Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Thubutu! Upate taifa la viwanda chini ya utawala wa CCM? Kila uchao ni kukurupuka tu. Hakuna kinachoeleweka.
Tusijidanganye wadau TZ hakuna chama chenye uwezo wa kuendesha nchi vizuri kuliko ccm, muhimu ni kushauri tu lakini sioni chama chenye uthubutu zaidi ya ccm.
 
Huu ni uongo mkubwa . Sisi wakazi wenyewe wa Morogoro hatuoni hilo. Barabara zinatengenezwa kwa usawa.
Zimechongwa Mji mzima bila kujali Diwani ni Chama gani.
Hata hivyo barabara hazitengenezwi na Halmashauri ambayo inaundwa na Madiwani Bali zinasimamiwa na TARURA , Chombo huru cha Serikali.
 
Hii thread ni ya siku nyingi ila kila napoisoma naona uhalisia wenyewe ulikuwa kama mtabiri. Sasa tumefika miaka mitano mawazo yako yametofautiana na yale ya mwanzo mtoa mada.
 
Hali ya biashara nchini ni mbaya sana.

Acha biashara kubwa ambazo nyingi zimefungwa, chukua biashara ndogo tu za mfano Bar au glocery. Utapata wateja siku 1 au 2 baada ya hapo huwaoni tena! Hata siku hizi 1 au 2 hawanunui cha maana zaidi ya kuangalia mazingira, glass mpya, na wahudumu. Kesho yake huwaoni. Hawana fedha.

Utakaowaona ni TRA. Nao mkimalizana kwa rushwa hawaji tena huku masikini wewe mwenye grocery hata mtaji wa kununua vinywaji umewapa TRA. Hivyo utalazimika kufunga biashara yako mwezi wa kwanza tu.

Kwa mtindo huu tutajikwamuaje kimaisha huku mishahara kwa walioajiriwa serikalini haijaongezwa huu mwaka wa 5?

Jamani tunateseka mtaani.
 
Pole sana.. Jaribu na kwenye kilimo.. Jembe halimtupi mkulima.. Tatizo kwa sasa bar zimekuwa nyingi sana.. Enzi zetu tunakaa Singida, ilikuwa ni Singida Motel au Stanley motel ndio maeneo ya kujidai.. Zaidi zaidi, Peoples club!
 
Tatizo wa TZ hata hatujui tunataka nini.
Maana ukiangalia..
1. Ajira hakuna
2. Ongezeko la mishahara hakuna
3.Ukisema ukakiajiri hupewi NSSF yako.
4. Biashara huku mtaani zinakufa kisa wateja hakuna na TRa wanakadiria kodi sio rafiki.
5. Bodi ya mikopo wanapandisha liasi cha kulipa kila uchwao

Hivi vyote kwa wenye akili ilipaswa ndio yawe maswali yetu wanapopita kuomba kura.
 
Uhalisia kiuchumi inaonekana Tanzania ina miradi mingi sana mikubwa iliyochini ya Serikali moja kwa moja. Kinyume na tunavyoaminishwa, miradi hii yote mikubwa ni fedha za mikopo. Duniani kote, mwelekeo wa uwekezakaji ni ama PRIVATE SECTOR au PUBLIC_ PRIVATE SECTOR (PPT).

Serikali ama ibaki kukusanya Kodi na kusimamia utoaji wa public good Kama ulinzi na Usalama au ijiingize kwenye uzalishaji Kama shareholder na si mzalishaji pekee. Kwa miaka 5 iliyopita, Serikali imekopa fedha nyingi mno kuwa mzalishaji pekee wa miradi mikubwa. Sasa Serikali hii inaomba ridhaa kubaki madarakani ili ikamilishe miradi hii.

Bila Shaka mikopo mikubwa itaendelea. Tatizo kubwa ni baada ya hiyo miaka 5 ijayo. Miradi hii yote itaanguka kwa kukosa usimamizi na uwizi mkubwa serikalini kama ilivyokuwa enzi za ujamaa. Cha umma hakina uchungu.

Sasa je, mikopo hii italipwajwe?
 
Ni lazima Watanzania wamkane shetani na nguvu zake zote, ushawishi wake wote na maovu yake yote. Hapo ndipo ndoto zao za matumaini zitafufuka tena. Ni lazima wapiga kura wafanye uamuzi sahihi ktk sanduku la kura ifikapo tarehe 28-10-2020.

Kwa maana jamaa anaonyesha wazi kabisa, kama akipata tena fursa kwa kuongoza tena kwa awamu ya pili bado anatamani kununua madege, meli na kuwekeza zaidi ktk miradi mikubwa huku maendeleo ya watu hayapo akilini mwake. Hakika vijana, wazazi wenu waliopo ktk ajira za utumishi wa umma, na babu na bibi zenu wastaafu ni makundi yasiyogusa vipaumbele vyake kabisa.

Ni lazima wananchi wachague kile kilichokuwa bora kwao. Hii ni kwa ajili ya mustakabali wa Tanzania iliyokuwa bora kwao.
 
Pole sana.. Jaribu na kwenye kilimo.. Jembe halimtupi mkulima.. Tatizo kwa sasa bar zimekuwa nyingi sana.. Enzi zetu tunakaa Singida, ilikuwa ni Singida Motel au Stanley motel ndio maeneo ya kujidai.. Zaidi zaidi, Peoples club!
Kyela mavuno ya mpunga mwaka huu ni makubwa mno lakini hakuna wateja kabisa baada ya wateja wakubwa kufilisika
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom