Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,120
2,000
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Hatuwezi kuwa na Rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli, hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya Rais au Waziri Mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu.

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je, anajua jinsi ya kututoa?! Anajua anakotupeleka?

Nimejitahidi kuangalia Bunge ili nione labda Mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!

Hofu yangu juu ya yanayoendelea nchini

Ni dhahiri sasa bila kumung'unya maneno nchi hii inaelekea katika ombwe la Demokrasia.

(1) Tulianza kwa kuona nyumba za wananchi mabondeni zikibomolewa bila huruma, tushukuru mahakama ilipifa stop lile zoezi la sivyo hali ingekuwa mbaya zaidi.

(2) Tumeona Bunge likiminywa, lisionekane Live

(3) Tumeona watu wakisimamishwa kazi hadharani kwenye majukwaa ya kisiasa

(4)Tumeona watoto UDOM, waliodahiliwa na serikali ileile ya CCM wakifukuzwa kwa notisi ya masaa machache tu

(5) Tumeona wafanyabiashara wakitaitiwa, wakipelekewa vyombo vya dola eti wameficha sukari.

(6)Sasa tunashuhudia Vyama vya upinzani vikizuiwa kufanya siasa

HOFU YANGU.
(1) Mitandao ya Kijamii yenye Sauti kama JF kuanza kusumbuliwa

(2) Kubambikiana Kesi, ili kuwanyamazisha watu wenye kuukosoa utawala huu

(3) Kufukuza watu Kazi kisiasa, kuwapelekea wafanyabiashara bili za kodi kubwa

(4) Watu kupotezwa

TUNAFANYAJE?

(1) Tuwaunge mkono Wabunge wote wenye kuweka mbele maslahi ya Umma badala ya vyama vyao

(2) Ni lazima Vyombo vya habari viwe jasiri kuliita Sepetu, Sepetu

(3) Ni lazima tuendelee kuzungumza, kupiga kelele na kuusimamia ukweli

(4) Kila mmoja kwa nafasi yake hana budi kuwaelimisha wananchi madhara ya Ubanaji huu wa Demokrasia unaotamalaki kwa kasi nchini, vijiwe vya kahawa, vijiwe vya magazeti, kwenye magulio huko vijijini, misibani, kwenye vikao vya kifamilia, sherehe n.k

(5) Wasomi wetu, tunawahitaji kuliko wakati wowote ule tangu mfumo wa vyama vingi uanze, ni lazima wasimame bila woga

(6) Ni muhimu sana kuitumia mahakama kwa ajili ya kudai haki

Nchi hii tulipigania uhuru siyo kwa ajili ya barabara, maji na umeme peke yake, Tulitaka uhuru wa Kuendesha nchi yetu kidemokrasia, Tulitaka heshima ya kujitawala kwa maana uongozi unaoheshimu raia, unaolinda haki za binadamu, unaoheshimu uhuru wa watu wake, unaoheshimu utu na uongozi wa sheria.

Katika vitu ambavyo Watanzania hawatokubali na ninawatahadharisha viongozi wote wa leo na Kesho ni kwamba kwa mujibu wa misingi iliyowekwa na waasisi wanchi hii, Kamwe Watanzania hawatakubali Kuburuzwa Kiimla. ile hasira ya Umma waliyokutana nayo mwaka 2015, inaweza ikageuka mara kumi yake!, Ni hatari, naogopa sana! . Ni vizuri wakajifunza na kulijua hili.
Kazi tu; Fukuza, teua, vunja... Nchi haijengwi hivi brother

Rais wa awamu ya tano ana kila dalili za kufeli kama hatojirekebisha.
Dalili za awali.

1. Hamna hata waziri mmoja aliyeanza naye ambaye sasa wanaenda wote kwa ile kasi ya mwanzo. Maana yake wameshagundua kuwa gari imepotea dira na chombo ndio kinaenda mrama!

2. Maamuzi yote ya kukurupuka yameleta madhara zaidi kuliko faida kwa wananchi. Rejea Bomoabomoa ya mabondeni, sukari, ada elekezi na hili la vilaza!

3. Kukosa support toka chamani ni ishara tosha, serikali anazungumza kichina na chama kinazungumza "kidhungu" hapo lugha gongana kabisa!
Kwanini Magufuli atafeli na anaweza kuishia kutawala awamu 1.

1. Anachofanya rais kwa sasa ni kitu cha ajabu kabisa. Anaishi kama nchi haikuwahi kuwa na dira na wala chama chake hakikuwa na Sera na ilani za chaguzi zilizopita. Dr. Slaa alishayafanya haya ya kutumbua majipu lkn watu hawakumchagua kwa kuwa wao walitaka taasisi yenye dira kuliko mtu mwenye nguvu!

Magufuli anatawala kama rais wa upinzani, yet kwa karibu miaka 20 alikuwa anatuambia anatekeleza ilani ya uchaguzi ya ccm! Leo anashangaa na kufuta kila kitu!

2. Rais wa sasa amefuta na kudumaza taasisi zote imara zinazoisaidia serikali, na sasa yeye ndiye mwenye nguvu na mtendaji pekee! Huu ni utawala wa kifalme (Monarchy) ndio mfalme ana absolute power!

Mkuu unapunguza nguvu ya CAG leo unamnyima pesa CAG Ila unampa pesa Jaji Mkuu kwa mahakama ya majizi ambayo ina substitute mahakama nyingine nyingi, unahamisha pesa muhimu za kazi mbalimbali na kuzipeleka barabarani lkn unamnyima huyu msimamizi mkuu wa pesa za umma!

Serikali yako inalinyima bunge nguvu huku ukihubiri kusaka wezi na kusimamia haki! Hadi sasa kesi zilizogundulika na kuhukumiwa na bunge ni kubwa na nyingi kuliko zilizosimamiwa na mahakama zote toka Uhuru!

Kesi ya Richmond, EPA, Escrow, Lugumi zote ziliibuliwa, kuchunguzwa na kuhukumiwa na wabunge wetu! Kesi zote hizo hamna hata moja iliyochunguzwa, kusimamiwa ama kuhukumiwa na chombo chochote cha serikali na hata kama vipo uchunguzi wake umeishia ktk makarabrasha!

Leo serikali kipenzi cha Mungu, nyinyi watenda haki mnapunguza nguvu za taasisi zinazosaidia na kusimamia haki zitendeke!

Rais na serikali yako, sisi tunataka matokeo mazuri tu, na ahadi zako ni njema kweli!

Shida kuu ya awamu hii, mnashindana na awamu iliyopita, hamtaki kufanya muendelezo hata wa Yale mema ya awamu zilizotangulia!

Mkumbuke Mwl alichosema "wao kuna mambo mazuri wamefanya na yapo ya kijinga, chukueni Yale mazuri na ya kijinga achaneni nayo", nyinyi mnaacha yote!

Failure is guaranteed;

Hadi mh. Umeanza kazi, hakuna taasisi aliyoijenga, kikwete pamoja na watu kumuona dhaifu lkn aliijenga ofisi ya CAG, alipanua demokrasia bungeni, alilijenga jeshi la polisi na jeshi la wananchi, alijenga barabara, alifufua elimu, alikuza mifuko ya hifadhi za jamii, shirika la nyumba, reli, kilimo (kilimo kwanza), nishati (umeme, gesi)!

Wewe miezi 6 sasa, ni kukamata, kufukuza, kufuta, kuteua, kugawa mali za watu etc!

Brother, every second counts, ni sasa or never!

Si chamanichamani wala serikalini ambapo tunaona legacy, hatuoni mfumo rasmi unaoutengeneza vinginevyo una create vacuum, siku ukiwa haupo ofisini kila kitu kitasimama au tutaanza upya!

Please mh. Raisi kaa chini, tengeneza task force ya watu watakaokushauri, tafuta strong person level ya Kikwete, Mkapa, Mwinyi, Malecela, Warioba, Mwamnyange, Pinda, Sitta, Msuya, Pengo, Karume etc!

Tafuta watu ambao hawatakuogopa, watu waliojitosheleza kimadaraka, wenye upeo na uongozi wa muda mrefu ili wakushauri! Jifanyie semina elekezi kwanza, kisha unda team ya kudumu na jopo la wazee wa kuwa consult!

Una uwezo mkubwa, unadhamira ya dhati, lkn skills za uongozi na mbinu za kisiasa upo butu sana! Unahitaji kujifunza na kujifunza sio ujinga!

Ni wapumbavu tu ndio wataobeza au kucheka wazo hili, lkn kiukweli hata mwenyewe unajua ndani ya nafsi yako hukuwa president material, umeupata uraisi bila ya kujiandaa, unachojua tu ni kuwa unaweza! Ni kama dereva wa basi kapewa trekta!
Ndivyo hali ilivyo. Inawezekana mwenyewe na wasaidizi wake wakaona wanapatia lakini kwangu mimi anabomoa tena sana.

Uchumi. Tunaambiwa makusanyo yamepanda hadi 1.3 Bill kwa mwezi lakini fedha haionekani na maisha yamezidi ugumu. Mizigo bandarini imepunguwa sana na hali ya uchumi hairidhishi.
Watu hawana ajira na ajira hazipo zimeyeyuka na ndio kwanza uhakiki wa wafanyakazi hewa unaendelea na ni zoezi endelevu sijui litaisha lini.

Huduma. Madawa hospitalini hayatoshi, idadadi ya wanafunzi waliokatiwa mikopo imeongezeka na malalamiko ya idara za serikali kukosa mafungu ya uendeshaji yapo japo kwa usiri mkubwa.

Hali ya Siasa. Mivutano na kuvurugwa kwa demokrasia, malalamiko ya kukiukwa katiba na haki za kisiasa yameongezeka ndani ya muda mfupi. Uvumilivu wa kisiasa unaelekea kuibuka na kupotezeana muda kwa kufanywa vitimbi vya makusudi vinavyoashiria kubomoka kwa misingi ya demokrasia iliyokwisha jengwa kwa muda wote wa siasa za vyama vingi tena sehemu zote mbili Bara na visiwani. Watu wananyimwa haki za kisiasa na uhuru wa kuzungumza . Kuna viashiria vya kidikteta kila eneo ambalo mtawala anaona ni hatari kwake. Mambo ni mengi tu.

Malalamiko ya wafanyakazi. Wafanyakazi wanatishwa na kutumbuliwa bila kufuatwa taratibu kazi iliyopo ni "Kutumbuwa, Kuteua na Kutengua" (KKK) hatuoni ufanisi. Kuna visasi na kutoaminmiana. wafanyakazi hawako huru kutumia weledi wao, wanasubiri maelekezo. Maelekezo hayana formula. Unaweza UKATUMBUWA KWA NAFASI YAKO KAMA MKUBWA WA ENEO LAKINI GHAFLA MAAMUZI YANATENGULIWA. Kumekosekana mfumo kuna maagizo tu kutoka juu.

Sera. Mimi siioni, sijui tunelekea wapi tena katika nyanja zote. Si kiuchumi ingawa tunaambiwa wa viwanda lakini siuoni msingi wake. Si kisiasa naona tunarudi nyuma sana na kupandikiza uadui na kushutumiana bure. Si kijamii nako kunaathiriwa na siasa mbaya vile vile. Sera ya mambo ya nje siijui, Tunaondowa na kuweka , Inasikitisha kwa mara ya Kwanza Tanzania Kuripotiwa Vibaya huko UNHCR na UN, tumeanza kupoteza heshima yetu na kutofautiana na rafiki zetu wa muda mrefu.

HITIMISHO. Kwa ufupi wa maneno wa makala hii fupi, ni muda wa mwaka tu tokea awamu hii ya tano iwepo lakini tumeshuka sana katika maeneo yaliyotajwa. Kwa mtazamo wangu malalamiko yamezidi, ajira hakuna, wafanyakazi wanalalamikia mengi, wanasiasa wanalia na kupaza sauti za demopkrasia, ajira hakuna na mengine mengi Hii si ishara nzuri.

Katika hali hii ,umoja wa kitaifa na amani ya nchi inakwazwa na uadui unajengeka miongoni mwa Watanzania. Kipindi hiki kifupi kimekuza nyufa kati ya WADAU wa kujenga Taifa letu na ukinzani wa mawazo kati ya Dola na watawaliwa umeanza kuibuka. Misingi ya Umoja hujengwa kwa sera madhubuti na kufuatwa KATIBA ambayo kwa sasa inasiginwa sana.

Kwa muhtasari huu Rais JPM kama kiongozi Mkuu wa Nchi hawezi kuepuka lawama na kwangu mimi anabomoa zaidi kuliko kujenga.

Kishada.
Tulianza na moto wa kubana matumizi, kutimua vyeti fwki na watumishi hewa yote haya yalikuwa na nia njema kabisa lakini utekelezaji wake ulipoanza kubagua nani atoke nani abaki tatizo likaanza. Chuki ikaanza kujijenga baina ya wanaopendelewa na wasiopendelewa.

Tanzania imejengwa katika utaifa, mtu anapoanza kuleta ukabila na uchama kwa lengo la kutugawa inabidi tumpinge wote kwa juhudi kubwa. Hatutakiwi kufumbia macho jambo hili sasahivi kuna chuki za kikabila zinaanza kujionyesha wazi wazi, chuki za kikanda na chuki za kivyama.

Ombi langu watanzania kama tulivyolelewa na tunavyopendana hebu tusiwasikilize viongozi wa aina hii.

Tuko kwenye kuivusha Tanzania kwenye umaskini uliotopea hizi chuki zitaturudisha nyuma kwa kasi sana.
1. Anatutoa kwenye usafiri wa treni wa enzi za kikoloni unaotumia muda mrefu njiani anatupeleka kwenye usafiri wa treni wa kisasa unaotumia umeme na muda mchache njiani kusafirisha Watu wengi na mizigo mingi.

2. Anatutoa kwenye usafiri wa anga wa ndege uliokufa anatupeleka kwenye ufufuo wa shirika la ndege lenye ndege mpya sita.

3. Ametutoa kwenye shirika la simu lililokufa ametupeleka kwenye ufufuo wa shirika la simu linaloleta ushindani mkubwa kwenye makampuni ya simu yaliyokuwapo kutokana na ubora wa huduma na wa gharama nafuu.

4. Ametutoa kwenye uchumi uliokuwa asilimia 5.1 mwaka 2015 mpaka kutupeleka kwenye uchumi unaokuwa wa zaidi ya asilimia 7.2

5. Ametutoa kwenye mzigo wa kulipia elimu mpaka kutupeleka kwenye unafuu wa elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari.

6. Amewatoa akina Mama Wajawazito kwenye mateso ya kujifungulia sakafuni ametupeleka kwenye faraja kwa akina Mama Wajawazito kujifungulia vitandani. Mjamzito mmoja, kitanda kimoja.

7. Ametutoa kwenye mateso ya kulanguliwa dawa na ukosefu wa dawa kwenye hospitali za Serikali ametupeleka kwenye upatikanaji wa madawa mahospitalini uliofikia kiwango cha upatikanaji cha asilimia 89, tena kwa bei nafuu.

8. Ametutoa kwenye usumbufu na mateso kwa Wamachinga na Mama Ntilie kusumbuliwa na Wagambo mpaka kutupeleka kwenye utulivu na amani ya kutosumbuliwa kwa Wamachinga na Mama Ntilie.

9. Ametutoa kwenye mfumo wa kuleana na kuchekeana dhidi ya wabadhilifu na wala rushwa na kutupeleka kwenye mfumo wa uwajibikaji wa kupelekwa mahakamani kwa wala rushwa na Mafisadi. Leo hii Tanzania imepanda kwa nafasi kwa nafasi 13 katika mwaka 2016 na mwaka 2017 na pia ikishika nafasi ya pili kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

10. Ametutoa kwenye mateso ya Wanafunzi kukaa chini kwa kukosa madawati na kukosa maabara. Leo hii ametupeleka kwenye hatua ya ukamilifu wa uondoshaji wa tatizo la madawati nchi nzima na maabara kwa baadhi ya shule.

11. Anatutoa kwenye uondoshaji wa tatizo la foleni jijini Dar na kutupeleka kwenye ujenzi wa barabara za juu (flyovers) za Tazara na Ubungo.

12. Amewatoa Wanazuoni wa chuo kikuu cha UDSM kwenye mateso ya kupanga na leo hii amewapeleka kwenye makazi bora ya mabweni ya kisasa wanayolipia gharama za chini kabisa.

13. Ametutoa kwenye balaa la utendaji na uwajibikaji wa hovyo kwa Watumishi wa umma na ametupeleka kwenye uimarishwaji wa kiwango cha kuridhisha cha uwajibikaji na uadilifu kwa Watumishi wa umma.

14. Ametutoa kwenye utitiri wa kodi kwenye kilimo na kutupeleka kwenye ufutwaji wa kodi mbalimbali za kilimo na kukifanya kuwa chenye tija kwa Wakulima. Leo hii bei ya korosho imepanda kutoka Tsh. 800 kwa kilo mpaka kufikia Tsh. 4000 kwa kilo.

15. Ametutoa kwenye usiri mkubwa wa mikataba na taarifa za madini na kutupeleka kwenye uwazi taarifa na mikataba ya madini. Leo hii tunajivunia mafanikio ya gawio sawia la faida za madini na Serikali ikimiliki asilimia 16 ya hisa katika makampuni ya uchimbaji wa madini.

16. Ametutoa kwenye tatizo zito na sugu la ajira na kutupeleka kwenye ongezeko la fursa za ajira kupitia kwenye viwanda zaidi ya 3000, kuwatimua wenye vyeti vyeki, miradi ya ujenzi ya bomba la mafuta, flyovers na reli ya kisasa ya standard gauge.

17. Ametutoa kwenye makusanyo ya Tsh. Bilioni 800 kwa mwezi mpaka kufikia kwenye makusanyo ya Tsh. Trilioni 1.5 kwa mwezi. Hali hiyo imeimarisha uwezo wa Serikali kibajeti.

18. Ametutoa kwenye urasimu na umangimeza kwa viongozi na kutupeleka kwenye uimarishwaji wa kiwango cha nidhamu, uwajibikaji na uadilifu kwa viongozi wa Serikali. Leo hii hakuna usumbufu kumuona kiongozi na viongozi wengi wapo site palipo shida za Wananchi wakizitatua.

19. Ametutoa kwenye mfumo wa walio nacho kujiona Mungu mtu na kuleta ukandamizi ndani ya jamii na kutupelekea kwenye uondoaji wa tabaka la uonevu kwenye masuala ya ardhi na sheria.

20. Ametutoa kwenye mkwamo wa Serikali kuhama Dar es Salaam na kutupeleka kwenye hamisho la Serikali kuhamia Dodoma. Mpaka sasa Waziri Mkuu, Wizara na idara mbalimbali zimehamia Dodoma. Tukumbuke mpango wa Serikali kuhamia Dodoma ulikuwepo na kushindikana kufanyika toka enzi za utawala wa Serikali ya awamu ya kwanza.

Hayo ni baadhi tu, sisi Wananchi wa Tabaka la chini tunaelewa Rais Magufuli alipotutoa na anapotupeleka.

*Tunasimama na Rais Magufuli*

*Na Emmanuel J. Shilatu*
 
Rene Jr.

JF-Expert Member
Jan 31, 2014
3,642
2,000
June 2020, still relevant!
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Hatuwezi kuwa na Rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli, hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya Rais au Waziri Mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu.

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je, anajua jinsi ya kututoa?! Anajua anakotupeleka?

Nimejitahidi kuangalia Bunge ili nione labda Mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
 
crocodile

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
2,751
2,000
Kutoeleweka muelekeo wa safari inaweza kuwa tatizo la muongoza chombo au tatizo la kutoelewa tu la abiria mwenyewe.
 
battawi

JF-Expert Member
Mar 29, 2014
1,555
2,000
Katupeleka kwenye uchumi wa kati.
Ahaaa ,uchumi ambao ajira zimeota mbawa, hela imetoweka ,na ukata umetamalaki, kw umasikini kuongezeka?
Uchumi wa kati ni fursa za Mabepari kujitanua,
pato la serikali limengezeka sana, lakini kwa gharama ya kuwabana mno masikini ambao tayari wengi wao walikuwa wanakula mlo mmoja kwa siku.
sasa hawanauhakika nahuo mlo mmoja kamwe.
Omba omba wameongezeka, utapeli, wizi, ubabaishaji nk.
 
Attachments

Alphonce Kagezi

JF-Expert Member
Sep 29, 2015
295
250
Sasa Tanzania iko grad ya Uchumi wakati bado hujafumbuliwa Mh JPM anatupeleka wapi?
Labda ludisha mkanda nyuma zilejee kumbukumbu kwa usahihi utaiona njia tunayoindea
 
battawi

JF-Expert Member
Mar 29, 2014
1,555
2,000
Nawaomba muisikilize kwa umakini hii video.
Tanzania tunajigamba kuongeza kipato kwa kuongezeka kwa pato la nchi na kupanda GDP ,lakiniukija kwa watu wa kawaida ,umasikini unazidi kuwaelemea.
jibu lipo hapa.
Acha kukopa sana ili uondokane na madeni makubwa baki na uchumi unaolingana na msuli wako ''better late than never'' uharaka wa kuingia uchumi wa kati utatupasua msamba kwa kuwaridhisha Wazungu na Mabeberu wa IMF huku raia wako wanaangamia.
 
Attachments

kitimotojikoni

JF-Expert Member
Sep 24, 2018
384
1,000
Nawaomba muisikilize kwa umakini hii video.
Tanzania tunajigamba kuongeza kipato kwa kuongezeka kwa pato la nchi na kupanda GDP ,lakiniukija kwa watu wa kawaida ,umasikini unazidi kuwaelemea.
jibu lipo hapa.
Acha kukopa sana ili uondokane na madeni makubwa baki na uchumi unaolingana na msuli wako ''better late than never'' uharaka wa kuingia uchumi wa kati utatupasua msamba kwa kuwaridhisha Wazungu na Mabeberu wa IMF huku raia wako wanaangamia.
True mkuu, wanaangalia uchumi wa nchi tu, wakati raia hali ni mbaya huku mtaani kwa ujumla
 
JOYOPAPASI

Member
Jan 10, 2016
34
125
https://m.facebook.com/groups/474636815945586?view=permalink&id=3059609734114935

KAFULILA AZICHANA HOJA ZA ZITTO KUHUSU UCHUMI WA KATI. Soma iyo

JICHO LA PILI NA HOJA NANE KUHUSU UKOSOAJI REKODI YA UCHUMI WA KATI.

Na David KAFULILA
Julai 5, 2020- SONGWE

Tangu Julai1,2020, Benki ya dunia itangaze Tanzania kuwa Taifa lenye Uchumi wa kati miaka 5 kabla ya mwaka 2025, mengi yamesemwa!

Naomba nisitumie makala hii kuwajibu lakini itoshe nianze kwa kuhitimisha kwamba kwa mapinduzi makubwa ya nchi hii chini ya JPM nisawa na kusema JPM anashindana na rekodi yake mwenyewe kama nitakavyoeleza miaka 5 ya mapigo 8 ya JPM..

#Pigo la kwanza ni dunia kutambua kwamba Tanzania chini ya JPM sio ileile!

Uchumi wa kati unamaanisha tumefuzu kujitegemea zaidi. Hii ni hatua muhimu kuelekea kuliondoa Taifa letu kwenye kundi la Mataifa yenye uchumi duni ambayo hupewa kipaumbele cha misaada na mikopo nafuu.

Uongozi wake kusomeka katika sura ya unyonge! Hivyo hili ni pigo la kwanza kwa ambao walipenda kuaminisha Umma kuwa Tanzania ni ileile.

Benki ya dunia wamejibu kwamba Tanzania ya awamu ya 5 sio ileile kwani sasa ipo uchumi wa kati!

#Pili ni hoja kwamba mikopo nafuu itapungua kwakuwa tumeingia uchumi wa kati.

Ingawa ni kweli kwamba mikopo nafuu itapungua lakini athari yake ni ndogo kulinganisha na faida ya kupanuka kwa wigo wa kukopa mikopo ya kibiashara ambayo kawaida haiambatani na masharti ya kikoloni.

Ukweli huu unathibitishwa na hoja mbili, kwanza ni kiasi cha misaada na mikopo hiyo kuendelea kuwa sehemu ndogo sana ya mapato ya yetu!

Tazama utekelezaji wa bajeti ya mwaka jana 2019/20, ambapo katika mapato yote yaliyofikia Trilioni 26 kufikia Mwezi Aprili2020, kiasi kilichotokana na misaada na mikopo nafuu kilikuwa Trilioni 2.4 sawa na asilimia 9% tu ya Trilioni26.

Hivyo kupungua kwa misaada na mikopo nafuu athari yake ni ndogo sana kwakuwa mwenendo(trend) wa kupungua kwa misaada na mikopo nafuu upo hivyo kwa muda sasa!

Zaidi kutanuka kwa upatikanaji wa mikopo ya kibiashara ambayo siku zote haiambatani na masharti ya kikoloni ni faida na zaidi ni heshima hasa kwa Serikali kama ya JPM iliyojizatiti kujenga msuli wa kujitegemea.

Serikali ya JPM inajenga msuli wa kujitegemea kwa uwekezaji mkubwa sekta ya miundombinu ya kiuchumi ya usafiri, ujenzi na umeme.

Sanjari na hayo, uwekezaji mkubwa kwenye rasilimali watu kama inavyonekana katika sekta za Elimu, Maji na Afya.

#Tatu, Hoja kwamba kipimo cha ongezeko la pato la mtu (per capital income) sio uhalisia katika maisha halisi. Hoja hii ni sahihi kwa mtazamo wa jumla katika taaluma ya uchumi .

Hii ni kwasababu inawezekana uchumi wa nchi husika sio jumuifu au sehemu kubwa ya kinachozalishwa kinaishia akaunti za mafisadi nje au matumizi makubwa yanafanyika kwenye mambo yasio na faida sana kwa wananchi wake.

Mfano ni Marekani inavyotumia sehemu kubwa ya pato lake kwenye vita badala ya kuboresha maisha ya watu wake na hivyo kufanya kuwa Taifa la saba duniani kwa ubora wa maisha ingawa linaongoza kwa ukubwa wa uchumi duniani ikiwa linamiliki asilimia 20% ya uchumi wa dunia.

Hata hivyo hoja hii kwa Tanzania chini ya JPM haibebi sura hiyo kwasababu kwanza, Tanzania ndio nchi inayongoza kwa uchumi jumuifu Afrika kusini Katikati nchi za Africa zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara.

Mantiki hii inamaanisha kwamba tofauti ya aliyenacho na asiyenacho ni ndogo( Ripoti ya World Economic Forum 2018).

Zaidi Tanzania inafanya vizuri sana duniani katika usimamizi wa matumizi ya Serikali ndio maana ikatajwa kuwa Taifa la 28 kati ya nchi 186 duniani kwa udhibiti wa matumizi ikiziacha mbali Kenya 70, Uganda100, Msumbiji 69, Malawi 106, Botswana 37 ( rejea ripoti ya WEF: Executive Opinion Survey 2019).

Nchi yenye picha hii ni wazi tafsiri ya ongezeko la pato la mtu inakuwa na maana pana kwa watu wengi kama nilivyoeleza .

# Nne, Hoja kwamba hakuna uwiano wa kiasi cha fedha za bajeti kilichotumika ndani ya miaka5 kulinganisha na ongezeko la pato la mtu mmoja mmoja.

Hoja hii ina makengeza kwasababu matokeo ya uwekezaji mkubwa unaofanywa kwenye miundombinu mikubwa kama reli ya kisasa( SGR), Mradi wa umeme wa Stirglers Gorge hata uwekezaji mkubwa kwenye miradi ya Elimu, kufufua shirika la ndege, meli na bandari, matokeo yake sio ya muda mfupi (payback period).

Kwenye Sayansi ya uwekezaji, muda wa kurejesha ulichowekeza na hata faida vinategemea aina ya uwekezaji.

Ukiwekeza shamba la mchicha unaweza kurejesha mapato ndani ya mwezi. Lakin ukiwekeza shamba la miti utarejesha baada ya miaka10 na kuendelea lakin umejenga msingi endelevu.

Sasa pengine kuna watu walitamani nchi hii tuijenge kwa falsafa ya uwekezaji kwenye mchicha. Hakuna nchi iliendelea kwa falsafa hiyo. Iwe Vietnam, Malaysia, Korea kusini, Singapore, nk.

Mawazo ya namna hii yakipewa nafasi kwa kinachoitwa demokrasia tunaweza kugeuka Taifa la wachuuzi kwa nusu karne nyingine. Haya ni ya kukemea!

#Tano ni hoja kwamba mafanikio ya kufikia uchumi wa kati sio ya JPM kwani watangulizi wake walifanya pakubwa.

Hoja hii ina mapungufu ya aina mbili, kwanza kumekuwa na hoja kwa muda mrefu binafsi nakubaliana nayo;

kwamba nchi yetu ilichelewa sana kwani nchi tulizokuwa sambamba nazo kiuchumi hadi kufikia miaka ya 1990, nchi kama vietnam ( ilikuwa na uchumi wa $6.5bn sisi 4.5bn mwaka 1990- kwa ripoti za Bank ya dunia), leo zimeshatupita zaidi ya mara nne( Vietnam $260bn wakati Tanzania $63bn).

Takwimu hizi zinathibitisha kwamba tulikotoka hatukufanya vema. Mimi ninaamini miongo kadhaa tulipoteza na ndio siri ya kuachwa.

Lakini nina amini kwamba kwa msukumo mkubwa tulionao sasa katika kujenga miundombinu ya uchukuzi na umeme, niwazi haitachukua miongo mingi kabla ya Taifa hili kucheza ligi moja na waliotuacha tulipozubaa.

Mapinduzi anayofanya JPM leo walianza kufanya wenzetu miaka 30 nyuma, sisi tulibaki na mawazo bila kuyatekeleza ndio siri ya kuachwa.

Sasa leo yanatekelezwa anakuja mtu na mawazo yaleyale ya kujenga uchumi kwa falsafa mchicha kama nilivoeleza hapo juu.

Mapungufu ya pili ya hoja hii ni wivu tu wakisiasa kama vile mtu aseme mfungaji fulani asingefunga kama beki asingeanzisha pasi ikaenda katikati ndipo akapewa na kisha kufunga.

Sipuuzi mchango wa awamu zilizotangulia lakini sioni kwanini kasi kubwa ya msukumo huu wa kulazimisha sasa!Mzee Mwinyi, Rais mstaafu alipata kusema kila zama na kitabu chake.

# Sita:mfano wa kutumia uamuzi wa kununua ndege 11 kwamba hauna tija kwenye uchumi ni ukosoaji uliokosa nguvu kwa muda mrefu. Nchi hii imezungumza kwa miongo kadhaa kuhusu haja ya kufufua sekta ya uchukuzi ikiwemo shirika la ndege,usafiri wa maji na reli.

Tafiti zimeonesha mara kadhaa kwamba kwa bahati ya nafasi ya Tanzania kijiografia, tukiwekeza kwenye sekta ya uchukuzi kikamilifu, mchango wake utakuwa mkubwa sana kuliko sekta yoyote ( Rejea Poverty & Human Development Report 2008).

Kamati ya Bunge ya Miundombinu, katika Bunge la 11 ambalo nilikuwemo, walitoa taarifa na kurudia mara kwa mara kwamba zaidi ya asilimia 60% ya pesa anayoitumia mtalii inaishia kwenye usafiri wa ndege.

Sote tunajua Utalii ni sekta kinara kwa fedha za kigeni nchini. Sote tunaelewa umuhimu wa fedha za kigeni kwa dunia ya kisasa iliyounganishwa (modern globalized world).

Kwa upekee wa nafasi ya Tanzania kijiografia Africa, maamuzi ya kufufua Shirika la ndege isingepaswa kuwa hoja ya kubishaniwa.

Pengine hoja ingekuwa tunalifufuaje. Kwa mfano uamuzi wa kukodi ndege mbovu kwa dola milioni43, ndege ambayo ilifanya kazi miezi 6 na miezi 37 ikawa gereji haikuwa mkakati sahihi (rejea CAG ripoti ya Aprili 2020).

Lakini mkakati wasasa wa JPM kutumia dola 32m kununua bombardier mpya , kiasi ambacho ni pungufu ya tulichotumia kukodi ndege mbovu huko tulikotoka, ni mkakati ambao kila mwenye mapenzi ya nchi hii ingetosha kupongeza na kukiri kwamba tumetoka mbali!

# Saba: Hoja kwamba Serikali ina uhaba wa mafanikio ndio sababu imefurahia taarifa ya Benki ya dunia kuipandisha Tanzania daraja kuingia kundi la uchumi wa kati ni upofu wenye msukumo wa kisiasa.

Serikali ya awamu ya tano inarekodi kubwa zisizobishaniwa ( undisputeble) kitaifa na kimataifa. Rekodi ambazo kila anaejua kinachoendelea duniani anazifahamu.

Rekodi za ndani kama kugharamia elimu bure, kuvunja rekodi ya mapato na mauzo ya nje sekta ya madini, rekodi ya kuongeza kusambaza umeme vijijini zaidi ya vijiji 7000 ndani ya miaka 5 ( 2015-2020) na kufikia vijiji 9300 kutoka vijiji 2018 mwaka 2015 ni rekodi.

Rekodi ya kuongeza usambazaji maji vijijini kutoka asilimia 47% mwaka 2015 mpaka asilimia71% ni rekodi.

Rekodi ya kujenga hospitali 10 za rufaa za mikoa, kuongeza fedha za dawa na vifaa tiba kwa zaidi ya asilimia 700% kutoka billioni 31 mwaka 2015 mpaka billioni 269 ni rekodi.

Kifupi kasi ya kupungua kwa umasikini wa huduma ni kubwa sana. Tulikotoka gharama za huduma za afya zilikuwa kubwa maradufu kwa sababu sehemu kubwa ya gharama ilihusu kuifikia huduma yenyewe kuliko gharama halisi ya huduma kutokana na umbali wa kufikia na zaidi upatikanaji dawa.

Iliwezekana kutumia elfu 80 kwajili ya usafiri , Malazi na chakula kuifuata huduma ambayo unailipia elfu20.

Natamani wachumi zaidi wafanye Tafiti eneo hili la namna umasikini wa huduma ulivyopungua kutokana na ukaribu wa vituo vya kutolea huduma na ongezeko la upatikanaji wa huduma yenyewe kwa maana ya dawa.

Ujenzi wa reli, Meli, Shirika la ndege, mradi mkubwa wa umeme sanjari na kuliondoa Shirika la Tanesco kwenye mikataba mibovu hata kulifanya lijitegemee zote ni rekodi.

Tanesco kwa miaka 30 ilikuwa jini nyonyadamu kwa uchumi wa Tanzania. Kuna wakati gharama za kuliendesha ililingana na Bajeti ya Zanzibar kwa mikataba ya 'kijangili'. Kufyekwa mikataba ya hovyo na udhibiti ni mapinduzi makubwa.

Sijui mtu anayesema Serikali hii inauhaba wa rekodi alitaka rekodi zipi zaidi ndani ya miaka5.

Hizi nimetaja chache tena za ndani , lakini kimataifa, JPM ameshatengeneza rekodi lukuki kama nilivyoeleza wiki iliyopita kwenye makala yangu ya JPM NA REKODI SABA KIMATAIFA.

# Nane. Nihitimishe kwakusema kwamba nchi hii bado inasukwa. Ndani ya miaka5 , JPM ameisuka pakubwa sana. A Kauli mbiu za kisiasa za "Kazi na Bata" hazitofautiani sana na mzaha wa Mzee Cheyo mwaka 1995 ya KUJAZA WATU MAPESA.
IMG-20200706-WA0097.jpg
 
bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
9,307
2,000
6 July 2020
Lindi, Tanzania

MEMBE baada ya kurudisha kadi ya CCM/tutajiunga na chama tutagombea uongozi wa juu tutashinda
Bernard Carmillus Membe akiwa kijijini kwake Rondo mkoani Lindi kusini mwa Tanzania aongea mazito baada ya kuiacha CCM kwa kurudisha kadi ya uanachama.

Alihudumu chini ya Rais Jakaya Kikwete kama Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania kwa miaka 10. Pia alipata kuwa mbunge wa CCM jimbo la Mtama mkoani Lindi. Alihudumu kama afisa mwambata wa ubalozi wa Tanzania kwa miaka 10 huko Canada ktk bara la Marekani ya Kaskazini. Pia alipata kuwa Afisa Mchambuzi wa ripoti ktk Kurugenzi ya Usalama na Intelejensia wa Taifa TISS katika Ofisi ya Rais.

Hali ya kisiasa mikoa ya Lindi na Mtwara na kwingineko Tanzania kwa ujumla inaonesha waTanzania wapo tayari kwenda na Bernard Membe ili kuweza kuweka sawa masuala ya kama kilimo, uvuvi, mifugo, gesi na Maendeleo ya Watu.
Source : Gilly Bonny Online TV
 
Mafiningo

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
1,171
2,000
https://m.facebook.com/groups/474636815945586?view=permalink&id=3059609734114935

KAFULILA AZICHANA HOJA ZA ZITTO KUHUSU UCHUMI WA KATI. Soma iyo

JICHO LA PILI NA HOJA NANE KUHUSU UKOSOAJI REKODI YA UCHUMI WA KATI.

Na David KAFULILA
Julai 5, 2020- SONGWE

Tangu Julai1,2020, Benki ya dunia itangaze Tanzania kuwa Taifa lenye Uchumi wa kati miaka 5 kabla ya mwaka 2025, mengi yamesemwa!

Naomba nisitumie makala hii kuwajibu lakini itoshe nianze kwa kuhitimisha kwamba kwa mapinduzi makubwa ya nchi hii chini ya JPM nisawa na kusema JPM anashindana na rekodi yake mwenyewe kama nitakavyoeleza miaka 5 ya mapigo 8 ya JPM..

#Pigo la kwanza ni dunia kutambua kwamba Tanzania chini ya JPM sio ileile!

Uchumi wa kati unamaanisha tumefuzu kujitegemea zaidi. Hii ni hatua muhimu kuelekea kuliondoa Taifa letu kwenye kundi la Mataifa yenye uchumi duni ambayo hupewa kipaumbele cha misaada na mikopo nafuu.

Uongozi wake kusomeka katika sura ya unyonge! Hivyo hili ni pigo la kwanza kwa ambao walipenda kuaminisha Umma kuwa Tanzania ni ileile.

Benki ya dunia wamejibu kwamba Tanzania ya awamu ya 5 sio ileile kwani sasa ipo uchumi wa kati!

#Pili ni hoja kwamba mikopo nafuu itapungua kwakuwa tumeingia uchumi wa kati.

Ingawa ni kweli kwamba mikopo nafuu itapungua lakini athari yake ni ndogo kulinganisha na faida ya kupanuka kwa wigo wa kukopa mikopo ya kibiashara ambayo kawaida haiambatani na masharti ya kikoloni.

Ukweli huu unathibitishwa na hoja mbili, kwanza ni kiasi cha misaada na mikopo hiyo kuendelea kuwa sehemu ndogo sana ya mapato ya yetu!

Tazama utekelezaji wa bajeti ya mwaka jana 2019/20, ambapo katika mapato yote yaliyofikia Trilioni 26 kufikia Mwezi Aprili2020, kiasi kilichotokana na misaada na mikopo nafuu kilikuwa Trilioni 2.4 sawa na asilimia 9% tu ya Trilioni26.

Hivyo kupungua kwa misaada na mikopo nafuu athari yake ni ndogo sana kwakuwa mwenendo(trend) wa kupungua kwa misaada na mikopo nafuu upo hivyo kwa muda sasa!

Zaidi kutanuka kwa upatikanaji wa mikopo ya kibiashara ambayo siku zote haiambatani na masharti ya kikoloni ni faida na zaidi ni heshima hasa kwa Serikali kama ya JPM iliyojizatiti kujenga msuli wa kujitegemea.

Serikali ya JPM inajenga msuli wa kujitegemea kwa uwekezaji mkubwa sekta ya miundombinu ya kiuchumi ya usafiri, ujenzi na umeme.

Sanjari na hayo, uwekezaji mkubwa kwenye rasilimali watu kama inavyonekana katika sekta za Elimu, Maji na Afya.

#Tatu, Hoja kwamba kipimo cha ongezeko la pato la mtu (per capital income) sio uhalisia katika maisha halisi. Hoja hii ni sahihi kwa mtazamo wa jumla katika taaluma ya uchumi .

Hii ni kwasababu inawezekana uchumi wa nchi husika sio jumuifu au sehemu kubwa ya kinachozalishwa kinaishia akaunti za mafisadi nje au matumizi makubwa yanafanyika kwenye mambo yasio na faida sana kwa wananchi wake.

Mfano ni Marekani inavyotumia sehemu kubwa ya pato lake kwenye vita badala ya kuboresha maisha ya watu wake na hivyo kufanya kuwa Taifa la saba duniani kwa ubora wa maisha ingawa linaongoza kwa ukubwa wa uchumi duniani ikiwa linamiliki asilimia 20% ya uchumi wa dunia.

Hata hivyo hoja hii kwa Tanzania chini ya JPM haibebi sura hiyo kwasababu kwanza, Tanzania ndio nchi inayongoza kwa uchumi jumuifu Afrika kusini Katikati nchi za Africa zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara.

Mantiki hii inamaanisha kwamba tofauti ya aliyenacho na asiyenacho ni ndogo( Ripoti ya World Economic Forum 2018).

Zaidi Tanzania inafanya vizuri sana duniani katika usimamizi wa matumizi ya Serikali ndio maana ikatajwa kuwa Taifa la 28 kati ya nchi 186 duniani kwa udhibiti wa matumizi ikiziacha mbali Kenya 70, Uganda100, Msumbiji 69, Malawi 106, Botswana 37 ( rejea ripoti ya WEF: Executive Opinion Survey 2019).

Nchi yenye picha hii ni wazi tafsiri ya ongezeko la pato la mtu inakuwa na maana pana kwa watu wengi kama nilivyoeleza .

# Nne, Hoja kwamba hakuna uwiano wa kiasi cha fedha za bajeti kilichotumika ndani ya miaka5 kulinganisha na ongezeko la pato la mtu mmoja mmoja.

Hoja hii ina makengeza kwasababu matokeo ya uwekezaji mkubwa unaofanywa kwenye miundombinu mikubwa kama reli ya kisasa( SGR), Mradi wa umeme wa Stirglers Gorge hata uwekezaji mkubwa kwenye miradi ya Elimu, kufufua shirika la ndege, meli na bandari, matokeo yake sio ya muda mfupi (payback period).

Kwenye Sayansi ya uwekezaji, muda wa kurejesha ulichowekeza na hata faida vinategemea aina ya uwekezaji.

Ukiwekeza shamba la mchicha unaweza kurejesha mapato ndani ya mwezi. Lakin ukiwekeza shamba la miti utarejesha baada ya miaka10 na kuendelea lakin umejenga msingi endelevu.

Sasa pengine kuna watu walitamani nchi hii tuijenge kwa falsafa ya uwekezaji kwenye mchicha. Hakuna nchi iliendelea kwa falsafa hiyo. Iwe Vietnam, Malaysia, Korea kusini, Singapore, nk.

Mawazo ya namna hii yakipewa nafasi kwa kinachoitwa demokrasia tunaweza kugeuka Taifa la wachuuzi kwa nusu karne nyingine. Haya ni ya kukemea!

#Tano ni hoja kwamba mafanikio ya kufikia uchumi wa kati sio ya JPM kwani watangulizi wake walifanya pakubwa.

Hoja hii ina mapungufu ya aina mbili, kwanza kumekuwa na hoja kwa muda mrefu binafsi nakubaliana nayo;

kwamba nchi yetu ilichelewa sana kwani nchi tulizokuwa sambamba nazo kiuchumi hadi kufikia miaka ya 1990, nchi kama vietnam ( ilikuwa na uchumi wa $6.5bn sisi 4.5bn mwaka 1990- kwa ripoti za Bank ya dunia), leo zimeshatupita zaidi ya mara nne( Vietnam $260bn wakati Tanzania $63bn).

Takwimu hizi zinathibitisha kwamba tulikotoka hatukufanya vema. Mimi ninaamini miongo kadhaa tulipoteza na ndio siri ya kuachwa.

Lakini nina amini kwamba kwa msukumo mkubwa tulionao sasa katika kujenga miundombinu ya uchukuzi na umeme, niwazi haitachukua miongo mingi kabla ya Taifa hili kucheza ligi moja na waliotuacha tulipozubaa.

Mapinduzi anayofanya JPM leo walianza kufanya wenzetu miaka 30 nyuma, sisi tulibaki na mawazo bila kuyatekeleza ndio siri ya kuachwa.

Sasa leo yanatekelezwa anakuja mtu na mawazo yaleyale ya kujenga uchumi kwa falsafa mchicha kama nilivoeleza hapo juu.

Mapungufu ya pili ya hoja hii ni wivu tu wakisiasa kama vile mtu aseme mfungaji fulani asingefunga kama beki asingeanzisha pasi ikaenda katikati ndipo akapewa na kisha kufunga.

Sipuuzi mchango wa awamu zilizotangulia lakini sioni kwanini kasi kubwa ya msukumo huu wa kulazimisha sasa!Mzee Mwinyi, Rais mstaafu alipata kusema kila zama na kitabu chake.

# Sita:mfano wa kutumia uamuzi wa kununua ndege 11 kwamba hauna tija kwenye uchumi ni ukosoaji uliokosa nguvu kwa muda mrefu. Nchi hii imezungumza kwa miongo kadhaa kuhusu haja ya kufufua sekta ya uchukuzi ikiwemo shirika la ndege,usafiri wa maji na reli.

Tafiti zimeonesha mara kadhaa kwamba kwa bahati ya nafasi ya Tanzania kijiografia, tukiwekeza kwenye sekta ya uchukuzi kikamilifu, mchango wake utakuwa mkubwa sana kuliko sekta yoyote ( Rejea Poverty & Human Development Report 2008).

Kamati ya Bunge ya Miundombinu, katika Bunge la 11 ambalo nilikuwemo, walitoa taarifa na kurudia mara kwa mara kwamba zaidi ya asilimia 60% ya pesa anayoitumia mtalii inaishia kwenye usafiri wa ndege.

Sote tunajua Utalii ni sekta kinara kwa fedha za kigeni nchini. Sote tunaelewa umuhimu wa fedha za kigeni kwa dunia ya kisasa iliyounganishwa (modern globalized world).

Kwa upekee wa nafasi ya Tanzania kijiografia Africa, maamuzi ya kufufua Shirika la ndege isingepaswa kuwa hoja ya kubishaniwa.

Pengine hoja ingekuwa tunalifufuaje. Kwa mfano uamuzi wa kukodi ndege mbovu kwa dola milioni43, ndege ambayo ilifanya kazi miezi 6 na miezi 37 ikawa gereji haikuwa mkakati sahihi (rejea CAG ripoti ya Aprili 2020).

Lakini mkakati wasasa wa JPM kutumia dola 32m kununua bombardier mpya , kiasi ambacho ni pungufu ya tulichotumia kukodi ndege mbovu huko tulikotoka, ni mkakati ambao kila mwenye mapenzi ya nchi hii ingetosha kupongeza na kukiri kwamba tumetoka mbali!

# Saba: Hoja kwamba Serikali ina uhaba wa mafanikio ndio sababu imefurahia taarifa ya Benki ya dunia kuipandisha Tanzania daraja kuingia kundi la uchumi wa kati ni upofu wenye msukumo wa kisiasa.

Serikali ya awamu ya tano inarekodi kubwa zisizobishaniwa ( undisputeble) kitaifa na kimataifa. Rekodi ambazo kila anaejua kinachoendelea duniani anazifahamu.

Rekodi za ndani kama kugharamia elimu bure, kuvunja rekodi ya mapato na mauzo ya nje sekta ya madini, rekodi ya kuongeza kusambaza umeme vijijini zaidi ya vijiji 7000 ndani ya miaka 5 ( 2015-2020) na kufikia vijiji 9300 kutoka vijiji 2018 mwaka 2015 ni rekodi.

Rekodi ya kuongeza usambazaji maji vijijini kutoka asilimia 47% mwaka 2015 mpaka asilimia71% ni rekodi.

Rekodi ya kujenga hospitali 10 za rufaa za mikoa, kuongeza fedha za dawa na vifaa tiba kwa zaidi ya asilimia 700% kutoka billioni 31 mwaka 2015 mpaka billioni 269 ni rekodi.

Kifupi kasi ya kupungua kwa umasikini wa huduma ni kubwa sana. Tulikotoka gharama za huduma za afya zilikuwa kubwa maradufu kwa sababu sehemu kubwa ya gharama ilihusu kuifikia huduma yenyewe kuliko gharama halisi ya huduma kutokana na umbali wa kufikia na zaidi upatikanaji dawa.

Iliwezekana kutumia elfu 80 kwajili ya usafiri , Malazi na chakula kuifuata huduma ambayo unailipia elfu20.

Natamani wachumi zaidi wafanye Tafiti eneo hili la namna umasikini wa huduma ulivyopungua kutokana na ukaribu wa vituo vya kutolea huduma na ongezeko la upatikanaji wa huduma yenyewe kwa maana ya dawa.

Ujenzi wa reli, Meli, Shirika la ndege, mradi mkubwa wa umeme sanjari na kuliondoa Shirika la Tanesco kwenye mikataba mibovu hata kulifanya lijitegemee zote ni rekodi.

Tanesco kwa miaka 30 ilikuwa jini nyonyadamu kwa uchumi wa Tanzania. Kuna wakati gharama za kuliendesha ililingana na Bajeti ya Zanzibar kwa mikataba ya 'kijangili'. Kufyekwa mikataba ya hovyo na udhibiti ni mapinduzi makubwa.

Sijui mtu anayesema Serikali hii inauhaba wa rekodi alitaka rekodi zipi zaidi ndani ya miaka5.

Hizi nimetaja chache tena za ndani , lakini kimataifa, JPM ameshatengeneza rekodi lukuki kama nilivyoeleza wiki iliyopita kwenye makala yangu ya JPM NA REKODI SABA KIMATAIFA.

# Nane. Nihitimishe kwakusema kwamba nchi hii bado inasukwa. Ndani ya miaka5 , JPM ameisuka pakubwa sana. A Kauli mbiu za kisiasa za "Kazi na Bata" hazitofautiani sana na mzaha wa Mzee Cheyo mwaka 1995 ya KUJAZA WATU MAPESA. View attachment 1499026
Wacha porojo Kafulila " weka tume huru ili wananchi tuamue.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom