Apson: The Beginning of TISS's Failure

Hapo Bwana Nungwi umepotosha na mawazo yako ya Apson kum support Mwandosya. Fanya home work uone huyo jamaa yuko upande gani?Chunguza pia uraia wake halisi
 
Mwanakijiji,

..nafikiri Watanzania wengi wanaamini kwamba kila mtumishi wa umma mwenye mali nyingi basi amezipata kwa njia za kifisadi.

..kuna umuhimu wa kuchunguza watumishi wa umma wa ngazi za juu, na wanasiasa, wanapata mshahara na mafao kiasi gani. nakuomba sana utumie sources zako kutupatia takwimu hizo.

..kwenye nchi za wenzetu utumishi wa umma ni kazi ya wito. hapa kwetu utumishi wa umma ni kwa wale wanaotaka utajiri.
 
tofauti yetu ni kwamba, wewe unaangalia 'here and now.' mie naangalia historical background ya system nzima!!!
kama ni medical assessment, wewe unafanya focus v/s head to toe kwa upande wangu!! hii ndio tafauti kubwa kati yetu......approach, approach and approach.

Na wewe tangu umesomea huo unesi wako huachi kutolea mifano yako ya kimedical....kafunge vidonda huko....Lol
 
DC na Northern Virginia hakufai kabisa....
Siku hizi pale St Peters wamekata kata miti ata jengo lenyewe linaonekana na kale kabarabara wamekawekea lami unakatiza tuu mbele ya jengo hawana noma sana sema ukisogelea geti ndio unaweza kuwekwa chini ya ulinzi kwa muda.

Anwyays ofisi ya station iko chini ya kitengo cha usalama wa ndani, walikuwa wanakaribisha wananchi wote kwenda pale kutoa mawazo yao..siku hizi wameihamishia kule sea view.

Nikatoe mawazo yangu Usalama wa taifa?
Kwangu haitatokea hata siku moja.
 
FMES,

Umenikumbusha ya brother Mwangota RIP, Looh, jamaa alikuwa akiingia, wote mnatawanyika haraka sana, mnajua hapo hakuna amani tena.

Siku nimemkuta Muhimbili kule juu, yuko taabani, utafikiri sio yeye.

Hii dunia, tutende mema maana wote ni wasafiri tu na hakuna mjanja kwenye kifo.


Fedha na Mamlaka ndiyo hirizi ya nguvu zao hawa jamaa.
Wakibanwa na kuumbuliwa asili ya utajiri na nguvu zao za kupindisha taratibu, mtawaona wakinyong'onyea na kuteketea kama manyoya ya kuku mbele ya moto.
 
Watanzania tuu wajinga sana mpaka mara nyingine tunasikitisha.

Nenda dunia yote utakuta vyombo vikuu vya masuala vya Ulinzi vinashibishwa ipaswavyo ili vifanye kazi zake vizuri kulinda nchi na maslahi yake.

Sisi tulipoamua kutumia "vijisenti" vyetu kushibisha Jeshi, Polisi, Magereza, Mgambo na Usalama wa Taifa ili nyie kina jinalakonilangu mlale salama salimini( pamoja na machozi ya kunyang'anywa mashamba na nyumba wakati wa Azimio) kila siku bila hofu ya mapinduzi au umwagaji damu ilikuwa ni dhambi?

Angalia tawala zote za dunia maana wengine wenu mnajidai ni mabingwa wa Historia. Anzia enzi za Waisraeli wakiwa kwa Farao, angalia enzi za Farao, njoo wakati wa Mfalme Daudi, Solomon, Nebukadineza, njoo Pilato, Herode, hata Caligula, Caliph wa Oman, Ottoman, Artatuk, Genghis Khan, Musolini, Mfalme Fahd, Ayatolla, Papa Mtakatifu na Kikwete, wote majeshi ya ulinzi na usalama hupewa kipaumbele na wametumia mbinu mbali mbali kuhakikisha kuwa wanalinda nchi na kufuata maelekezo ya viongozi wao hata kama walikuwa na maoni tofauti.

Jeshi pamoja na kuwa ni chombo cha kulinda Taifa, lakini kinatumika kwa kufuata mwongozo wa Serikali.

Sikatai kuna majemedari wabaya na waovu, na hao ni jukumu la Serikali na mkuu wa Serikali kuwachukulia hatua. Lakini ikiwa wanafanya kazi zao kufuata maelekezo ya Serikali na hali halisi ya upepo wa kisiasa katika nchi na jamii, basi ile dhamana ya maamuzi tuliyompa Mkuu wa Serikali inaangukia kwake.

TUnachomtaka Kikwete afanye sasa hivi ni kuhakikisha kuwa Uhujumu na Udhalimu hauendelei kwa kutumia migongo ya dola na majeshi yake!

Mliopoteza Kondoo na Sungura kwa ajili ya siasa za kuleta usawa wa mali, zilizotumia vitisho kwa mwenye kuleta kokoro, mshukuru Mungu Serikali ilitaifisha na si Wananchi waliwavalia njuga na kuwapga mawe.

Wote tumefika hapa kujiamini na kulia au kusifu kutokana na juhudi za kuunda Taifa letu. Kuunda na kujenga Taifa si kazi nyepesi. Ina majaribu mengi, vigingi, na si kazi ya mzaha. Tumshukuru Mungu kuwa tulipo hapa leo ambapo tunachapana makondo ya kifalsafa ni kutokana nakukubali kwa wazazi wetu kufuata utii kwa Serikali.

Sisi tuna nafasi ya kuchangua yaliyopita kwa kuchuja yasiyofaa, kuboresha yenye mianya mibovu kwa maana sisi ndio tunaounda na kuanza kuongoza Taifa kwa miaka mingine 40. Katika kipindi hicho, watoto na wajukuu wetu wataangalia sisi tulifanya nini, watachambuana na kujengana na kuendeleza libeneke la kujenga Taifa letu mpaka siku ya mwisho.

Hivyo basi, leteni hoja na ushahidi na si kulalama tuu na kunyoosha vidole. Especially wewe Yournameismine. Ni mlalamikaji mwepesi tuu, lakini ukiulizwa leta hoja unakimbilia kebehi.

Tupe mifano halisi unayofahau na kama kuna iliyokusibu, basi useme, si wote tulikuwa upande wako wakati wa Azimio, wengine tulinufaika ati zile nyumba zenu zilipogawiwa kwa wananchi!
 
Fedha na Mamlaka ndiyo hirizi ya nguvu zao hawa jamaa.
Wakibanwa na kuumbuliwa asili ya utajiri na nguvu zao za kupindisha taratibu, mtawaona wakinyong'onyea na kuteketea kama manyoya ya kuku mbele ya moto.

Madela,

Amani, Utulivu na Mshikamano ulipatikana kwa kafara chafu. I will be the first one to dare and openly criticize all the awamus for turning a blind eye kwenye uchafu uliofanywa na Jeshi, Polisi na Usalama wa Taifa.

Badala ya vyombo hivi kufuata mkondo wa kawaida kama Raia wengine, wao walitumia njia fupi na chafu kujineemesha na kutuliza zali katika vikosi, huku sisi wananchi tukipigwa marungu tukilalamika juu ya bei ya Sembe.

Serikali zote 4 kwa hofu ya machafuko na kukosekana ulinzi zilitumia "busara" mbovu na kuhodhi tabia hizi chafu. Imekuwa ni mambo ya kufa kufaana!

Serikali badala ya kugeuza nguvu zake katika uzalishaji mali mkubwa ili pato la Taifa liongzeke na hivyo kuongeza mgawanyo wa mapato kukidhi adha na ukali wa maisha, ulibuni njia batili kufumbia macho maovu ya vikosi vya jeshi.

Pesa nyingi zimepotea Ulinzi, Polisi na Usalama wa Taifa, na Serikali kuu ikatumia kifua chake kufuta mapengo haya ya fedha zilizopotea (bad debts)!

Sasa hivi tuko kwenye nyakati tofauti, uwezo wa kujiimarisha kiuchumi tunao na hivyo kuondokana na utegemezi. Tatizo linabakia ile tabia ya kujipatia kwa haraka imeshamiri na kuwa chronic au terminal. Inabidi shoka la nguvu litumike ku-amputate tabia hizo maaana chemotherapy haifanyi kazi!
 
Ufiasdi unaozidi kipimo huko idara, unaanzia kwa Kombe ambaye alikomba hela zote ikafikia walinzi wa viongozi kusafiri nao bila posho, according to the dataz ndio hasa chanzo cha kifo chake, nasikia kuna wakati aliwahi kukutwa na dola lakini moja na nusu huko London na zile hela zikarudishwa bongo, lakini akaenda tena safari nyingine akiwa na hela zaidi ya zile za kwanza Waingereza again wakazirudisha zile hela kwa serikali, na haikuchukua muda, mkulu akafa,

Waliokuwepo huko kabla ya kombe, hawakuwa kabisa na utajiri wa kutisha, mmoja wapo ni Mzena, hakutoka na ktiu huko kabisa, isiapokuwa kuna walioktoka na mali nyingi sana wakati wa Mwalimu, kama Liani, Mgaya, Aziz kule polisi, hawa walifanya kufuru kama Mahita, alivyofanya!
 
Ufiasdi unaozidi kipimo huko idara, unaanzia kwa Kombe ambaye alikomba hela zote ikafikia walinzi wa viongozi kusafiri nao bila posho, according to the dataz ndio hasa chanzo cha kifo chake, nasikia kuna wakati aliwahi kukutwa na dola lakini moja na nusu huko London na zile hela zikarudishwa bongo, lakini akaenda tena safari nyingine akiwa na hela zaidi ya zile za kwanza Waingereza again wakazirudisha zile hela kwa serikali, na haikuchukua muda, mkulu akafa,

Waliokuwepo huko kabla ya kombe, hawakuwa kabisa na utajiri wa kutisha, mmoja wapo ni Mzena, hakutoka na ktiu huko kabisa, isiapokuwa kuna walioktoka na mali nyingi sana wakati wa Mwalimu, kama Liani, Mgaya, Aziz kule polisi, hawa walifanya kufuru kama Mahita, alivyofanya!

Wajua ni kwa nini Kombe akiwa Mukulu aliibiwa gari pale migomigo?
 
Basi tuseme tuna tatizo kubwa zaidi kuliko tunavyofikiria. Naomba msikose makala yangu maalum inayotokana na mjadala huu itakayotoka kwenye gazeti la "kulikoni" kesho.
 
Ufiasdi unaozidi kipimo huko idara, unaanzia kwa Kombe ambaye alikomba hela zote ikafikia walinzi wa viongozi kusafiri nao bila posho, according to the dataz ndio hasa chanzo cha kifo chake, nasikia kuna wakati aliwahi kukutwa na dola lakini moja na nusu huko London na zile hela zikarudishwa bongo, lakini akaenda tena safari nyingine akiwa na hela zaidi ya zile za kwanza Waingereza again wakazirudisha zile hela kwa serikali, na haikuchukua muda, mkulu akafa,

Waliokuwepo huko kabla ya kombe, hawakuwa kabisa na utajiri wa kutisha, mmoja wapo ni Mzena, hakutoka na ktiu huko kabisa, isiapokuwa kuna walioktoka na mali nyingi sana wakati wa Mwalimu, kama Liani, Mgaya, Aziz kule polisi, hawa walifanya kufuru kama Mahita, alivyofanya!

Mkuu umeyasema yote...ila kifo cha Kombe nacho kina utata sana wengine wanadai aliondolewa na makachero wa Kagame wakishirikiana na wa TISS maana alijua mpango mzima wa kutungua ndege ya Habyarimana na alimwambia Habyarimana pale airport kuhusu hiyo plot....wengine wanadai alikuwa analeak siri kwa Mrema.
Lakini kwa kifupi mkulu alichuma sana TISS nina uhakika amechangia sana kuanguka kwa miradi mingi ya TISS.

Was it necessary kupitisha TISS act ya 1996? maana hapo ndiko majibu mengi yako.
 
Icadon, kuna sheria kadhaa ambazo zimekuja 1996, na zimekuja baada ya Mkapa kuingia madarakani.
 
TISS walihusika na kifo cha Kombe

Ili iweje?

Na Sokoine ni Nyerere alimuua? Ooh! hili nalo linanisumbua: Nani kamuua Ditopile?

Na maadam upo hapa, ngoja niulize na lingine linalo tutatiza wengi: Ni Suge Knight alimuua Tupac?
 
kweli hili swali umelifikiria au umeuliza tu alimradi uulize? Nikupe mifano ya wageni waliokuja na kuingia hadi chumbani na kuondoka na vito vyetu vya thamani huku walinzi wakiwa nje wanacheza bao?

Naongelea aina za wageni uliosema walizuiwa enzi zile, kama makaburu, wageni tunaoweza kusema wa kisiasa, wanaohusika na usamala wa nchi, usalama usio husiana na wizi wa hela.

Usitake kupindisha mambo hapa.

Enzi za nyuma pembe za ndovu zilikuwa hazitoki? Hata hizo pesa, zilikuwa hazitoki? Unamkumbuka Sara Martin Simbaulanga alivyo tusua vijisenti BOT?

Haya mimi nimekupa mifano. Wewe unasema 'Nikupe mifano? Kwa nini unapenda kuficha ficha vitu Mwnkjj? Unakuwa kama gazeti la 'THIS DAY' wanaosema 'jina tunalihifadhi, alikuwa Waziri wa Mkapa.' Kama husemi basi usichombeze nusu nusu! Mwnkjj, sikudangaji ndugu lakini napata shida sana ku dili na namna yako ya midahalo. Labda mi ndio wrong bwana. Poa.
 
kuhani,
wala haupo wrong jamaa ni character ya namna yake, which is a good thing!!! ana claim sana, akishakuwa na perception flani juu ya suala husika basi haachi room wala hataki kusikia/kuelewa mawazo mbadala au chalenji toka kwa wengine!!! kupunguza maneno ni kwamba jamaa ni mbishi kama role model wake(yule babu marehemu, RIP)........

Sidhani kama ni 'good thing' kwa sababu 'ana claim.' Hata Kibweterere wa Uganda aliyejichoma moto na waumini wake alikuwa ana claim. Adolf Hilter pia alikuwa ana claim ndani ya Nazi Germany.

Hata yule babu nae alikuwa ana claim, lakini ningekuwa karibu na nae enzi zile angenifunga kwa sababu nisingekubali vyote anavyosema kwa sababu ana claim. Huyu mtu wetu hapa analijua hili sana, lakini anaendelea kuwa hivyo kwa sabau ana claim!
 
Back
Top Bottom