Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
P
Wanajanvi.
Magufuli ni kiongozi mwenye kutegemea siasa za ghilba, uongo na danganya toto. analazimisha kupenda.
Juzi akitoka msibani alikuja kwa gari. Kama ilivyokawaida kwa wapambe wakamwandalia mikutano (amesimamishwa na wananchi ?). alikwenda mbali zaidi kwa kujiandalia zawadi ya kuku mwenyewe ili ionekane kapewa na wananchi. Hilo sio kweli. hata ukimuona tu yule kuku utabaini kwamba SIYO WA KIENYEJI. ni kuku wa kufugwa wengine wanawaita wa kizungu. kwanza ni safi kuliko hawa wanaochakula.
mwananchi wa kawaida kabisa hawezi moja kwa moja atoke huko alikotoka apelike kuku kwa mkuu wa nchi Tena anayelinda kwa mitutu ya bunduki na uzio wa chuma sio rahisi.
Hoja ni je watu wa kusini wana nini cha kujivunia toka kwako hadi upewe kuku kama zawadi badala ya zawadi kama ule moshi?
Uliwapora korosho zao mpaka leo wanadai, hapakuwa na sabababu ya serikali kupora korosho za watu wanaoitwa wanyonge ikijua haina pesa za kuwalipa (Mpaka leo wanadai) na kila akienda huko hutangaza kwamba zimeingizwa BL 21 ili kuwalipa kumbe uongo.
Aliingia madarakani kukiwa na zao la mbaazi. tena ikiwa bei juu kwelikweli. Badala ya kuimarisha akaanza kuingiza mambo binafsi na kina MANJI waliokuwa wanunuzi wakubwa. leo mbaazi imekufa kifo cha kawaida kabisa huku aliyeua akijiita kiongozi wa wanyonge
Akiwa Mkuranga aliandaliwa KADA Wa chama kuuliza swali (MKURANGA NAKO KUNA KOROSHO). ni MKURANGA ambako wananchi waliuwawa kwa kisingizio cha VITA ya ugaidi mpaka leo hakuna gaidi aliyekamatwa. miaka 3 nyuma wananchi wa huko walilazimika kutembea na VITAMBULISHO kwenye ardhi ya nyumbani nenda Rufiji leo ukaambiwe watu walivyo vunjiwa utu wao, utashangaa. hivi familia ya Anzory Gwanda inaweza kutoa jogoo na kumpa Magufuli?
swala la Mgogoro wa Ardhi mkuranga sio la leo lilikuwepo tangu 1960. wewe ulishawahi kuwa waziri wa ardhi kwanini hukulitatua hadi uwe raisi? ulaghai huu.
Nampa hongera motto yule alikuuliza swala la MADAWATI hakika ulikosa majawabu nina hakika yule hakupangwa alikustukiza.
Ndugu zangu hata hapa Dar kuna shule nyingi tuu watoto wanakaa chini zipo na Magufuli anazijua. badala ya kumaliza kabisa tatizo la madawati yeye ananunua MIDUBWASHA/NDEGE na kuipaki pale JKN
Hata iweje Aliyeporwa KOROSHO hawezi kumpa mporaji wake zawadi ya JOGOO
Ni GHIRIBA TU
Peleka upumbafu wako huko majuha wenzio! Hizo tuhuma zako dhidi ya Magu ni za kubumba! Watz hatuhitaji lecture za kipumbavu! Tumeshampima Magu na tumeridhika pasi mashaka Kuwa anatufaa na ni mtendaji zaidi...siyo Kama wapuuzi wenzenu huko kuchakuchwa ni makelele kwa Magu lakini ukiwauliza waonyeshe chema walixhofanya ktk nafasi zao unakuta upuuzi mtupu na Sacco's zao! Hao ndio mnatumia nguvu kubwa kuwanadi! Niwape pole maana mnayofanya yote watz tunaelewa na tutawafundisha SoMo Oct 2010!
Magu ni zawadi ya Mungu kwa watz walioomba kwa miongo kadhaa Sasa!
 
Baada ya kuuwa soko la mbaazi akaamua kuua kabisa soko la korosho. Mbazi tulizolima mwaka 2017 ziliozea shambani tulishindwa hata kuzivuna. Mnunuzi mkuu bwana Manji aliwekwa maabusu miezi kibao soko likafa na mkuu akafurahi sana. Korosho akatuma wanajeshi waje kutunyanyang'anya tukawa tunatakiwa kuonyesha mashamba utafikiri kuna mtu amelalamika kaibiwa korosho zake.

Na kwavile mzee wa malofa kafa maana alitegewa kulazimisha kutangazwa kwa kura zisizo halali. utaambulia Moshi kama ule wa Nachingwea.
 
Umempima na mama yako. Kenge wee
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Hatuwezi kuwa na Rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli, hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya Rais au Waziri Mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu.

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je, anajua jinsi ya kututoa?! Anajua anakotupeleka?

Nimejitahidi kuangalia Bunge ili nione labda Mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Ametutoa tulipokuwakwenda uchumi wa kati. Wewe hii huioni!
 
Hakuna mabadiliko mepesi usipotaka kwendana na kasi ya mabadiliko lazima utaona kila kitu unaonewa, Tumpe muda kwani alipotutoa ni pabaya mno kuliko alipotufikisha, Tunatakiwa kumuunga mkono kwa sababu anapambana sana kwa maslahi ya Taifa letu.
 
1. Nimepita sehemu pale morogoro nikakuta barabara ya vumbi imekwanguliwa vizurii lakini baada ya km kadhaa barabara ni mbovu sana. Nikauliza wenyeji kulikoni greda liliishia hapa wakati huko mbele barabara ni mbovu nikaambiwa huko mbele diwani ni wa upinzani. Nijachoka

2. Hivyo nikavutiwa kufanya kautafiti kadogo kwa kupita maeneo mengine kadhaa nikagundua sehemu zingine nyingi ni hivyo hivyo. Kipande cha lami kinajengwa na kuichia njiani kisa mbele ya hapo diwani ni mpinzani.

Kama hali iko hivi inchi nzima basi mjue mchawi wa kukwamisha maendeleo ya inchi hii ni serikali zinazoundwa na CCM hasa awamu ya tano.

Nimeamini kisemwacho, CCM haina nia ya dhati kuleta maendeleo ya inchi zaidi ya kufikiria kutawala.

Wananchi wote maeneo yote ya uwakilishi wanalipa kodi iweje miradi ya maendeleo ipelekwe kibaguzi?

Mchawi wa maendeleo ya inchi hii ni ccm na haina nia ya dhati kuwaletea watanzania maendeleo zaidi ya kufikilia kutawala.
 
Hakuna mabadiliko mepesi usipotaka kwendana na kasi ya mabadiliko lazima utaona kila kitu unaonewa, Tumpe muda kwani alipotutoa ni pabaya mno kuliko alipotufikisha, Tunatakiwa kumuunga mkono kwa sababu anapambana sana kwa maslahi ya Taifa letu.
Nakubaliana na ili mkuu...
 
Baada ya kuuwa soko la mbaazi akaamua kuua kabisa soko la korosho. Mbazi tulizolima mwaka 2017 ziliozea shambani tulishindwa hata kuzivuna. Mnunuzi mkuu bwana Manji aliwekwa maabusu miezi kibao soko likafa na mkuu akafurahi sana. Korosho akatuma wanajeshi waje kutunyanyang'anya tukawa tunatakiwa kuonyesha mashamba utafikiri kuna mtu amelalamika kaibiwa korosho zake.

Na kwavile mzee wa malofa kafa maana alitegewa kulazimisha kutangazwa kwa kura zisizo halali. utaambulia Moshi kama ule wa Nachingwea.
Nadhani nivyema kuwa mkweli kuliko kujitoa ufaham...kusu korosho lengo lilikuwa nikwafaida ya mkulima....hatakama majibu hayakuja kwa kiwango kile bado haiondoi adhima yake....siasa za uongo hazina nafasi akuna wajinga sikuizi
 
Watu wote;-
  1. Tuliopotelewa na ndugu zetu kwa utekaji
  2. Tuliopata hasara katika mazao yetu, mfano korosho
  3. Tuliopotelewa na ndugu zetu wakakutwa kwenye viroba
  4. Tuliosomesha watoto halafu hawajapata ajira
  5. Tulioumizwa na ubaguzi, matusi na dharau
  6. Tuliofilisika kwa sera ya "matajiri wataishi kama mashetani"
Sote tuungane tumnyime kura arudi kwao.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom