanakamilishwa na watachukuliwa hatua za kisheria haraka Kadri iwezekanavyo kwa kufuata mifumo ya kisheria kiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospital ya Rufaa Mwananyamala kukamilisha uchunguzi.
View attachment 2828811

View attachment 2828814
Nina mashaka makubwa sana kuhusiana na 'Afya ya Akili' ya Askari Polisi karibu wote wa Tz.
Inajulikana wazi kabisa kwamba "silaha ni kifo," Je, ilikuwaje mpaka Askari Polisi aliyepewa Mafunzo ya kutumia silaha afyatue risasi hovyo na kwa uholera hadi kusababisha kifo cha mtu???????
Nini hasa kilitokea mpaka huyo Askari akalazimika kufyatua risasi na kumuua mtu??? Taarifa hii ya Jeshi la Polisi iko shallow sana, huenda pengine kutokana na uzembe mkubwa uliofanywa na Askari wao, kuweka wazi kila kitu wanaona kama "kulivua nguo" Jeshi lao.
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dares Salaam lilipokea taarifa kuwa tarehe 29/11/2023, Saa sita usiku maeneo ya Sinza Mapambano Kinondoni askari wawili walimjeruhi kwa risasi mu mmoja aliyefahamika kwa Jina la Razaki Azan mwenye umri miaka 29 mlinzi binafsi wa Bar itwayo Board room iliyopo Sinza Dar es salaam ambaye baaade alipoteza maisha.

Jeshi la Polisi tayari limewakamata askari hao na mambo ya kisheria yanakamilishwa na watachukuliwa hatua za kisheria haraka Kadri iwezekanavyo kwa kufuata mifumo ya kisheria kiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospital ya Rufaa Mwananyamala kukamilisha uchunguzi.
View attachment 2828811

View attachment 2828814
Ndugu kwani leo ni saa ngapi na tarehe gani
 
Back
Top Bottom