Kwi kwi kwi!!!! Wakati mwingine JF mnachekesha kweli kweli.
Wacha nijaribu kuweka facts ninazozijua:
Ni kweli Mwang'onda ni mtu wa Mbeya kwa jina. Nasema kwa jina kwasababu
Apson alikuwa na uhusiano mdogo sana na mkoa wa Mbeya. Yeye kwa jina kwa muda mrefu anajulikana kama Apson Cornel, alizaliwa Tabora kwa baba toka Kyela, Mbeya na mama Mnyamwezi.
Babake Apson alienda Tabora kwenye mashamba ya Tumbaku akiwa kijana na hakurudi tena Kyela. Hata alipofariki alizikwa huko huko Tabora.
Apson alifika Kyela kwa mara ya kwanza akiwa ni mtu mkubwa. Kyela alikuta ukoo wake wote umeisha na alimkuta shangazi yake tu na akamchukua na kumjengea Mbozi.
Ameanza kujihusisha na mambo ya Mbeya hasa baada ya kuwa mkubwa hapo usalama wa taifa, ndio akaanza kujichanganya zaidi na zaidi na watu wa kwao.
Yeye makazi yake sasa ni Mbozi ambako ana shamba kubwa la kahawa nafikiri na mahindi. Kyela ana nyumba tu na biashara na rafiki zake wakiwemo mkuu wa mkoa na wale vigogo wa zamani wa jeshi la polisi.
Sasa hapo ndipo usemi wa kwamba kajaza watu wa Mbeya, napata kigugumizi kuuamini.
Tukija kwenye urais 2010. Apson alifanya double act, huku alikuwa anonyesha anamuunga Malecela kumbe kichini chini anamuunga Muungwana. Hakuwa na uhusiano kabisa na Mwandosya na mpaka sasa yeye ni kundi moja na Mwakipesile, mkuu wa mkoa wa Mbeya. Ondoa kabisa wazo la Mwakyembe na Apson, hayo ni makundi mawili ambayo ni paka na panya. Kwa taarifa tu hata
biashaya ya akina Apson pale Kyela ambayo ni hotel ya maana inaitwa Kyela Resort, Mwakyembe yuko tayari kwenda kulala nje kuliko kulala pale.
Hapo kwa mara nyingine naona facts zako sio sahihi. Mkuu usitulishe sumu, wakati waungwana wa JF wanajua ni sumu.
Hata jina la Mwang'onda kaanza kulitumia sasa labda kama njia ya kumsaidia Thom ili akubalike pale Mbeya mjini.
Hizo appointments nyingi zinatoka wapi wakati yeye sio mkurugenzi tena?
Acheni kuendeleza mambo ya ukabila hata mahali ambapo hakuna facts zozote zinazoonyesha kuna ukabila.
Hayo ya Mwamunyange siku nyingine, ila huyo mkulu hata watu wa Mbeya wanamwogopa, haingiliki, sasa mbona unataka naye kumhusisha na ukabila?
Yaani mtu akiitwa Mwa... tayari ni mkabila?