Apson: The Beginning of TISS's Failure

Ufisadi ni kosa gani la kisheria?
Theft? Embezzlement?

...add failure to declare assets in contravention of the Public Ethics Act, and as well as engaging in conduct manifesting blatant Conflict on Interest, as when the President and the Minister of Energy enter bid to buy coal mines, where two members of the board who are evaluating the bids are also buying partners of the President, and the head of Privatisation Commission, President's appointee who went to school with him at Pugu Sekondari, approves a dirt cheap sweet deal, of which only 10% is paid off!
 
Tume ya maadili haina chochote. Kiundwe chombo ambacho kinaweza kudili na hawa watu. Ni afadhali hata ya huo ufisadi kuliko acts of espionage. Mtu aweza kuiuza nchi na hao watu tunao hata kwenye hiyo system na kuwatoa ni kazi. Espionage ndio mzizi mkuu wa ufisadi wewe utajiuliza swali iweje siri za nchi au hata rasilimali za nchi ambazo hata wewe raia huna taarifa nazo unaambiwa na watu Tel Aviv, Washington ,London au Paris Club.
 
Aisee!!,Hii tungo kiboko bwana.naelekea kufikiri kama wakapewa TMK,Wanaume Family,basi hiyo single itauza sana.....
TE TE TE TE TE TE SINGLE YANGU NAWEZA UZA BILBORD EHEE,MSHIKAJI SI NDUGU YANGU WALA NIKIMWONA SIMJUI,BALI SIKU MOJA NILINGIA VICTIRIA NIKAONA KAZI NZURI,KWA HIYO NACHANGIA NACHOJUA SIFUATI UPEPO PALI NASOMA MAPYA NA KUYAPIMA
 
TE TE TE TE TE TE SINGLE YANGU NAWEZA UZA BILBORD EHEE,MSHIKAJI SI NDUGU YANGU WALA NIKIMWONA SIMJUI,BALI SIKU MOJA NILINGIA VICTIRIA NIKAONA KAZI NZURI,KWA HIYO NACHANGIA NACHOJUA SIFUATI UPEPO PALI NASOMA MAPYA NA KUYAPIMA

Mafanikio yanapimwa kwa majengo?
I give up!!!!
 
swali langu lilisema "ufisadi ni kosa gani la kisheria".... ?
Wizi wa mali ya uma

...ambao hauko wa aina moja. Na kama ufisadi ulivyo wa aina nyingi, pia hakuna sheria moja, bali zipo nyingi zinazokataza vitendo anuwai ya ufisadi.

Na baadhi ya sheria zinazo elezea na kukataza ufisadi ni:

-Prevention of Corruption Act, of 1971 -Ufisadi wa Rushwa unakatazwa hapa
-Public Leadership Ethics Act, 1995 -Ufisadi wa kukiuka misingi ya maadili
-Penal Code of 1980 - Ufisadi wa 'abuse of office" na wizi kwa Ujumla
-Anti-money laundry Act, 2006 - ufisadi wa kuficha na kusafisha hela chafu
-Public Procurement Act, 2004 - ufisadi kwenye mikataba unakatazwa hapa
-Income Tax Act, 2004 - Ukwepaji Kodi
-Foreign Exchange Act, 1992 - Ufisadi wa Kuficha hela nje unakatazwa

-na kuendelea na kuendelea...
 
...kinyume na sheria mbalimbali kama nilivyo ziorodhesha hapo juu.

(naona uliacha kipande cha jibu langu.)

I got you..

umesema ni kujineemesha kwa kujipatia mali ya umma kinyume cha hizo sheria..

so ufisadi kwako ni lazima ihusishe kujipatia mali ya umma kinyume cha sheria? Au yawezekana kuna vitendo vingine vya kifisadi ambavyo havihusiani na kujipatia mali ya umma?
 
so ufisadi kwako ni lazima ihusishe kujipatia mali ya umma kinyume cha sheria? Au yawezekana kuna vitendo vingine vya kifisadi ambavyo havihusiani na kujipatia mali ya umma?

kujineemesha, sio tu kujipatia, mali ya umma.

Ninaposema kujineemesha nina maana kunufaika. Now, bear in mind, Benjamin akimsaidia mkewe, Anna, kumiliki mtambo wa kutengeneza Umeme kinyume cha sheria, basi Benjamin nae amenufaika, na anaingia katika definition yangu ya ufisadi.

Nina maana yangu ya kutaka usahihi wa hivi vitu kabla hatujaenda mbali.
 
kujineemesha, sio tu kujipatia, mali ya umma.

Ninaposema kujineemesha nina maana kunufaika.


Let us rewind:

Kujineemesha kwa kujipatia mali ya umma kinyume na sheria mbalimbali kama nilivyo ziorodhesha hapo juu.

Kwa hiyo kauli yako ya kufafanua "kujineemesha" ina modify hiyo hapo juu; maana mwanzoni ulielezea kujineemesha "kwa kujipatia"... Je mtu asipojineemesha (yeye au mwingine) kwa kutumia mali ya umma lakini akavunja sheria mbali mbali ambazo zimepoteza mabilioni ya shilingi au mali (lakini yeye mwenyewe hakufaidika wala watu wake wa karibu) huyo na anaweza kuwa kwenye ufisadi, au ni lazima kuwa na kunufaika kwa namna fulani kwa mhusika?



Now, bear in mind, Benjamin akimsaidia mkewe, Anna, kumiliki mtambo wa kutengeneza Umeme kinyume cha sheria, basi Benjamin nae amenufaika, na anaingia katika definition yangu ya ufisadi.

Kwa hiyo katika definition yako hii ni lazime mtu "anufaike" ndipo kuwe na ufisadi. Hivyo kama Lowassa alivyofanya na hakuna ushahidi wa yeye kunufaika na Richmond ni haki kuita uzembe wake na kutokuwajibika kwake kuwa ni sehemu ya ufisadi?


Nina maana yangu ya kutaka usahihi wa hivi vitu kabla hatujaenda mbali.

Tuko pamoja ndio maana nataka tuwe crystal clear tunazungumzia kitu kile kile.
 
Kwa hiyo katika definition yako hii ni lazime mtu "anufaike" ndipo kuwe na ufisadi. Hivyo kama Lowassa alivyofanya na hakuna ushahidi wa yeye kunufaika na Richmond ni haki kuita uzembe wake na kutokuwajibika kwake kuwa ni sehemu ya ufisadi?

Tukisema kwamba hakuna ushahidi Lowassa alinufaika, lakini twajua alihusika katika vitendo vilivyo sababishia Taifa hasara ya mabilioni, sheria za ufisadi zitataka kujua, je, huko kutokuwajibika kulikuwa na nia ya kunufaika?

Benjamin na Anna wakigundua kwamba "soo" linataka kuibuka, halafu, haraka haraka, wakauza hisa zao za mtambo wa kuzalisha umeme kabla haujaanza kuzalisha umeme, kesi ya Ufisadi itawakuta kama tuking'amua kwamba Benjamin na Anna walikuwa na nia, au walikula njama, au walificha ushahidi wa jinai, wa kutaka kujineemesha na mali na umma visivyo halali, japo hawakuwahi kufanikiwa kunufaika.

Kwa hiyo, kisheria, Ufisadi unajumuisha nia na njama ya kufanya ufisadi.
 
Kwa maneno mengine ufisadi si lazima mtu mwenyewe anufaike..

ukisema kwamba hakuna ushahidi Lowassa alinufaika, lakini twajua alihusika katika vitendo vilivyo sababishia Taifa hasara ya mabilioni

Je vitendo vilivyosababishia nchi hasara ya mabilioni hata kama mtu hajanufaika yeye mwenyewe tunaweza kuviita ni vya kifisadi?
 
Je vitendo vilivyosababishia nchi hasara ya mabilioni hata kama mtu hajanufaika yeye mwenyewe tunaweza kuviita ni vya kifisadi?

Mahakama inaweza kusema "hapana."

Kama hakunufaika na alikuwa hana nia ya kunufaika au kuwanufaisha ndugu, jamaa na rafiki zake, basi hayo ni makosa mengine ya kiutendaji kazi, ambayo yanaweza yasiitwe ufisadi.

Lakini hii haisemi lolote kuhusu uzito au wepesi wa hayo makosa mengine ambayo siyo ufisadi. Nayo yanaweza kuwa ni makosa mabaya kama ufisadi, japo hayaitwi ufisadi.

Katika mifumo ya Common Law, mtu ambae ameua, kwa mfano, bila kuwa na nia ya kuua, anaweza kupotelea jela, kama ikigundulika kwamba kitendo chake ni cha kizembe na kilionyesha kutokujali thamani ya maisha ya mtu (recklessness plus extreme indifference to the value of human life (P + EIVHL). Kwa hiyo, japo kosa halita itwa Murder, hiyo haita maanisha kwamba hilo kosa lingine ni jepesi (Manslaughter/Involuntary Homicide... n.k.)

Na hapa pia, kama Lowassa kasababishia taifa hasara ya mabilioni bila kuwa na nia ya kunufaika au kuwanufaisha ndugu, jamaa na marafiki, basi hajatenda ufisadi, isipokuwa makosa mengine ya kiutendaji ambayo yanaweza kukaribia, au kuwa mabaya kama, ufisadi mbele ya sheria.
 
Kuhani
Nadhani unataka kutoka nje ya mstari.
Ufisadi si kunufaika tuu kama unavyonadi na kudhani. Ufisadi ni pamoja na kuuwekea mbolea na kuukuza kisha wakala wengine.
Kama ilivyo rusha au uozo mwingine au hata criminal offence ambapo kushindwa kuzuia kosa ni kosa hata kama hukutenda hilo kosa ila ulikuwa na uwezo wa kulizuia....
 
Back
Top Bottom