Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Hivyo ni masuala ya kutoa dukuduku hivyo ni mambo binafsi, ni kama leo JK afe halafu Dr Ulimboka atoa dukuduku lake.
Kifo hakina dhamana hujui nani atatangulia, ikiwa Dr. Ulimboko anataka kutoa dukuduku lake afanye tu kwa nini amsubire mpaka mkwere afe?
Na Mwere sidhani kama ata-mind ikiwa yatakyosemwa ni kweli.
Suala la kukosoa au kumsema vibaya Mheshimwa Magufuli ni suala binafsi kwa wale waliyoathirika katika utawala wake ninajua kuna wengi tu wanamsifia na kumzungumzia vizuri raisi wetu aliyepita na huu ndiyo msimamo wa kitaifa, hivyo basi wacheni wale wanaotoa dukuduku zao wafanye hivyo. Tumeona hata baadhi ya watu wanamsema MUNGU vibaya itakuwa binaadamu wenzetu.
Jaribu kujiweka huru kama jina lako ulilolichagua. Kwenye siasa usimuamini yoyote kwa lolote.
 
Sasa mbona unaongea kitu kama unajua wakati majibu hauna viswali vya darasa la nne hivi museven alikua Rais toka mwaka 86 huyu PK ni juzi tuu mwaka 2000 yaani huyo mzee alikuwepo kwenye vita ya rebbelion ya Iddi Amin na Obote na PK ni Rais wa awamu ya sita hapo Rwanda...
Unarukia ndonga kwa mbele huku ukiwa hujui hata unachoongea.

Ungejua wakina Rwigyema,Kagame na wenzake walikua ni wakina nani hapo NRA na waasisi 23 wa NRA(iliyomuingiza madarakani M7) ni wakina nani usingekua hapa una discuss usichokijua.

We komaa na siasa za Chadema vs Mataga huku kwingine utapigwa ndonga.
 
Binaadamu wote tuna mapungufu yetu sasa sijaelewa ni funzo gani tunalolipata kwa kumzungumzia vibaya marehemu? kinachofanyika ni kumzungumzia vibaya marehemu na kibaya zaidi madudu yote anabebeshwa yeye peke yake ila wale aliyekuwa nao kwenye hiyo serikali yenye madudu wako kimya kama hawahusiki na lolote vile.
UHURU unajifanya hujui au hukuwepo?
Kila Mtu alitakiwa aseme Lazima hii NI KUTOKANA NA SERIKALI YA POMBE
uwe CCM AU Mbunge ni lazima kutanguliza hilo neno sawa na mtukufu
Hii Barabara ya lami imewekwa na Serikali ya POMBE
hili Daraja km si juhudi ya Serikali ya POMBE
Natoa shukrani zangu kwa kuchaguliwa katika hii serikali ya POMBE
Hakuna hata siku moja waliposema Serikali ya TANZANIA au inayoongozwa na CCM
Ndio maana leo Wabunge na Mawaziri wanatema Nyongo SGR miaka 80 mara Bwawa la Nyerere hapo ujue Wabunge hawakuhusishwa hiyo mipango kibao ukiwemo wa Daraja la Kigongo Busisi
Nikodmus Maganga Mbunge wa Mbongwe ni wilaya iliyopo mkoa wa Geita,ni kms 90 kufika chato
 
Kwa tunaojaza taarifa za ajira kule tamisemi poleni kwa changamoto.

Wengineo nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lugha yetu adhimu ya kiswahili ina misemo mingi lakini Leo naomba niutumie huo. Msemo huu hutumika kuelezea jambo mtu au watu hulazimika kulifanya ili tu kufanikisha azma zao.

Methali hii haiwafai wenye unafuu na wenye mamlaka maana wao hawana haja ya kuinama ili kuvipata vyauvunguni. Wao wanaweza kubinua au kupasua kitanda au chochote chenye huo uvungu.

Miezi 7 iliyopita hakuna Dunia hii ambae hakutujua sisi kama Tanzania kuwa ni Taifa lenye nguvu ya maamuzi maana hatukutaka kuinama ili tupate vya uvunguni. Kwa muda wote huo tulijinasibu kuwa tunatumia fedha za ndani na hatuhitaji kuinama maana tumekalia utajiri.

Katika vita dhidi ya Corona tulishasema tupo huru na hatuhitaji kuonamishwa na mabeberu ili tupate vimisaada vyao. Msimamo huo ulienda sambamba na kususia taratibu zao za kuvaa barakoa na masuala ya chanjo n.k.

Leo tumepata kiongozi mkuu wa nchi mwingine ambae nae alianza kwa msimamo huo huo ingawa kaja na mabadiriko makubwa. Katika masuala ya uchumi amesema sisi ni masikini na MASIKINI HAPENDI MWANA na kuongeza kuwa tunahitaji kusaidiwa na kuongeza nguvu kuinua uchumi wa nchi.

Katika vita dhidi ya Corona alisema ameunda tume maalum ili kujiridhisha kama ipo au haipo! Wakati akisema hayo hakuchukua tahadhari yeyote yakujikinga na Corona. Shughuli zote za serikali ziliendeshwa bila kuzingatia tahadhari dhidi ya janga hilo.

Ghafla ndani ya wiki moja toka atoke kuwasalimia majirani dalili zaonesha mambo magumu kama taifa tunatakiwa kuinama ili tupate vya uvunguni. Kabla hata ripot ya hiyo kamati haijatolewa naona barakoa zimetamalaki kwenye shughuli za kiserikali hasa zinazomhusisha kiongozi moja kwa moja.

Kuna uwezekano ameona kama taifa ili tufanikiwe kupata mikopo na misaada toka kwa wanazengo na wanyanyi wa Dunia ni lazima tuiname. Kama nchi tunatakiwa kuonesha nasi tunaungana na ulimwengu katika vita hii ili kuendana nao maana jirani anapolia si vema wewe kula bata.

Kutokana na kuinama huku nimeona sasa kama nchi mambo yanaanza kwenda sawa. Nchi ya Ujerman wametoa msaada wa mabilioni yapesa kutusaidia katika sekta ya utalii. Huku mabalozi wengine wakiahidi mambo kem kem ambayo yananeema katika nchi.

Kubwa zaidi mipaka inafunguka, wawekezaji wanaanza kujitokeza na vijana akina Msungwite tuliosota kitaa kwa nusu muongo tumeambiwa tutume maombi tena na matumaini ni makubwa yakupata ajira.

Kama masikini hatuna budi kuinama ili kupata vya uvunguni ili kufikia maisha bora kwa watanzania lakini tuiname kwa tahadhari. Maana unaweza kuinama halafu wakatulalia na kurudi pale pale kuwa TULILALIWA SANA.


Ukishindwa kupambana nao ungana nao, na mtaka cha uvunguni sharti AINAME.
View attachment 1780636
 
Mama anajua kuwachezea mabeberu,niliusoma mwongozo wa wizara ya afya kuhusu quarantine kwa watanzania wanaorudi kutoka nje ya nchi niliishia kucheka tu maana ile ni bonge la danganya beberu
 
Kwa sasa popote pale Wanaume ndio wanaongoza kwa mipasho na taarabu

Iwe bungeni, kwenye Nyumba za ibada masikini, viwanjani nk Wanaume ndio wapiga tararira wakuu. Why?!

Au ni ukosefu wa ajira

Nikikupa cheo kisha nikakutumbua kuna.maajabu gani?

Mwiba hutokea ulipoingilia
 
Ulishaona wanaume wanaanguka mapepo kanisani, na i wanawake tu jiulize kwa nini,shetani ana mkataba na wanawake sio wanaume,refer pale bustani ya eden shetani alimteka akili eva sio adam,wanaume hatudanganyiki na shetani
 
Unaruka ruka tu na wewe, jifunze kujenga hoja. Mara wanaume, mara ajira, mara kutumbua, ilimradi vituko.
 
Kwa sasa popote pale Wanaume ndio wanaongoza kwa mipasho na taarabu

Iwe bungeni, kwenye Nyumba za ibada masikini, viwanjani nk Wanaume ndio wapiga tararira wakuu. Why?!

Au ni ukosefu wa ajira

Nikikupa cheo kisha nikakutumbua kuna.maajabu gani?

Mwiba hutokea ulipoingilia
Hata hapa JF ni mianaume mipuuzi tu
 
Ulishaona wanaume wanaanguka mapepo kanisani, na i wanawake tu jiulize kwa nini,shetani ana mkataba na wanawake sio wanaume,refer pale bustani ya eden shetani alimteka akili eva sio adam,wanaume hatudanganyiki na shetani
Yeye mwenyewe ni mwanamke analijua hilo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom