Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,693
- 40,700
Tunapozungumzia idara ya Usalama wa Taifa na jinsi imeiangusha serikali yetu na kuweka usalama wa taifa letu hatarini nafasi ya Bw. Apson Mwang'onda haiwezi kupuuzwa. Baadhi ya matukio yaliyotokea na kuruhusu ufisadi nchini yalitokea wakati wa "ulinzi" wake na hatujui ni kwa kiasi gani alisimamia idara hiyo katika Usalama wa Taifa.
Wakati umefika na huyu naye ajibu, alifanya nini kuiimarisha idara hiyo na kuhakikisha inajijenga sawasawa kukabiri matishio ya ulimwengu wa utanda wazi?
Kwa vile Rada ilinunuliwa wakati wa uongozi wake wananchi wana haki ya kujua ni kwa kiasi gani idara yake ilishiriki katika kuhalalisha mauzo ya kurushwa kwa Vithlani? Zaidi ya yote binafsi ningependa kujua mambo yafuatayo kuhusu idara ya TISS enzi za Apson:
a. Walijua nini kuhusu Saileth Vithlani yule Dalali aliyetoweka kwa kupanda ndege baada ya kuwaaga?
b. Idara ya Usalama wa Taifa ilijua nini kuhusu Jeetu Patel na uanzishaji wa banki ya Azania wakati Bw. Patel alishawahi kufilisi moja ya makampuni yake na sheria ya Fedha ilikuwa hairuhusu mtu aliyefilisiwa kuingia katika sekta ya Fedha? Kwanini Patel alipewa exception?
c. Apson alijua nini kuhusu kitendo cha Rais Mkapa na Waziri wake wa Nishati kutumia vyeo vyao kujinufaisha na kujigawia mgodi wa Kiwira?
Je yawezekana matatizo yetu mengi ya kiusalama yametokana na uongozi wa ndugu huyu na wakati wake wa kujibu umefika ili kina RO wajifunze kutokana na makosa?