Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,939
- 20,400
Katibu Mwenezi, Itikadi na sisa wa CCM Paul Makonda, yupo barabarani akizungukia maeneo mbalimbali ya nchi ambako amekutana na shida lukuki.
Kuna shida zingine ni rahisi sana kutatuliwa bila kutumia nguvu wala migogoro.
Shida zingine wananchi hukutana nazo kutoka kwenye idara za serikali ambazo haziko tayari kuwasaidia wananchi khasa kwenye masuala ya ardhi.
Tulikuwa na waziri Lukuvi wizara ya ardhi akaondolewa na kapelekwa Ridhiwani Kikwete ambae yajulikana alikwenda kwa kazi gani pale.
Lakini akaletwa kijana waziri Slaa ambae kasi yake ya kutatua matatizo ya ardhi imekuwa ndogo.
Lakini Paul Makonda tangu achukue nafasi ya ukatibu mwenezi, kumeibuka madudu lukuki yanofanywa na waajiriwa wa wizara ya ardhi khasa pale wanapohusihwa na vitendo viovu vya dhulma kwa wananchi.
Na matatizo hayo asilimia tisini ni yaleyale ambayo wananchi haohao walikuwa wakipiga simu katika kutuo cha Runinga cha Shule Ya Uongozi katika dawati la aliekuwa katibu mwenezi Humphrey Polepole ambapo matatizo yalikuwa yakipokewa na kuahidiwa kutatuliwa ama papo kwa hapo au kesho yake.
Serikali ya jamhuri ya wapigaji haikupenda jambo lile na bwana Humphrey Polepole akazuiwa kuendelea na kipindi chake na akapewa ubalozi akae mbali kule.
Sasa, CCM na serikali yake yashangaza sana sisi wengine ambao mshangao wetu ni kuona kuwa masuala yaleyale ambayo yalikuwa yakiletwa kupitia ile shule ya uongozi yangeweza kutatuliwa bila kutumia gharama kubwa badala ya gharama za sasa ambazo zahusu matumizi ya mafuta kwenye magari, kulipana posho na pia wananchi wa jamhuri ya wapigaji wakihakikisha waneemeka na ziara hizi za Paul Makonda.
Hivi ni lini CCM itaketi kikao kuhakiki matendo yake kwa Watanzania?