Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,120
2,000
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Hatuwezi kuwa na Rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli, hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya Rais au Waziri Mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu.

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je, anajua jinsi ya kututoa?! Anajua anakotupeleka?

Nimejitahidi kuangalia Bunge ili nione labda Mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!

Hofu yangu juu ya yanayoendelea nchini

Ni dhahiri sasa bila kumung'unya maneno nchi hii inaelekea katika ombwe la Demokrasia.

(1) Tulianza kwa kuona nyumba za wananchi mabondeni zikibomolewa bila huruma, tushukuru mahakama ilipifa stop lile zoezi la sivyo hali ingekuwa mbaya zaidi.

(2) Tumeona Bunge likiminywa, lisionekane Live

(3) Tumeona watu wakisimamishwa kazi hadharani kwenye majukwaa ya kisiasa

(4)Tumeona watoto UDOM, waliodahiliwa na serikali ileile ya CCM wakifukuzwa kwa notisi ya masaa machache tu

(5) Tumeona wafanyabiashara wakitaitiwa, wakipelekewa vyombo vya dola eti wameficha sukari.

(6)Sasa tunashuhudia Vyama vya upinzani vikizuiwa kufanya siasa

HOFU YANGU.
(1) Mitandao ya Kijamii yenye Sauti kama JF kuanza kusumbuliwa

(2) Kubambikiana Kesi, ili kuwanyamazisha watu wenye kuukosoa utawala huu

(3) Kufukuza watu Kazi kisiasa, kuwapelekea wafanyabiashara bili za kodi kubwa

(4) Watu kupotezwa

TUNAFANYAJE?

(1) Tuwaunge mkono Wabunge wote wenye kuweka mbele maslahi ya Umma badala ya vyama vyao

(2) Ni lazima Vyombo vya habari viwe jasiri kuliita Sepetu, Sepetu

(3) Ni lazima tuendelee kuzungumza, kupiga kelele na kuusimamia ukweli

(4) Kila mmoja kwa nafasi yake hana budi kuwaelimisha wananchi madhara ya Ubanaji huu wa Demokrasia unaotamalaki kwa kasi nchini, vijiwe vya kahawa, vijiwe vya magazeti, kwenye magulio huko vijijini, misibani, kwenye vikao vya kifamilia, sherehe n.k

(5) Wasomi wetu, tunawahitaji kuliko wakati wowote ule tangu mfumo wa vyama vingi uanze, ni lazima wasimame bila woga

(6) Ni muhimu sana kuitumia mahakama kwa ajili ya kudai haki

Nchi hii tulipigania uhuru siyo kwa ajili ya barabara, maji na umeme peke yake, Tulitaka uhuru wa Kuendesha nchi yetu kidemokrasia, Tulitaka heshima ya kujitawala kwa maana uongozi unaoheshimu raia, unaolinda haki za binadamu, unaoheshimu uhuru wa watu wake, unaoheshimu utu na uongozi wa sheria.

Katika vitu ambavyo Watanzania hawatokubali na ninawatahadharisha viongozi wote wa leo na Kesho ni kwamba kwa mujibu wa misingi iliyowekwa na waasisi wanchi hii, Kamwe Watanzania hawatakubali Kuburuzwa Kiimla. ile hasira ya Umma waliyokutana nayo mwaka 2015, inaweza ikageuka mara kumi yake!, Ni hatari, naogopa sana! . Ni vizuri wakajifunza na kulijua hili.
Kazi tu; Fukuza, teua, vunja... Nchi haijengwi hivi brother

Rais wa awamu ya tano ana kila dalili za kufeli kama hatojirekebisha.
Dalili za awali.

1. Hamna hata waziri mmoja aliyeanza naye ambaye sasa wanaenda wote kwa ile kasi ya mwanzo. Maana yake wameshagundua kuwa gari imepotea dira na chombo ndio kinaenda mrama!

2. Maamuzi yote ya kukurupuka yameleta madhara zaidi kuliko faida kwa wananchi. Rejea Bomoabomoa ya mabondeni, sukari, ada elekezi na hili la vilaza!

3. Kukosa support toka chamani ni ishara tosha, serikali anazungumza kichina na chama kinazungumza "kidhungu" hapo lugha gongana kabisa!
Kwanini Magufuli atafeli na anaweza kuishia kutawala awamu 1.

1. Anachofanya rais kwa sasa ni kitu cha ajabu kabisa. Anaishi kama nchi haikuwahi kuwa na dira na wala chama chake hakikuwa na Sera na ilani za chaguzi zilizopita. Dr. Slaa alishayafanya haya ya kutumbua majipu lkn watu hawakumchagua kwa kuwa wao walitaka taasisi yenye dira kuliko mtu mwenye nguvu!

Magufuli anatawala kama rais wa upinzani, yet kwa karibu miaka 20 alikuwa anatuambia anatekeleza ilani ya uchaguzi ya ccm! Leo anashangaa na kufuta kila kitu!

2. Rais wa sasa amefuta na kudumaza taasisi zote imara zinazoisaidia serikali, na sasa yeye ndiye mwenye nguvu na mtendaji pekee! Huu ni utawala wa kifalme (Monarchy) ndio mfalme ana absolute power!

Mkuu unapunguza nguvu ya CAG leo unamnyima pesa CAG Ila unampa pesa Jaji Mkuu kwa mahakama ya majizi ambayo ina substitute mahakama nyingine nyingi, unahamisha pesa muhimu za kazi mbalimbali na kuzipeleka barabarani lkn unamnyima huyu msimamizi mkuu wa pesa za umma!

Serikali yako inalinyima bunge nguvu huku ukihubiri kusaka wezi na kusimamia haki! Hadi sasa kesi zilizogundulika na kuhukumiwa na bunge ni kubwa na nyingi kuliko zilizosimamiwa na mahakama zote toka Uhuru!

Kesi ya Richmond, EPA, Escrow, Lugumi zote ziliibuliwa, kuchunguzwa na kuhukumiwa na wabunge wetu! Kesi zote hizo hamna hata moja iliyochunguzwa, kusimamiwa ama kuhukumiwa na chombo chochote cha serikali na hata kama vipo uchunguzi wake umeishia ktk makarabrasha!

Leo serikali kipenzi cha Mungu, nyinyi watenda haki mnapunguza nguvu za taasisi zinazosaidia na kusimamia haki zitendeke!

Rais na serikali yako, sisi tunataka matokeo mazuri tu, na ahadi zako ni njema kweli!

Shida kuu ya awamu hii, mnashindana na awamu iliyopita, hamtaki kufanya muendelezo hata wa Yale mema ya awamu zilizotangulia!

Mkumbuke Mwl alichosema "wao kuna mambo mazuri wamefanya na yapo ya kijinga, chukueni Yale mazuri na ya kijinga achaneni nayo", nyinyi mnaacha yote!

Failure is guaranteed;

Hadi mh. Umeanza kazi, hakuna taasisi aliyoijenga, kikwete pamoja na watu kumuona dhaifu lkn aliijenga ofisi ya CAG, alipanua demokrasia bungeni, alilijenga jeshi la polisi na jeshi la wananchi, alijenga barabara, alifufua elimu, alikuza mifuko ya hifadhi za jamii, shirika la nyumba, reli, kilimo (kilimo kwanza), nishati (umeme, gesi)!

Wewe miezi 6 sasa, ni kukamata, kufukuza, kufuta, kuteua, kugawa mali za watu etc!

Brother, every second counts, ni sasa or never!

Si chamanichamani wala serikalini ambapo tunaona legacy, hatuoni mfumo rasmi unaoutengeneza vinginevyo una create vacuum, siku ukiwa haupo ofisini kila kitu kitasimama au tutaanza upya!

Please mh. Raisi kaa chini, tengeneza task force ya watu watakaokushauri, tafuta strong person level ya Kikwete, Mkapa, Mwinyi, Malecela, Warioba, Mwamnyange, Pinda, Sitta, Msuya, Pengo, Karume etc!

Tafuta watu ambao hawatakuogopa, watu waliojitosheleza kimadaraka, wenye upeo na uongozi wa muda mrefu ili wakushauri! Jifanyie semina elekezi kwanza, kisha unda team ya kudumu na jopo la wazee wa kuwa consult!

Una uwezo mkubwa, unadhamira ya dhati, lkn skills za uongozi na mbinu za kisiasa upo butu sana! Unahitaji kujifunza na kujifunza sio ujinga!

Ni wapumbavu tu ndio wataobeza au kucheka wazo hili, lkn kiukweli hata mwenyewe unajua ndani ya nafsi yako hukuwa president material, umeupata uraisi bila ya kujiandaa, unachojua tu ni kuwa unaweza! Ni kama dereva wa basi kapewa trekta!
Ndivyo hali ilivyo. Inawezekana mwenyewe na wasaidizi wake wakaona wanapatia lakini kwangu mimi anabomoa tena sana.

Uchumi. Tunaambiwa makusanyo yamepanda hadi 1.3 Bill kwa mwezi lakini fedha haionekani na maisha yamezidi ugumu. Mizigo bandarini imepunguwa sana na hali ya uchumi hairidhishi.
Watu hawana ajira na ajira hazipo zimeyeyuka na ndio kwanza uhakiki wa wafanyakazi hewa unaendelea na ni zoezi endelevu sijui litaisha lini.

Huduma. Madawa hospitalini hayatoshi, idadadi ya wanafunzi waliokatiwa mikopo imeongezeka na malalamiko ya idara za serikali kukosa mafungu ya uendeshaji yapo japo kwa usiri mkubwa.

Hali ya Siasa. Mivutano na kuvurugwa kwa demokrasia, malalamiko ya kukiukwa katiba na haki za kisiasa yameongezeka ndani ya muda mfupi. Uvumilivu wa kisiasa unaelekea kuibuka na kupotezeana muda kwa kufanywa vitimbi vya makusudi vinavyoashiria kubomoka kwa misingi ya demokrasia iliyokwisha jengwa kwa muda wote wa siasa za vyama vingi tena sehemu zote mbili Bara na visiwani. Watu wananyimwa haki za kisiasa na uhuru wa kuzungumza . Kuna viashiria vya kidikteta kila eneo ambalo mtawala anaona ni hatari kwake. Mambo ni mengi tu.

Malalamiko ya wafanyakazi. Wafanyakazi wanatishwa na kutumbuliwa bila kufuatwa taratibu kazi iliyopo ni "Kutumbuwa, Kuteua na Kutengua" (KKK) hatuoni ufanisi. Kuna visasi na kutoaminmiana. wafanyakazi hawako huru kutumia weledi wao, wanasubiri maelekezo. Maelekezo hayana formula. Unaweza UKATUMBUWA KWA NAFASI YAKO KAMA MKUBWA WA ENEO LAKINI GHAFLA MAAMUZI YANATENGULIWA. Kumekosekana mfumo kuna maagizo tu kutoka juu.

Sera. Mimi siioni, sijui tunelekea wapi tena katika nyanja zote. Si kiuchumi ingawa tunaambiwa wa viwanda lakini siuoni msingi wake. Si kisiasa naona tunarudi nyuma sana na kupandikiza uadui na kushutumiana bure. Si kijamii nako kunaathiriwa na siasa mbaya vile vile. Sera ya mambo ya nje siijui, Tunaondowa na kuweka , Inasikitisha kwa mara ya Kwanza Tanzania Kuripotiwa Vibaya huko UNHCR na UN, tumeanza kupoteza heshima yetu na kutofautiana na rafiki zetu wa muda mrefu.


HITIMISHO. Kwa ufupi wa maneno wa makala hii fupi, ni muda wa mwaka tu tokea awamu hii ya tano iwepo lakini tumeshuka sana katika maeneo yaliyotajwa. Kwa mtazamo wangu malalamiko yamezidi, ajira hakuna, wafanyakazi wanalalamikia mengi, wanasiasa wanalia na kupaza sauti za demopkrasia, ajira hakuna na mengine mengi Hii si ishara nzuri.

Katika hali hii ,umoja wa kitaifa na amani ya nchi inakwazwa na uadui unajengeka miongoni mwa Watanzania. Kipindi hiki kifupi kimekuza nyufa kati ya WADAU wa kujenga Taifa letu na ukinzani wa mawazo kati ya Dola na watawaliwa umeanza kuibuka. Misingi ya Umoja hujengwa kwa sera madhubuti na kufuatwa KATIBA ambayo kwa sasa inasiginwa sana.

Kwa muhtasari huu Rais JPM kama kiongozi Mkuu wa Nchi hawezi kuepuka lawama na kwangu mimi anabomoa zaidi kuliko kujenga.

Kishada.
Tulianza na moto wa kubana matumizi, kutimua vyeti fwki na watumishi hewa yote haya yalikuwa na nia njema kabisa lakini utekelezaji wake ulipoanza kubagua nani atoke nani abaki tatizo likaanza. Chuki ikaanza kujijenga baina ya wanaopendelewa na wasiopendelewa.

Tanzania imejengwa katika utaifa, mtu anapoanza kuleta ukabila na uchama kwa lengo la kutugawa inabidi tumpinge wote kwa juhudi kubwa. Hatutakiwi kufumbia macho jambo hili sasahivi kuna chuki za kikabila zinaanza kujionyesha wazi wazi, chuki za kikanda na chuki za kivyama.

Ombi langu watanzania kama tulivyolelewa na tunavyopendana hebu tusiwasikilize viongozi wa aina hii.

Tuko kwenye kuivusha Tanzania kwenye umaskini uliotopea hizi chuki zitaturudisha nyuma kwa kasi sana.
1. Anatutoa kwenye usafiri wa treni wa enzi za kikoloni unaotumia muda mrefu njiani anatupeleka kwenye usafiri wa treni wa kisasa unaotumia umeme na muda mchache njiani kusafirisha Watu wengi na mizigo mingi.

2. Anatutoa kwenye usafiri wa anga wa ndege uliokufa anatupeleka kwenye ufufuo wa shirika la ndege lenye ndege mpya sita.

3. Ametutoa kwenye shirika la simu lililokufa ametupeleka kwenye ufufuo wa shirika la simu linaloleta ushindani mkubwa kwenye makampuni ya simu yaliyokuwapo kutokana na ubora wa huduma na wa gharama nafuu.

4. Ametutoa kwenye uchumi uliokuwa asilimia 5.1 mwaka 2015 mpaka kutupeleka kwenye uchumi unaokuwa wa zaidi ya asilimia 7.2

5. Ametutoa kwenye mzigo wa kulipia elimu mpaka kutupeleka kwenye unafuu wa elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari.

6. Amewatoa akina Mama Wajawazito kwenye mateso ya kujifungulia sakafuni ametupeleka kwenye faraja kwa akina Mama Wajawazito kujifungulia vitandani. Mjamzito mmoja, kitanda kimoja.

7. Ametutoa kwenye mateso ya kulanguliwa dawa na ukosefu wa dawa kwenye hospitali za Serikali ametupeleka kwenye upatikanaji wa madawa mahospitalini uliofikia kiwango cha upatikanaji cha asilimia 89, tena kwa bei nafuu.

8. Ametutoa kwenye usumbufu na mateso kwa Wamachinga na Mama Ntilie kusumbuliwa na Wagambo mpaka kutupeleka kwenye utulivu na amani ya kutosumbuliwa kwa Wamachinga na Mama Ntilie.

9. Ametutoa kwenye mfumo wa kuleana na kuchekeana dhidi ya wabadhilifu na wala rushwa na kutupeleka kwenye mfumo wa uwajibikaji wa kupelekwa mahakamani kwa wala rushwa na Mafisadi. Leo hii Tanzania imepanda kwa nafasi kwa nafasi 13 katika mwaka 2016 na mwaka 2017 na pia ikishika nafasi ya pili kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

10. Ametutoa kwenye mateso ya Wanafunzi kukaa chini kwa kukosa madawati na kukosa maabara. Leo hii ametupeleka kwenye hatua ya ukamilifu wa uondoshaji wa tatizo la madawati nchi nzima na maabara kwa baadhi ya shule.

11. Anatutoa kwenye uondoshaji wa tatizo la foleni jijini Dar na kutupeleka kwenye ujenzi wa barabara za juu (flyovers) za Tazara na Ubungo.

12. Amewatoa Wanazuoni wa chuo kikuu cha UDSM kwenye mateso ya kupanga na leo hii amewapeleka kwenye makazi bora ya mabweni ya kisasa wanayolipia gharama za chini kabisa.

13. Ametutoa kwenye balaa la utendaji na uwajibikaji wa hovyo kwa Watumishi wa umma na ametupeleka kwenye uimarishwaji wa kiwango cha kuridhisha cha uwajibikaji na uadilifu kwa Watumishi wa umma.

14. Ametutoa kwenye utitiri wa kodi kwenye kilimo na kutupeleka kwenye ufutwaji wa kodi mbalimbali za kilimo na kukifanya kuwa chenye tija kwa Wakulima. Leo hii bei ya korosho imepanda kutoka Tsh. 800 kwa kilo mpaka kufikia Tsh. 4000 kwa kilo.

15. Ametutoa kwenye usiri mkubwa wa mikataba na taarifa za madini na kutupeleka kwenye uwazi taarifa na mikataba ya madini. Leo hii tunajivunia mafanikio ya gawio sawia la faida za madini na Serikali ikimiliki asilimia 16 ya hisa katika makampuni ya uchimbaji wa madini.

16. Ametutoa kwenye tatizo zito na sugu la ajira na kutupeleka kwenye ongezeko la fursa za ajira kupitia kwenye viwanda zaidi ya 3000, kuwatimua wenye vyeti vyeki, miradi ya ujenzi ya bomba la mafuta, flyovers na reli ya kisasa ya standard gauge.

17. Ametutoa kwenye makusanyo ya Tsh. Bilioni 800 kwa mwezi mpaka kufikia kwenye makusanyo ya Tsh. Trilioni 1.5 kwa mwezi. Hali hiyo imeimarisha uwezo wa Serikali kibajeti.

18. Ametutoa kwenye urasimu na umangimeza kwa viongozi na kutupeleka kwenye uimarishwaji wa kiwango cha nidhamu, uwajibikaji na uadilifu kwa viongozi wa Serikali. Leo hii hakuna usumbufu kumuona kiongozi na viongozi wengi wapo site palipo shida za Wananchi wakizitatua.

19. Ametutoa kwenye mfumo wa walio nacho kujiona Mungu mtu na kuleta ukandamizi ndani ya jamii na kutupelekea kwenye uondoaji wa tabaka la uonevu kwenye masuala ya ardhi na sheria.

20. Ametutoa kwenye mkwamo wa Serikali kuhama Dar es Salaam na kutupeleka kwenye hamisho la Serikali kuhamia Dodoma. Mpaka sasa Waziri Mkuu, Wizara na idara mbalimbali zimehamia Dodoma. Tukumbuke mpango wa Serikali kuhamia Dodoma ulikuwepo na kushindikana kufanyika toka enzi za utawala wa Serikali ya awamu ya kwanza.

Hayo ni baadhi tu, sisi Wananchi wa Tabaka la chini tunaelewa Rais Magufuli alipotutoa na anapotupeleka.

*Tunasimama na Rais Magufuli*

*Na Emmanuel J. Shilatu*
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
9,498
2,000
Breaking News !

Dr. Faustine Engelbert Ndugulile ashinda kura za maoni za ndani ya chama cha CCM jimbo la Kigamboni jijini Dar es Sakaam.

Kura za maoni za wajumbe halali zilikuwa 399 hakuna kura iliyoharibika na Dr. Faustine Engelbert Ndugulile amefanikiwa kupata kura 190 za wajumbe hao wa mkutano wa wilaya ya Kigamboni..kuelekea uchaguzi Mkuu Oktoba 2020
 

Kinoamiguu

JF-Expert Member
Nov 29, 2018
2,853
2,000
Wanajamvi,

Magufuli ni kiongozi mwenye kutegemea siasa za ghilba, uongo na danganya toto. Analazimisha kupenda.
Juzi akitoka msibani alikuja kwa gari. Kama ilivyokawaida kwa wapambe wakamwandalia mikutano (amesimamishwa na wananchi ?). alikwenda mbali zaidi kwa kujiandalia zawadi ya kuku mwenyewe ili ionekane kapewa na wananchi. Hilo sio kweli. Hata ukimuona tu yule kuku utabaini kwamba SIYO WA KIENYEJI, ni kuku wa kufugwa; wengine wanawaita wa kizungu. Kwanza ni safi kuliko hawa wanaochakula.

Mwananchi wa kawaida kabisa hawezi moja kwa moja atoke huko alikotoka apeleke kuku kwa mkuu wa nchi, tena anayelindwa kwa mitutu ya bunduki na uzio wa chuma, sio rahisi.

Hoja ni je watu wa Kusini wana nini cha kujivunia toka kwako hadi upewe kuku kama zawadi badala ya zawadi kama ule moshi?

Uliwapora korosho zao mpaka leo wanadai, hapakuwa na sabababu ya serikali kupora korosho za watu wanaoitwa wanyonge ikijua haina pesa za kuwalipa (Mpaka leo wanadai) na kila akienda huko hutangaza kwamba zimeingizwa BL 21 ili kuwalipa kumbe uongo.

Aliingia madarakani kukiwa na zao la mbaazi, tena ikiwa bei juu kwelikweli. Badala ya kuimarisha akaanza kuingiza mambo binafsi na kina MANJI waliokuwa wanunuzi wakubwa. leo mbaazi imekufa kifo cha kawaida kabisa huku aliyeua akijiita kiongozi wa wanyonge.

Akiwa Mkuranga aliandaliwa kada wa chama kuuliza swali (MKURANGA NAKO KUNA KOROSHO). Ni MKURANGA ambako wananchi waliuwawa kwa kisingizio cha VITA ya ugaidi mpaka leo hakuna gaidi aliyekamatwa. miaka 3 nyuma wananchi wa huko walilazimika kutembea na VITAMBULISHO kwenye ardhi ya nyumbani nenda Rufiji leo ukaambiwe watu walivyo vunjiwa utu wao, utashangaa.

Hivi familia ya Anzory Gwanda inaweza kutoa jogoo na kumpa Magufuli?

Swala la Mgogoro wa Ardhi mkuranga sio la leo lilikuwepo tangu 1960. Wewe ulishawahi kuwa waziri wa ardhi kwanini hukulitatua hadi uwe rais? Ulaghai huu.

Nampa hongera mototo yule alikuuliza swala la MADAWATI. Hakika ulikosa majawabu nina hakika yule hakupangwa alikustukiza.

Ndugu zangu hata hapa Dar kuna shule nyingi tu watoto wanakaa chini zipo na Magufuli anazijua. Badala ya kumaliza kabisa tatizo la madawati yeye ananunua MIDUBWASHA/NDEGE na kuipaki pale JKNIA.

Hata iweje, aliyeporwa KOROSHO hawezi kumpa mporaji wake zawadi ya JOGOO. Ni ghiliba tu.
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
50,550
2,000
Mapupuli sinema zake Ni sawa na sinema za x ambazo watu wamevaa nguo, hazivutii na Wala hazina msisimko.
Yaani mtu atoke huko na linguo lake la kijani na kuku mkononi kisha ampe Rais? Sasa ulinzi wote ule wa mabunduki una kazi gani Kama raisi Yuko easily approached namna ile?
 

Hero

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
2,166
2,000
P
Wanajanvi.
Magufuli ni kiongozi mwenye kutegemea siasa za ghilba, uongo na danganya toto. analazimisha kupenda.
Juzi akitoka msibani alikuja kwa gari. Kama ilivyokawaida kwa wapambe wakamwandalia mikutano (amesimamishwa na wananchi ?). alikwenda mbali zaidi kwa kujiandalia zawadi ya kuku mwenyewe ili ionekane kapewa na wananchi. Hilo sio kweli. hata ukimuona tu yule kuku utabaini kwamba SIYO WA KIENYEJI. ni kuku wa kufugwa wengine wanawaita wa kizungu. kwanza ni safi kuliko hawa wanaochakula.
mwananchi wa kawaida kabisa hawezi moja kwa moja atoke huko alikotoka apelike kuku kwa mkuu wa nchi Tena anayelinda kwa mitutu ya bunduki na uzio wa chuma sio rahisi.
Hoja ni je watu wa kusini wana nini cha kujivunia toka kwako hadi upewe kuku kama zawadi badala ya zawadi kama ule moshi?
Uliwapora korosho zao mpaka leo wanadai, hapakuwa na sabababu ya serikali kupora korosho za watu wanaoitwa wanyonge ikijua haina pesa za kuwalipa (Mpaka leo wanadai) na kila akienda huko hutangaza kwamba zimeingizwa BL 21 ili kuwalipa kumbe uongo.
Aliingia madarakani kukiwa na zao la mbaazi. tena ikiwa bei juu kwelikweli. Badala ya kuimarisha akaanza kuingiza mambo binafsi na kina MANJI waliokuwa wanunuzi wakubwa. leo mbaazi imekufa kifo cha kawaida kabisa huku aliyeua akijiita kiongozi wa wanyonge
Akiwa Mkuranga aliandaliwa KADA Wa chama kuuliza swali (MKURANGA NAKO KUNA KOROSHO). ni MKURANGA ambako wananchi waliuwawa kwa kisingizio cha VITA ya ugaidi mpaka leo hakuna gaidi aliyekamatwa. miaka 3 nyuma wananchi wa huko walilazimika kutembea na VITAMBULISHO kwenye ardhi ya nyumbani nenda Rufiji leo ukaambiwe watu walivyo vunjiwa utu wao, utashangaa. hivi familia ya Anzory Gwanda inaweza kutoa jogoo na kumpa Magufuli?
swala la Mgogoro wa Ardhi mkuranga sio la leo lilikuwepo tangu 1960. wewe ulishawahi kuwa waziri wa ardhi kwanini hukulitatua hadi uwe raisi? ulaghai huu.
Nampa hongera motto yule alikuuliza swala la MADAWATI hakika ulikosa majawabu nina hakika yule hakupangwa alikustukiza.
Ndugu zangu hata hapa Dar kuna shule nyingi tuu watoto wanakaa chini zipo na Magufuli anazijua. badala ya kumaliza kabisa tatizo la madawati yeye ananunua MIDUBWASHA/NDEGE na kuipaki pale JKN
Hata iweje Aliyeporwa KOROSHO hawezi kumpa mporaji wake zawadi ya JOGOO
Ni GHIRIBA TU
Peleka upumbafu wako huko majuha wenzio! Hizo tuhuma zako dhidi ya Magu ni za kubumba! Watz hatuhitaji lecture za kipumbavu! Tumeshampima Magu na tumeridhika pasi mashaka Kuwa anatufaa na ni mtendaji zaidi...siyo Kama wapuuzi wenzenu huko kuchakuchwa ni makelele kwa Magu lakini ukiwauliza waonyeshe chema walixhofanya ktk nafasi zao unakuta upuuzi mtupu na Sacco's zao! Hao ndio mnatumia nguvu kubwa kuwanadi! Niwape pole maana mnayofanya yote watz tunaelewa na tutawafundisha SoMo Oct 2010!
Magu ni zawadi ya Mungu kwa watz walioomba kwa miongo kadhaa Sasa!
 

nditolo

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
2,245
2,000
Baada ya kuuwa soko la mbaazi akaamua kuua kabisa soko la korosho. Mbazi tulizolima mwaka 2017 ziliozea shambani tulishindwa hata kuzivuna. Mnunuzi mkuu bwana Manji aliwekwa maabusu miezi kibao soko likafa na mkuu akafurahi sana. Korosho akatuma wanajeshi waje kutunyanyang'anya tukawa tunatakiwa kuonyesha mashamba utafikiri kuna mtu amelalamika kaibiwa korosho zake.

Na kwavile mzee wa malofa kafa maana alitegewa kulazimisha kutangazwa kwa kura zisizo halali. utaambulia Moshi kama ule wa Nachingwea.
 

nditolo

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
2,245
2,000
P

Peleka upumbafu wako huko majuha wenzio! Hizo tuhuma zako dhidi ya Magu ni za kubumba! Watz hatuhitaji lecture za kipumbavu! Tumeshampima Magu na tumeridhika pasi mashaka Kuwa anatufaa na ni mtendaji zaidi...siyo Kama wapuuzi wenzenu huko kuchakuchwa ni makelele kwa Magu lakini ukiwauliza waonyeshe chema walixhofanya ktk nafasi zao unakuta upuuzi mtupu na Sacco's zao! Hao ndio mnatumia nguvu kubwa kuwanadi! Niwape pole maana mnayofanya yote watz tunaelewa na tutawafundisha SoMo Oct 2010!
Magu ni zawadi ya Mungu kwa watz walioomba kwa miongo kadhaa Sasa!
Umempima na mama yako. Kenge wee
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom