BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,118
1. Polisi wawili waua kwa risasi mlinzi wa Bar maarufu ya Boardroom iliyopo Sinza Jijini Dar es Salaam.
2. Mlinzi waliyeuwawa kwa risasi anaitwa Razak Anan mwenye umri wa miaka 29 muajiriwa wa Bar ya Boardroom, Sinza
3. Polisi kutoka kituo cha Polisi Mabatini walifika na gari na kupaki nje ya Bar ya Board room na kuanza msako wa Dada poa kwa kusema ni agizo la Mkuu wa Mkoa.
4. Lakini Polisi hao walikuwa wakiwatoa nje wahudumu na wateja katika Bar hiyo ambao walikuwa na min skirt (sketi fupi) kwa kusema kuwa watu hao kwa mavazi yao walikuwa wanajiuza katika Bar hiyo ya usiku (night Club)
5. Wateja wengine walipona udhalilishaji na manyanyaso hayo walianza kuondoka katika Bar hiyo ya Boardroom na waliobakia waligoma kutolewaa nje ya Bar kwa muonekano wa mavazi yao.
5. CCTV za Bar ya Board room inayonyesha Polisi hao walipoona wadada wanakata kufananishwa na machangudoa walienda katika gari na kuchujua silaha aina ya bunduki (SMG) na kuanza kutishia wateja na kuelekezea katika meza za wateja waliokuwa wanakunywa katika Bar hiyo.
6. Polisi hao ambao walikuwa wanaonekana wametumia kilevi walifyatua risasi kadhaa kisha kuondoka na gari yao kutoka eneo hilo la Bar ya Boardroom na baada ya kuondoka wateja walirejea na kukuta mlinzi mmoja wapo akiwa amelala chini akiwa amepigwa risasi na kuvuja damu nyingi (video inaonyesha damu ya marehemu)
7. Mlinzi wa Board room alifariki njiani akiwa katika Bajaji anakimbizwa hospitali.
8. Matukio ya polisi kuvamia sehemu za starehe na nyumba za watu binafsi ni maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambaye anaendesha zoezi la kutafuta madanguro na kusaka madada poa.
9. Leo Mkuu wa Mkoa amesisitiza mauaji kufanywa na polisi ni Jambo la kawaida "Mtu akifia kituo cha polisi tunasema Polisi wameua, Mtu akifia hospitali tunasema ni Mapenzi ya Mungu" RC-DSM, Chalamila
10. Nawakumbusha kulaani tukio lolote la Polisi kuua raia kwa kisingizio chochote kile, Leo kwa huyu kesho kwake.
Boniface Jacob EX Mayor Ubungo
Pia soma >>> Polisi kuua mlinzi wa bar Dar: Je, Chalamila anakwepaje kuwajibika?