Jamani APSON kafanya kufuru alipokuwa mkurugenzi wa Usalama ni tajiri kupita kiasi na bahati mbaya ameweka vijana wengi toka kabila la watu wa Mbeya kwenye usalama wa Taifa hii ni hatari sana kwa Taifa.
1. Mkuu Nungwi, kuna mengi uko sawa isipokuwa hili la ukabila, watu wa Mbeya huko ndani wako wengi siku nyingi sana, toka enzi za Mwalimu, hata Chief Bodyguard wake Mwangota, Daktari wake wa binafsi Mwakyusa, kina Simbeye, na wengine wengi wa nafasi za chini walikuwa ni kutoka mkoa huo, sababu ni kwamba wanaaminika sana kwa royality, Mkurugenzi mstaafu aliwakuta huko tayari, kumbuka huwa wanakuwa recruited toka wakiwa shule na sehemu mbali mbali za taifa, hawachukuliwi tu wakiwa watu wazima, kwenye hili uko mbali na ukweli, lakini mengi uliyosema uko karibu sana na ukweli.
2. Mkuu Mtanzania, strong analysis na as far as the main topic is concerned, kwa kweli inatisha sana mimi ninasema kwamba ukimkamata Mkapa, utakuwa umeua ufisadi completely kwa sababu huu ufisadi ambao ni extreme, umeanzia kwake, hawa wengine walikuwa wanachukua mgawo tu, ndio maana nimesema huko nyuma kuwa kama Chenge, ana hela zote alizonazo, na alikuwa Mwanasheria Mkuu tu, sasa vipi waliokuwa na mawaziri enzi zile na hawa kina mstaafu wa idara? Maana dataz zinaonyesha kuwa Chenge, alipata hela hizo akiwa sheria, chini ya Mkapa, kina Kigoda, wanaendesha magari ya Range Rover za dola elfu sabini je wamepata wapi hizo hela? Hivi kweli kipindi chote cha uwaziri wa Kigoda, alilipwa mshara wa kuweza kununua hilo gari analoendesha sasa?
3. Mstaafu wa idara ni kweli ana mali nyingi sana, alizo ilimbikiza kipindi cha Mkapa, na ni kweli kwenye ule uchaguzi alicheza a double play game, na alifanya vile only kum-please Mkapa, lakini in the process akaishia kujiweka sawa na muungwana na hata kumrishisha mkulu wa sasa, kwa sababu sio siri kuwa ni yeye single handed aliyeamua na according to the dataz ni kwamba alikuwa amemtayarisha kwa siri, lakini kwa muda mrefu sana bila watu wa huko ndani kujua, maana namjua mkulu mmoja aliyedhani kuwa yuko karibu naye na kwamba atamrithisha, time ilipofika aka-wa-suprise mpaka ma-senior huko ndani, you wonder in all this ni kwa ajili ya interest ya wananchi au ya nani?
Wa-Tanzania, ni lazima tuendelee kupiga kelele kwa sababu tunajua kuwa tumetoka mbali sana politically, binafsi napenda kutoa heshima kwa serikali ya sasa kwa kutoa nafasi kwa wananchi kutoa maoni yetu kuhusiana na kila sekta ya serikali yetu, bila vipingamizi never before wa-Tanzania tumekuwa na hii nafasi ya uwazi bila kunyanyaswa, ingawa bado hii tabia haijawaingia vizuri huko serikalini na watawala wetu kwa ujumla, lakini ninaaamini kwamba mijadala kama hii na ya ufisadi wa kina Chenge, ni changamoto nzito sana kwetu wananchi kuwashupalia viongozi wetu wasiotaka kuwa kama sisi wananchi, yaaani wawazi na ninarudia kwamba ili kumaliza mzizi wa fitina na ishu ya uifisadi, ni lazima in one way or another Mkapa, ahusishwe na uchunguzi wa kina otherwsie tutakuwa tunacheza na mikia tu, huku kichwa kinaendelea kutuumiza!
Ahsante Wakuu!