BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,118
JESHI la Polisi jijini Dar es Salaam, limewafukuza kazi askari wawili wa Kituo cha Mabatini wanaodaiwa kumuua kwa kumpiga risasi mlinzi wa baa ya Board Room, Riziki Azan (29).
Azan ambaye alikuwa mlinzi wa baa hiyo iliyoko Sinza jijini hapa, aliuawa usiku wa kuamkia Novemba 29, mwaka huu wakati askari hao wakitaka kumkamata muhudumu wa baa hiyo kwa madai anafanya biashara ya kujiuza.
Hata hivyo, siku moja baada ya tukio hilo kutokea, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kupitia Kaimu Kamanda, Gabriel Pupa alitoa taarifa akisema kuwa wanawashikilia askari wiwili wakihusishwa na tukio hilo.
Akizungumza na chombo kimoja cha Habari, Kamanda Pupa amesema askari hao wameshachukuliwa hatua za kinidhamu kwa kufukuzwa kazi huku mmoja wao akifikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji.