Dar es Salaam: Vijana wawili wafariki mikononi mwa polisi

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
4,448
16,313
Vijana wawili ambao ni Bakari Ismail (21) na Shomari Kacheuka maarufu Babuu (22) wamefariki dunia huku vifo vyao vikigubikwa na utata kwakuwa mara ya mwisho December 27,2023 walichukuliwa kwa nguvu nyumbani kwao Vingunguti Jijini Dar es salaam na Watu waliojitambulisha kuwa ni Askari na kisha kupelekwa kusikojulikana na baada ya Familia kuwatafuta bila mafanikio hatimaye December 28,2023 asubuhi miili yao ikafikishwa Amana Hospital na Watu waliojitambulisha ni Askari wakidai miili hiyo wameiokota.

Mzee Swalehe Kacheuka ambaye ni Baba Mzazi wa Shomari ameiambia @AyoTV_ kuwa “Babuu alikuwa anafanya kazi Kariakoo kampuni ya kuuza pikipiki, aliporudi kazini wakaja Wat waliojitambulisha ni Askari ila hawajavaa sare wakamsimamisha kwamba upo chini ya ulinzi akawauliza nimefanyaje wakawa wanabishana wakampiga risasi ya mguu, Kaka yake katoka wakamnyooshea bastola, akaja Rafiki yake Ismail wakati wanamkunja akasogea wakampiga risasi ya mguuni na wakawachukua wote wakaondoka nao, Ismail walimpakia kwenye IST, Bakari wakampakia kwenye Defender”

Kwa upande wake Mzazi wa Shemeji wa Bakari Ismail amesema “Tulipopata taarifa asubuhi December 28,2023 tukaamkia Polisi Buguruni tukaambiwa hawajaletwa, tukazunguka vituo vya polisi karibu sita hatukufanikiwa, tukazunguka Hospitali tukaambiwa hawajaletwa, mida ya saa 8 mchana tukaambiwa kuna miili Amana ambayo imepelekwa na Polisi wakisema wameowakota Vingunguti”

Familia hizo mbili zimesema miili ya Vijana hao imekutwa na matundu ya risasi na macho yao yametobelewa, Ayo TV imefanya jitihada za kulitafuta Jeshi la Polis Kanda Maalum ya Dar es salaam ili kupata taarifa zaidi kuhusu tukio hilo lakini hatujafanikiwa ingawa bado tunaendelea na jitihada za kuwatafuta.

©MillardAyo
 
kwamba upo chini ya ulinzi akawauliza nimefanyaje wakawa wanabishana wakampiga risasi ya mguu, Kaka yake katoka wakamnyooshea bastola, akaja Rafiki yake Ismail wakati wanamkunja akasogea wakampiga risasi ya mguuni na wakawachukua wote wakaondoka nao,
Aiseee yaani Askari anaruhusiwa kupiga raia amabaye hana silaha kwa sababu tu amehoji?

Tutafika tu, hali ilishakuwa mbaya!
 
Vijana wawili ambao ni Bakari Ismail (21) na Shomari Kacheuka maarufu Babuu (22) wamefariki dunia huku vifo vyao vikigubikwa na utata kwakuwa mara ya mwisho December 27,2023 walichukuliwa kwa nguvu nyumbani kwao Vingunguti Jijini Dar es salaam na Watu waliojitambulisha kuwa ni Askari na kisha kupelekwa kusikojulikana na baada ya Familia kuwatafuta bila mafanikio hatimaye December 28,2023 asubuhi miili yao ikafikishwa Amana Hospital na Watu waliojitambulisha ni Askari wakidai miili hiyo wameiokota.

Mzee Swalehe Kacheuka ambaye ni Baba Mzazi wa Shomari ameiambia @AyoTV_ kuwa “Babuu alikuwa anafanya kazi Kariakoo kampuni ya kuuza pikipiki, aliporudi kazini wakaja Wat waliojitambulisha ni Askari ila hawajavaa sare wakamsimamisha kwamba upo chini ya ulinzi akawauliza nimefanyaje wakawa wanabishana wakampiga risasi ya mguu, Kaka yake katoka wakamnyooshea bastola, akaja Rafiki yake Ismail wakati wanamkunja akasogea wakampiga risasi ya mguuni na wakawachukua wote wakaondoka nao, Ismail walimpakia kwenye IST, Bakari wakampakia kwenye Defender”

Kwa upande wake Mzazi wa Shemeji wa Bakari Ismail amesema “Tulipopata taarifa asubuhi December 28,2023 tukaamkia Polisi Buguruni tukaambiwa hawajaletwa, tukazunguka vituo vya polisi karibu sita hatukufanikiwa, tukazunguka Hospitali tukaambiwa hawajaletwa, mida ya saa 8 mchana tukaambiwa kuna miili Amana ambayo imepelekwa na Polisi wakisema wameowakota Vingunguti”

Familia hizo mbili zimesema miili ya Vijana hao imekutwa na matundu ya risasi na macho yao yametobelewa, Ayo TV imefanya jitihada za kulitafuta Jeshi la Polis Kanda Maalum ya Dar es salaam ili kupata taarifa zaidi kuhusu tukio hilo lakini hatujafanikiwa ingawa bado tunaendelea na jitihada za kuwatafuta.
View attachment 2857458

©MillardAyo
Mmmhh!
Kumekucha tena na Polisi wa Tz!
Hivi janga hili kubwa zaidi lililopo hapa Tz la hawa wanaoitwa Jeshi la Polisi Tanzania litaisha lini????Litaisha kwa njia gani??
Nini kifanyike ili kuondokana kabisa na janga hili ??????????????
 
Sasa kazi ya sheria ni nini?

Wanapaswa kuhukumiwa kwa sheria na si vinginevyo.

Ingekua ndugu zako je?
Ukiwapeleka mahakamani hao wanakaa jela kwa muda, mwenendo wa Kesi raia hawaendi kutowa ushahidi mahakamai na Mahakama haiwezi kumuhukumu mtu pasipo na ushahidi usio na Shaka ndio unakuta wanaachiwa wanaendelea kusumbuwa RAIA mtaani.

Sasa ukiona Polisi wanakamata na kuuwa huwa msipende kuwalaumu Polisi hayo ndio maamuzi Sahihi Kwa mtu aliyekataa kustaarabika.

Lakini tuweke akiba ya maneno mpaka tupate wasifu wa kweli wa hao vijana hapo mtaani au nje ya mtaa, maana kuna wengine Wana kazi zao kabisa kama cover lakini ni majambazi hatari na Polisi wanawajuwa vizuri, unapoona Polisi wanakamata na kuuwa elewa wanawajuwa vizuri hao watu.
 
Back
Top Bottom