Jiji la Dar ni kubwa sana na lina maeneo mengi sana yenye majina tofauti tofauti, Je! Nini kilipelekea mpaka haya maeneo yakapewa majina kama MABIBO, MBAGALA, TEMEKE, UBUNGO, ILALA, KARIAKOO, SINZA, MASAKI, KIGAMBONI, MSASANI, TAZARA, TABATA, TEGETA, BUNJU, MOROCO NK. Ni kwa nini haya maeneo yalipewa hayo majina, mwenye historia nzuri ya jiji hili atujuze.
Kulikuwa na mzee maarufu akiitwa Musa Hassan, sasa wamakonde walikuwa wanashindwa kumuita ipasavyo wakawa wanamuita NCHA CHANI, kwa hiyo ndo ikatokea hilo jina la MSASANI.
mkuu kweli ?
Musoma imetokana na lugha ya kijita "Omusoma " yaani sehemu ya aridhi iliyochongoka kuingia majini.
iringa imetoholewa na wajerumani kutoka neno lilinga manaake himaya/ngome
- makunduchi......kisiwasi zanzibar.
- kunduchi.........dar es salaam
- mchambawima.........kisiwani zanzibar
- kibanda maiti........kisiwani zanzibar
- boko.......dar es salaam
- kawe.........dar es salaam
- gongo la mboto........dar es salaam
- mbeya.........tanzania
- iringa...........tanzania
- sumbawanga.........tanzania
- kiboloroni.........kilimanjaro
- rombo............kilimanjaro
naomba kwanza nianze na hii michache tu na si vibaya na wewe ukaongeza na yako unayoijua ila nitafurahi kama nitajuzwa kwa hiyo michache niliyoitaja hapo juu.
siyo kwamba neno "musoma" limetokana na kwamba watu wengi wa mkoa wa mara (musoma) ni wasomi na wanapenda mno kusoma na wameelimika?
siyo kwamba neno "musoma" limetokana na kwamba watu wengi wa mkoa wa mara (musoma) ni wasomi na wanapenda mno kusoma na wameelimika?
Kama walivyoshindwa Simon Michael badala yake wakatamka Samora Macheli !