JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,309
- 5,464
Imeelezwa vituo vyote Binafsi vya Afya vitasitisha kutoa huduma kwa Wagonjwa wapya wanaotumia Kadi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)kuanzia Usiku wa Saa Sita kuamkia Machi 1, 2024 huku wale ambao watakuwa katika Uangalizi Maalum (ICU) wakiongezewa muda wa Saa 48 kuendelea kupata huduma.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Vyama vya Watoa Huduma Binafsi za Afya Tanzania (#APHFTA), Dkt. Egina Makwabe ambaye amesisitiza maamuzi hayo yameafikiwa katika kikao chao Bodi ya APHFTA kilichofanyika Februari 29, 2024.
Amesema “Watakaohitaji huduma watalazimika kulipa fedha Taslim kuongezea pale ambapo gharama za kadi zao za bima zinapoishia, wale wa ICU baada ya muda huo tutafanya mchakato wa kuwahamishia Hospitali za Serikali.”
Uamuzi huo umefikiwa baada ya NHIF kufanya maboresho ya Kitita cha Mafao kwa Wanachama wake na kutangaza utekelezaji wake utaanza rasmi Machi Mosi.
Pia soma - Wenye Hospitali binafsi wakataa kuwahudumia wateja wa NHIF kutokana na vifurushi vipya
News Alert: - Hatimaye APHFTA na Hospitali Binafsi zote Warejesha huduma Hospitalini